Kipindi cha SKONGA, EATV. Kitendawili kinachohitaji Majibu

Elimu ya kizazi hiki ishatupwa chooni... Mungu atatuuliza kuhusu hili siku moja
 
Kizazi cha leo hakina mwelekeo wa ubunifu katika maisha ya kila siku, wenye vipaji wanazidi kupungua kadri Muda unavyosonga mbele, imagine kizazi cha miaka ya kuanzia, 90 wakati huo technology ya Tehama ilipoanza kukua kwa kasi ndo Hao ambao wameanza kushika ofisi na taasisi za maamuzi ni hatari, kila mmoja kamba masikioni siyo nje tu hadi ofisini, kisa miziki na mapicha au mipasho, wanafunzi ndo usipime, baba, mama, Dada, kaka kila mmoja yupo na kiselula hapo home, hakuna kuongea, TV channel 5 au sinema za wanga, Hawa wamechanganyikiwa kutoka labda mitandao iwe inazimwa iwashwe saa 5 usiku.
 
Teachers are discouraged by the community, teachers are paid less, what do you expect?. Lakini pia wanaidai serikali hela ya likizo, mishahara ,matibabu na masomo. Walimu hawana morality sijui ni mgomo baridi
Salute boss!

Mbona umeegemea upande mmoja wa walimu?. Mwanafunzi anamtegemea Mwalimu kwa 25% pekee. Hizi 75% zinazobaki unazielekeza wapi?.

Karibu.
 
Huuu ukweli aiseee hawa ndo wanachosha yaan mtu anaulizwa hata Africa Mashariki ina nchi ngapi,ila yuko form four hakujui
Na hivi wanavyoambiwa kuwa wanasoma bure sidhani kuwa hata wanajua Tanzania ina mikoa mingapi eti kiongozi anasema watoto wanasomeshwa bure ..kweli NA UNATEGEMEA NINI
 
Mleta mada umenena mambo nyeti sana hadi umenikumbusha siku moja wanafunzi wanaulizwa majina ya wanyama waliko kwenye shilingi mia moja hawajui. Inasikitisha sana, siasa zimeingia kwenye elimu yetu, viongozi wanatoa matamshi ya kufurahisha wazazi ili waweze kupata wapiga kura kesho, nilimsikia mama mmoja kipindi limetokea lile tukio la walimu wa mbeya waliomchangia mwanafunzi kwa viboko, alikuwa kiongozi fulani serikali, alikuwa anatoa ufafanuzi wa kutia adhabu kwa wanafunzi, nilisikitika aliposema eti anayepaswa kuchapa ni mkuu wa shule tu, km mwalimu mwingine unataka kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi basi uombe kibali cha kumuadhibu kutoka kwa mkuu wa shule tena kwa barua, alafu ukiruhusiwa basi umchape viboko na visizidi vitatu. Ukitafakari utaratibuu huu ni wa kupotosha na kuzidi kuwapa watoto kiburi hatimaye hawaonyeki tena mwisho ndo tunakuta mtoto wa kidato cha nne hajui hata rangi za bendera ya Taifa lake.
 
Walau umetambua kitu cha muhimu sana katika hicho kipindi mkuu na hii ni aibu kwa tasnia nzima ya elimu nchini.
Nilishangaa sana juzi kati mwanafunzi wa kidato cha tatu kuulizwa nini kirefu cha USD akaishia kujibu eti United Socket alafu akishindwa kuendelea.

Binafsi lawama zangu za kwanza napeleka kwa wazazi/walezi. Asilimia kubwa ya wazazi/walezi siku hizi wamekuwa wa kushindana kupiga selfies na kupost facebook, instagram etc, etc na pia wengi wa wazazi hawatilii maanani maendeleo ya watoto wao mashuleni wala kufatilia nini anachokifanya mwanafunzi shuleni. Mbaya zaidi wazazi/walezi hawana msaada mkubwa kwa watoto wao hata pale mtoto anapokuja na homework au tatizo lolote linalohitaji msaada.

Lakini pia serikali pia imechangia sana katika kudidimiza elimu yetu. Na hili linakuja pale ambapo walimu wana malimbikizo ya muda mrefu sana kitu kinachowakatisha tamaa na motisha ya kufanya kazi.

Kazi ya ualimu sasa hivi haina thamani tena. Miaka ya nyuma ualimu ulikuwa na heshima yake mtaani. Ulikuwa ukisema mimi ni mtoto wa mwalimu flani au mzazi wangu ni mwalimu basi wenzio wanakutamani.

Bahati mbaya sana sasa hivi hata kwenye vyuo vyetu course za ualimu zinaonekana ni za wakosefu. Mtoto akifanya vibaya shuleni akija kuhangaika huku duniani kutafuta ajira akakosa utaskia wanaulizana yaani uwekosa hata ualimu jamani?

Mbaya zaidi wanaoenda kusomea ualimu ni wale ambao matokeo yake hayaridhishi hata kidogo. Kwa lugha nyepesi wale ambao alama zao za ufaulu hazikidhi mahitaji ndio wanao kimbilia kufundisha hivyo kwa mtaji huu tusitegemee kuzalisha wanafunzi bora.

Na hali iko hivyo hadi vyuoni. Nakumbuka wakati nikiwa mwaka wa pili chuo, mwalimu wangu wa course moja inaitwa sociology of family & marriage hakuwa anaweza kunyoosha walau sentensi tatu zilizonyooka kwa lugha ya kiingereza lakini ndio hvyo.
 
Nilicheka sana nyumbu moja ya form two inaulizwa kutoka A mpaka Z ni herufi ngapi inajibu 20.. nilitamani niitandike makofi pumbavv..!!
 
Lowasa aliona mbali sana
1. ELIMU

2. ELIMU

3. ELIMU

Cha ajabu bado kuna wengi hawajamuelewa hadi leo alimaanisha nini...!
 
Mkuu umesema ukweli mtupu,binafsi nikiangalia skonga mpk nasikia kusisimkwaa kwa ule upududu
Sijui tunakosea wapi inasikitisha sanaa
 
Mkuu kuna mengi yamechangia. Tukisema ccm imechoka tunatukanwa ila ukweli ndo huo. Utakumbuka kuna wakati ccm hawa walibadilisha syllabus eti wakafuta bookkeeping na kilimo kisha physics na chemistry kikawa somo moja na maujinga mengine yakafanyika baraza la mawaziri kikabariki ngoma ikashushwa kwenye utekelezaji. Kama uliwahi kufuatilia au kama kuna waalimu humu jukwaani watajua nasema ukweli. Combinationa ya ECA iliwahi kupotea miaka kama 2 au 3 hv yaani ikawa ngumu hakuna mtoto aliyeenda eca na walimu wa masomo ya biashara wakajikuta wanalzimika kufundisha civics lkn ndo serikali ya ccm hyo.

Lkn leo bado maujinga yapo mengi. Kama mnataka mcheke tafuta mwl wa shule ya msingi muulize je wanatumia kitabu gani kufundisha watoto darasanai??? Kama ni mzalendo utasinoneka au hata kutokwa na chozi ila kama ni bongofleva utapotezea. Ukweli wana vitabu kama 5 hv yaani sasa sijui mtoto anakua kwa standrd zipi. Halafy tunaita waalimu na maafisa elimu kuwaweka kitimoto ati kwann watoto Dar wanafeli sana na mtafanya mpango gani wasifeli! Huu ndo upeo wa viongozi wetu.

Bado sijaona kiongozi mwenye nia ya dhati kunusuru vijana wetu taifa letu sijaona. Mama Joyce Ndalichako naye kama kama walewale. Amechakachuliwa na wanasiasa hana issue tena.
 
Tutawalaum buree tatz wanatuon kk zao tumemalz vyuo hatuna kaz au tunafny mishe za wasio na elim ss ile morali ya kusom inapungua sn.
 
nakumbuka yule dogo alienda kwenye shule ya mama salma kikwete maswali yote aliyouliza walipata wanafunzi nikagundua dogo alipewa miongozo ili asiharibu jina la shule ila ata hivyo yale maswali yanaulizwa kwa lengo ukose japo sio magumu
lakini ata hivyo bado kiingeleza ni kigumu nakumbuka kipindi nipo shule nilikuwa nakosa nafasi ya kuchangia mada sababu ya lugha mwish nikawa na hali yakutojiamini
nafikiri ndo hali inayowakumba hawa madogo zetu kushindwa kujiamini kuongea mbele za watu
 
Mungu Ni Mwema Sana

Yaani Bahati Nzuri Sana Watu Hukifuatilia Sana Hiki Kipindi Na Kujionea Kila Kitu Hadharani

Yaani Nafikiria Lile Tangazo La Malaria Kuhusu Bwana Machafuko Alipoambiwa Hana Malaria
Akawa Mkali Sana Kuwa Malaria Yake Anaijua Inaanzia Tumboni. .


Zama Kweli Zimebadilika Sana
Yaani Mwanafunzi Akiulizwa Maswali Ya Ufahamu
Mfano Kila Mkoa Na Umaarufu Wake Wa Kuzalisha Mazao Hawajui
 
Katika dunia ya leo uelewa wa lugha mbalimbali unachangia pakubwa katika kuimarisha jinsi mtu anavyo jifundisha na kuelewa mambo mbali mbali kwani ulelwa mambo mengi unatokana na mazingira unayoishi. Media zetu zimekomalia sana kwenye fani ya burudani na kutokana na wengi wa watu wetu kutofuatilia au kutoelewa mambo yanayopeperushwa kwa lugha zingine wanabaki kubugia kile kinachosambazwa na media zetu.
Kuna vyanzo vingi sana vya elimu nje ya mfumo wa shule kama Youtube, websites, blogs, gazeti, majarida ambazo unakuta vipo kwenye lugha tofauti na kama hauzielewi, yanakupita tu.
 
Back
Top Bottom