Kipindi cha talaka/divorce

Kipindi cha talaka/divorce

Jiulize swali;
Kwa nini napewa/naitaka hii talaka?? Kama mtu wako kakuchoka, angalia pia kilichomfanya kakuchoka. Penzi halizeeki bali hukua kila siku. Ilitokea nini?? Habari za kuvumilia ati hili nalo litapita tu sio kweli. Hatuvumilii kwenye penzi bali huwa tunalidai penzi letu. Ukifika pale mahakamani kataa hiyo talaka kuwa kama yeye kakuchoka, wewe hujamchoka.
Hizo dhiki unazoziona sasa ndio zitakuja kuwa msingi wa raha, furaha na amani baadaye. Kitu pekee cha kuchunga ni kuwa, isijekuwa pendo lako limeingiliwa na vijimambo vya nje. Hakuna ugomvi usio na suluhu. Mahakama itawapeni muda wa kujitathmini. Huo ndio muda wako wa kujitathmini. Kama jamaa amezamia kwa nyumba ndogo, wala usimpigie kelele. Mpe haki yake siku huko nyumba ndogo kuna matope tena kwa ufundi mkubwa bila kelele na kebehi. Wanawake wengi midomo yenu ndio inawaponza.
Mwisho jiulize; Labda alikukuta bado msichana, akakutoa usichana wako, amesha kukutotoa toto 2, 3, 4. Leo umesha kongoroka na ukichanganya na unayosema mateso kama ukiingia bafuni huwa unahofu kujianglia. Sasa unataka kwenda wapi?? Nasema; Komaa naye hadi bp imuue kwani akienda kazini akirudi akukute na bonge la tabasam na sifa kem kem kuwa hakuna dume ka wewe uliyenitoa usichana wangu. Imba hadi sikio lake liizoee sauti yako. Hakuna talaka kwa mkristo
Da mange kaachwa na haohao waliouleta ukristo.
 
Kwanza inabidi hizo tofauti zenu ziwe zimefika kwa wasimamizi, wakashindwa kutatua, wazazi nao wawe wameshirikishwa wakashindwa kusuluhisha. Baada ya hapo unaenda ngazi ya wazee wa kata (afisa mtendaji) mtaitwa na kusuluhishwa, ikishindikana mnapelekwa kwny baraza la usuluhishi nao wakishindwa ndo mnaenda mahakamani.

Mdai talaka anapeleka shauri mahakamani, alafu anapewa barua/taarifa kumpelekea mtalikiwa ya kuitwa mahakamani. Siku ya mahakama kusikiliza kesi yenu, mnaulizwa maswali mengi tu ikiwemo kwa nini mna talikiana/kwa nn mdai talaka anataka talaka, alafu wazee wa usuluhishi pale mahakamani wanatoa maoni yao..

Kama mna watoto mnaulizwa mtawatunzaje/ wanaenda kuishi na nani kati yenu. Mnaulizwa mali mlizochuma pamoja na jinsi ya kugawana then mkishakubaliana hukumu inatoka siku hiyo hiyo na talaka inatoka. Ila wengi wanachukua muda mrefu kutokana na mgawanyo wa mali maana wengi hawako tayari kugawana.

Khs kumove on, hapa inategemea na wote wawili, je mmejiandaa na kutengana? Kama unashindwa ku move on inabidi mtengane kwa kipindi chote cha process, mpeane nafasi. Hii itasaidia kuzoea hali ya utengano.
Talaka mahakamani duh! Hili no janga kite huko? Ndiko mlikooana hebu tuwe serious jamani.
 
Back
Top Bottom