Kipindi cha Star TV; Tuongee asubuhi na Donatus Rutagimbwa

OMEGA

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
693
300
Kwa mujibu wa taarifa zake binafsi katika facebook,huyu mtu ni kada wa CCM, mwanasheria, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii ,alisomea Mpwapwa high school na ni graduate wa UDOM.Pia aliwahi kukaribishwa star TV tuongee asubuhi tarehe 3/7/17 ,5 /7/17 na 13/7/17.

Leo hii kakaribishwa tena kipindi cha tuongee asubuhi,sina kawaidaya kuangalia iki kipindi lakini leo nilivyofungua clouds na kumouna yule dogo aliyekuwa fiesta amerudi ,ambaye aliwahi kusema watu wa aina ya TL ni wa kuuwawa nikakosa appetite ya kipindi nikajikuta nime tune star TV.

Kwa kweli huyu jamaa wa star TV leo ameboa sana na kaonyesha uwezo mdogo sana wa kuchambua mada ,eti kadai mbunge wa Bukoba vijijini na meya wake wana akili ndogo sana sababu wanatoka CHADEMA na wanashindwa kubuni kiwanda cha kukoboa kahawa kama alivofanya mbunge wa Mishenyi ambaye ana akili kwa sababu ni CCM.Akamalizia na kusema kuwa watu wa Bukoba ana amini hawatarudia makosa mwaka 2020 kuchagua watu wasio na akili.

Nimetafakari sana na kujiuliza hivi star TV wanavyo karibisha watu wa aina hii uwa wamekosa kabisa watu wenye upeo na wenye lugha za staha katika vipindi vyao? pia nimejiuliza uwezo wa graduate wa vyuo vikuu siku hizi,hivi kweli huyu ni mwanasheria,hivi amesoma na kuhitimu kweli? wanaomjua vizuri huyu mtu naomba watusaidie,mimi nadhani hayuko ok kwenye medula oblangata.
 
Back
Top Bottom