Kipindi cha SKONGA, EATV. Kitendawili kinachohitaji Majibu

Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
1,518
Likes
1,984
Points
280
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
1,518 1,984 280
Sabalkheri wana Jamii Forums?.

Naanza kwa usaili na nitamaliza pia kwa usaili. Usaili ni kuuliza masuala ya msingi. Kuanzia unachokiona, unachokisikia, unachokidhania, unachokishika na kadhalika. Hivi ndivyo walivyofanya kina Socrates, Pythagoras, Galileo Galilei, Fantz Fanon, Mwl J.K.Nyerere na orodha inaendelea...

Huu waraka ni Nasaha kwa Wizara ya Elimu, mzazi, mlezi, kaka, dada na Jamii yote ya Watanzania wenye tafakuri za kina na wenye mapenzi ya dhati kwa Taifa lao la sasa na la baadaye. Maagizo haya yametoka kwa Mungu. Ni sharti Mzazi amlee mtoto katika njia impasayo kwakuwa (Mtoto) hatoiacha kamwe hata atakapokuwa Mzee ( Mithali 22;6). Nb; Silaha zinaandaliwa wakati wa amani na si wakati wa vita.

Hivi karibuni, miezi kadhaa ilopita nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu uso na mashaka kipindi cha SKONGA kiendeshwacho katika luninga kupitia East Africa Television (EATV).

Nikiandikacho hapa ni ushuhuda wa nilichokishuhudia na ninachozidi kukisaili (siyo kuhadithiwa) kama pengine ambavyo huenda ukawa ndiyo kwanza unalisikia jina hili la kipindi cha SKONGA katika maandishi haya. Ninatazama kipindi hiko na ninazidi kukitizama kila panapobidi. Kama pia uliwahi kukitizama ni vizuri lakini pia kama hukuwahi kukitizama ni vizuri pia. Nitajaribu kudokeza kidogo ili sote tupate taswira kamili juu ya kipindi hiki.

Kiekweli, bila kupepesa ukope wala kumungunya maneno kuna walakini katika Taasisi yetu ya Elimu, Taasisi ya Familia na Taifa kwa ujumla. Kuna kasoro katika mitaala yetu ya kielimu. Silabasi zetu hazimuandai Mwanafuni kukabiliana na mazingira ya wakati wa sasa na ujao.

Kuna wakati wa Q & A (Questions and Answers) katika kipindi hiki cha SKONGA. Kiukweli hapa ndipo ninapochoka juu ya wanafunzi wetu. Round knowledge ya mambo anuai, current news na kadhalika ni baadhi tu ya mambo yanayoifanya kipindi hiki kiwe cha vichekesho na pengine si kusadifu lengo la kuanzishwa kwake.

Tuna upungufu Mkubwa sana wa Maarifa (General knowledge) vichwani kwa Wanafunzi wetu. Si wanafunzi wa S/Msingi, Sekondari na hata Vyuoni. Ni unazi, utunduwizi, ufisadi na ufisidi, umaamuma, ushabiki, utovu wa adabu, mbwembwe, ulimbwede, dharau na kedi, migoda mikogo na kadhalika.

Wanafunzi hawa hawafahamu mengi na wameridhika na hali walizonazo. Pengine hili si kosa lao, rafiki yangu mmoja anapenda kuniambia "Aliyetuloga keishakufa". Maswali yaulizwayo katika kipindi hiki ni ya kawaida mno ila wanayakosa makusudi. Tatizo ni nini?. Nani apewe lawama?.

Hivi mwanafunzi wa Kidato cha nne unashindwa vipi Square root ya 144?. Kirefu cha USD, TAZARA, BOT, EAC nk?. Humfahamu vipi Shaaban Robert?.

Mbona tunafahamu kirefu cha WCB, Washindi wa Miss Tanzania/World?. Mbona tunafahamu sinema za Kikorea na waigizaji wake?. Mbona tunafuatilia Fiesta kama tumerukwa na akili?.

Wanafunzi hawahawa wanamiliki simu za mkononi bila Mzazi/mlezi, Mwalimu kufahamu. Bora basi hata wangekuwa wanatumia simu hizi katika masuala ya msingi lakini wapi?..Ukibahatika kuzishika hizo simu utavunjika moyo sana na pengine atapandwa na presha (Bp) bure. Huku ni kufeli kwa Taasisi za kifamilia. Wazazi na Jamii kwa ujumla hawayaelewi madhara ya utandawazi ndiyo maana watoto wengi wanavutiwa na vikolombwezo hivi viso na mantiki..

Nilifikiria sana na kupata majibu kuwa "Ndiyo maana tu wepesi kufuatilia Big brother na Miss world kama tumerukwa na akili kuliko kufuatilia washindi wa Tuzo ya Nobel kwa mwaka huu". "Ndiyo maana tu wepesi kufahamu jina la Miss Tanzania kuliko jina la mwanafunzi aliyepata maksi za juu katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu". Kwanini wanafunzi wetu ni wahanga wa kufuatilia masuala yaso wajenga?.

Hizi ni Zama za 'Maarifa na Taarifa (Information age). Uelewa wa Mambo na ujenzi wa hoja ndivyo vinvyompa mwanafunzi nafasi ya kuwa bora zaidi ya mwingine na si usadikifu pofu wa kimakundi, ushabiki uso na mantiki na Umaamuma. Ukiona nafsi yako inataka kujua vilivyo bora zaidi sambamba na visomo, pima mashauri kwa kusudio lenye kuakisi mapenzi mema, nia kuu zaidi na upendo usio na mipaka juu yote na kila kitu.

Ni sharti Ubongo, Nafsi na Roho ya Mwanafunzi iJifunze si tu ya watu wa asili ya kabila moja, bara moja, rangi moja na kadhalika. Dunia yote na watu wake ni jamii yake na ni fahari za utu, mwangaza na fanaka kujaliwa kheri na kweli moja iliyo ni Uzima. Misimamo ama itikadi iso na staha si vya kupewa nafasi kabisa, ni sharti kuvibeza kwa akili na roho huku utunduwizi na ujinga vikifutiliwa mbali.

Ninachohitaji kukikusudia hapa ni kutoa ushauri kwa wahusika na haraka iwezekanavyo juhudi za makusudi zichukuliwe mapema ili kujinasua katika kile Prof Chachage alichokiita "Collective imbecilization".

Tusijipumbaze kihalaiki katika hili. Mwanafunzi achukue wajibu wake, Mwalimu na mzazi pia. Hakuna kutegeana katika hili. Utegevu ukiwepo, lazima pengo lionekane.

USHAURI.

Wazazi, walezi, kaka, dada na kadhalika waelekeze nguvu za ziada kwa walengwa (wanafunzi) kwa kuwawezesha kuwekeza zaidi katika Maarifa ikiwa ni pamoja na kuwasimamia vizuri katika matumizi yao ya muda. Kwenda katika sinema zisizo na tija, vibanda vya luninga, Kuzidisha michezo, kutazama luninga sana ni moja ya mambo ya kukatazwa na mwenye dhamana kwa mwanafunzi.

Ni vyema mwanafunze apate utulivu wa akili (Calmness of mind) walau kila siku ili ajiboreshe zaidi na zaidi. Kushughulika na mambo mengi yaso na tija ni kuuharibu ubongo wa mwanafunzi na madhara yake ni makubwa sana kwa siku za usoni.

Tuache kujenga Baa majumbani na badala yake walau tujikite katika ujenzi wa Maktaba (Library) kwa ajili ya kujisomea na kuongeza wigo mpana wa Uelewa kwa wanafunzi wetu na kujenga Taifa la wasomi wanaojitanua kimawazo.

Wanafunzi wanunue/ wanunuliwe vitabu vya kujisomea (Kiada na ziada). Siyo ununuzi wa vitabu vya mitaala ya shuleni tu. Vitabu nje ya mitaala (Riwaya, Tamthiliya, Ushairi nk). Mkusanyiko wa maudhui yapatikanayo katika vitabu vya Ushairi, Riwaya na Tamthiliya huweza kuwa na mchango chanya kwa wanafunzi kuliko magazeti ya udaku pamoja na vitabu visivyowajenga kimaarifa.

Hapa najua wengi watazungumzia gharama (cost) za vitabu ila ukweli ni kwamba, Tatizo siyo gharama ya kitabu. Tatizo ni gharama atakayoilipa mwanafunzi kwa kutokusoma kitabu. Sisi ni matokea ya yale tunayojifunza kwahiyo kama huna wigo mpana wa mambo basi wewe si chochote. Na kwa mujibu wa tafiti "Maarifa unayoyajua sasa yatakuwa yamepitwa na wakati baada ya miaka miwili hadi mitatu". Kila uchwao tujifunze na kujifunza tena.

Mithali 4 : 13
"Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako."
Proverbs 4:13
"Hold on to instruction, do not let it go; guard it well, for it is your life."

One Thing; #Be Wise with your comment(s).
 
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
1,518
Likes
1,984
Points
280
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
1,518 1,984 280
MKUU HIKI KIZAZI KILISHAJIFIA NDUGU.WATOTO KUANZIA MIAKA YA 1995 NI PASUA KICHWA.NCHI NAYO IMEPOTEZA DILA KATIKA KUANDAA VIJANA MAKINI.
Heshima Comrade.

Mbona sasa unakata tamaa mapema?. Huoni kuwa ukipiga mahesabu ya kulea mtoto hutokaa uzae?.

Kwanini kimeshajifia?. Wahusika ni kina nani?. Kifanyike kipi?.

Tusikate tamaa. Tuwarudishe watoto katika misingi bora.

Impossible is nothing.
 
nkilondama

nkilondama

Member
Joined
Nov 9, 2016
Messages
95
Likes
43
Points
25
Age
24
nkilondama

nkilondama

Member
Joined Nov 9, 2016
95 43 25
Kwa kweli ni kichekesho swali analoulizwa mwanafunzi na jibu analotoa ni kituko
Hadi hawa wanafunzi wanasoma kweli?
 
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
342
Likes
328
Points
80
Age
22
Asclepius

Asclepius

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
342 328 80
Kiukweli skonga inaonyesha mapungufu makubwa sana kwenye system yetu ya elimu na hasa kwa wanafunzi wenyewe binafsi hua nasikitika saana.......... Ni muda wa wazazi kua strictly na watoto wao wawa limit channel wanazoangalia simu pia
 
niachiemimi

niachiemimi

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
1,967
Likes
1,464
Points
280
Age
35
niachiemimi

niachiemimi

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
1,967 1,464 280
Kuna siku mwanafunzi nadhani ni wa kidato cha tatu au pili, aliulizwa, mkusanyiko wa viti na meza pale sebuleni kwao, kwa jina moja kwa lugha ya english vinaitwaje? akasema vinaitwa vegetable.
 
Kinyozi wetu

Kinyozi wetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Messages
326
Likes
52
Points
45
Kinyozi wetu

Kinyozi wetu

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2014
326 52 45
Kuna siku mwanafunzi nadhani ni wa kidato cha tatu au pili, aliulizwa, mkusanyiko wa viti na meza pale sebuleni kwao, kwa jina moja kwa lugha ya english vinaitwaje? akasema vinaitwa vegetable.
Hahaa niliiona hii kidogo machozi yanitoke kwa kicheko cha uchungu.
 
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
1,518
Likes
1,984
Points
280
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
1,518 1,984 280
Kiukweli skonga inaonyesha mapungufu makubwa sana kwenye system yetu ya elimu na hasa kwa wanafunzi wenyewe binafsi hua nasikitika saana.......... Ni muda wa wazazi kua strictly na watoto wao wawa limit channel wanazoangalia simu pia
I agree with you Comrade..

Siku hizi kuna janga kubwa limeibuka katika suala zima la Teknolojia. Leo hii vingamuzi vingi vina chaneli hata zaidi ya 500. Na chaneli nyingi kati ya hizo ni Uchafu wa magharibi, miziki iso na tafakuri za kina pamoja na sinema za hovyo (kumradhi).

Sambamba katika simu. Wengi hatufahamu matumizi sahihi ya simu janja (smartphones). Wengi ni mitandao ya kijamii isiyo na tija (Ni Whatsap, Insta, na Immo) ndizo tuzijuazo. Tunatumia bando kufanya mambo ya kijinga.

Trueth comes with pain. Ni sharti tuwe strictly Asclepius .
 
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
1,518
Likes
1,984
Points
280
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
1,518 1,984 280
Jana kuna mwanafunzi kaambiwa aandike neno "psychology" kaandika "cycorogy"
I was shocked.

Halafu kibaya zaidi wanacheka. Nb; sisemi unune ila ujutie kukosa swali la kijinga. Niliudhika sana na ndicho kilichochangia pia niandike uzi huu.

Wazazi tuwe makini. Mwanafunzi pia awe makini.
 
Ngushi

Ngushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
7,805
Likes
15,030
Points
280
Ngushi

Ngushi

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
7,805 15,030 280
Mmmh inaumiza sana!

Nina wadogo zangu fulani mapacha nimepiga kelele sana nikaona Sasa mpaka bi Mkubwa anataka kunichukia!
Yaani hata uzungumze nao kwa hisia namna gani hawakuelewi.......

Vichwani bure kabisa!! Nao ni sampuli ya hao hao wanaoonekana kwenye hicho kipindi cha skonga!
Mpaka Kuna wakati unajuiliza Kuna mtu kawaloga wadogo zetu?

Nimekuja kugundua nitaumia bure tu kwa kuwawazia wao ugumu watakaokutana nao mbele!
Ni kuachana nao
 
chris bedo

chris bedo

Member
Joined
Apr 11, 2014
Messages
60
Likes
57
Points
25
chris bedo

chris bedo

Member
Joined Apr 11, 2014
60 57 25
Huuu ukweli aiseee hawa ndo wanachosha yaan mtu anaulizwa hata Africa Mashariki ina nchi ngapi,ila yuko form four hakujui
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
28,406
Likes
15,435
Points
280
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
28,406 15,435 280
itawezekana kama
smartphone zikipigwa marufuku.. tofauti na hapa
Mungu aingilie kati
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
11,310
Likes
10,599
Points
280
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
11,310 10,599 280
Kuna siku mwanafunzi nadhani ni wa kidato cha tatu au pili, aliulizwa, mkusanyiko wa viti na meza pale sebuleni kwao, kwa jina moja kwa lugha ya english vinaitwaje? akasema vinaitwa vegetable.
Hahah aisee huyo dogo arudishwe darasa la 4 tu
 
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
1,518
Likes
1,984
Points
280
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
1,518 1,984 280
Mmmh inaumiza sana!

Nina wadogo zangu fulani mapacha nimepiga kelele sana nikaona Sasa mpaka bi Mkubwa anataka kunichukia!
Yaani hata uzungumze nao kwa hisia namna gani hawakuelewi.......

Vichwani bure kabisa!! Nao ni sampuli ya hao hao wanaoonekana kwenye hicho kipindi cha skonga!
Mpaka Kuna wakati unajuiliza Kuna mtu kawaloga wadogo zetu?

Nimekuja kugundua nitaumia bure tu kwa kuwawazia wao ugumu watakaokutana nao mbele!
Ni kuachana nao
Hongera kwa jitihada hizo boss!

Vipi lakini tukiwatumia wataalamu mbalimbali kuzungumza na wanafunzi wetu itakuwaje?. Nasema hivyo kwakuwa pengine approach (njia stahili) tunazozitumia siyo sahihi ndiyo maana hawatusikilizi sisi kama wazazi na walezi.

Wataalami wa saikolojia, sosholojia (Taalimujamii), Theolojia (TaalimuMungu) na kadhalika hawawezi kufanikiwa katika hili badala ya kupeleka Fiesta, na wasanii wa singeli mashuleni?.

Karibu tujadili Ngushi .
 
M

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
320
Likes
145
Points
60
M

MKEHA

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
320 145 60
Teachers are discouraged by the community, teachers are paid less, what do you expect?. Lakini pia wanaidai serikali hela ya likizo, mishahara ,matibabu na masomo. Walimu hawana morality sijui ni mgomo baridi
 
P

poa tu

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Messages
1,182
Likes
1,601
Points
280
Age
47
P

poa tu

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2016
1,182 1,601 280
Sabalkheri wana Jamii Forums?.

Naanza kwa usaili na nitamaliza pia kwa usaili. Usaili ni kuuliza masuala ya msingi. Kuanzia unachokiona, unachokisikia, unachokidhania, unachokishika na kadhalika. Hivi ndivyo walivyofanya kina Socrates, Pythagoras, Galileo Galilei, Fantz Fanon, Mwl J.K.Nyerere na orodha inaendelea...

Huu waraka ni Nasaha kwa Wizara ya Elimu, mzazi, mlezi, kaka, dada na Jamii yote ya Watanzania wenye tafakuri za kina na wenye mapenzi ya dhati kwa Taifa lao la sasa na la baadaye. Maagizo haya yametoka kwa Mungu. Ni sharti Mzazi amlee mtoto katika njia impasayo kwakuwa (Mtoto) hatoiacha kamwe hata atakapokuwa Mzee ( Mithali 22;6). Nb; Silaha zinaandaliwa wakati wa amani na si wakati wa vita.

Hivi karibuni, miezi kadhaa ilopita nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu uso na mashaka kipindi cha SKONGA kiendeshwacho katika luninga kupitia East Africa Television (EATV).

Nikiandikacho hapa ni ushuhuda wa nilichokishuhudia na ninachozidi kukisaili (siyo kuhadithiwa) kama pengine ambavyo huenda ukawa ndiyo kwanza unalisikia jina hili la kipindi cha SKONGA katika maandishi haya. Ninatazama kipindi hiko na ninazidi kukitizama kila panapobidi. Kama pia uliwahi kukitizama ni vizuri lakini pia kama hukuwahi kukitizama ni vizuri pia. Nitajaribu kudokeza kidogo ili sote tupate taswira kamili juu ya kipindi hiki.

Kiekweli, bila kupepesa ukope wala kumungunya maneno kuna walakini katika Taasisi yetu ya Elimu, Taasisi ya Familia na Taifa kwa ujumla. Kuna kasoro katika mitaala yetu ya kielimu. Silabasi zetu hazimuandai Mwanafuni kukabiliana na mazingira ya wakati wa sasa na ujao.
Kuna wakati wa Q & A (Questions and Answers) katika kipindi hiki cha SKONGA. Kiukweli hapa ndipo ninapochoka juu ya wanafunzi wetu. Round knowledge ya mambo anuai, current news na kadhalika ni baadhi tu ya mambo yanayoifanya kipindi hiki kiwe cha vichekesho na pengine si kusadifu lengo la kuanzishwa kwake.

Tuna upungufu Mkubwa sana wa Maarifa (General knowledge) vichwani kwa Wanafunzi wetu. Si wanafunzi wa S/Msingi, Sekondari na hata Vyuoni. Ni unazi, utunduwizi, ufisadi na ufisidi, umaamuma, ushabiki, utovu wa adabu, mbwembwe, ulimbwede, dharau na kedi, migoda mikogo na kadhalika.

Wanafunzi hawa hawafahamu mengi na wameridhika na hali walizonazo. Pengine hili si kosa lao, rafiki yangu mmoja anapenda kuniambia "Aliyetuloga keishakufa". Maswali yaulizwayo katika kipindi hiki ni ya kawaida mno ila wanayakosa makusudi. Tatizo ni nini?. Nani apewe lawama?.

Hivi mwanafunzi wa Kidato cha nne unashindwa vipi Square root ya 144?. Kirefu cha USD, TAZARA, BOT, EAC nk?. Humfahamu vipi Shaaban Robert?.

Mbona tunafahamu kirefu cha WCB, Washindi wa Miss Tanzania/World?. Mbona tunafahamu sinema za Kikorea na waigizaji wake?. Mbona tunafuatilia Fiesta kama tumerukwa na akili?.

Wanafunzi hawahawa wanamiliki simu za mkononi bila Mzazi/mlezi, Mwalimu kufahamu. Bora basi hata wangekuwa wanatumia simu hizi katika masuala ya msingi lakini wapi?..Ukibahatika kuzishika hizo simu utavunjika moyo sana na pengine atapandwa na presha (Bp) bure. Huku ni kufeli kwa Taasisi za kifamilia. Wazazi na Jamii kwa ujumla hawayaelewi madhara ya utandawazi ndiyo maana watoto wengi wanavutiwa na vikolombwezo hivi viso na mantiki..

Nilifikiria sana na kupata majibu kuwa "Ndiyo maana tu wepesi kufuatilia Big brother na Miss world kama tumerukwa na akili kuliko kufuatilia washindi wa Tuzo ya Nobel kwa mwaka huu". "Ndiyo maana tu wepesi kufahamu jina la Miss Tanzania kuliko jina la mwanafunzi aliyepata maksi za juu katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu". Kwanini wanafunzi wetu ni wahanga wa kufuatilia masuala yaso wajenga?.

Hizi ni Zama za 'Maarifa na Taarifa (Information age). Uelewa wa Mambo na ujenzi wa hoja ndivyo vinvyompa mwanafunzi nafasi ya kuwa bora zaidi ya mwingine na si usadikifu pofu wa kimakundi, ushabiki uso na mantiki na Umaamuma. Ukiona nafsi yako inataka kujua vilivyo bora zaidi sambamba na visomo, pima mashauri kwa kusudio lenye kuakisi mapenzi mema, nia kuu zaidi na upendo usio na mipaka juu yote na kila kitu.

Ni sharti Ubongo, Nafsi na Roho ya Mwanafunzi iJifunze si tu ya watu wa asili ya kabila moja, bara moja, rangi moja na kadhalika. Dunia yote na watu wake ni jamii yake na ni fahari za utu, mwangaza na fanaka kujaliwa kheri na kweli moja iliyo ni Uzima. Misimamo ama itikadi iso na staha si vya kupewa nafasi kabisa, ni sharti kuvibeza kwa akili na roho huku utunduwizi na ujinga vikifutiliwa mbali.

Ninachohitaji kukikusudia hapa ni kutoa ushauri kwa wahusika na haraka iwezekanavyo juhudi za makusudi zichukuliwe mapema ili kujinasua katika matope haya juu ya kile Prof Chachage alichokiita "Collective imbecilization".

Tusijipumbaze kihalaiki katika hili. Mwanafunzi achukue wajibu wake, Mwalimu na mzazi pia. Hakuna kutegeana katika hili. Utegevu ukiwepo, lazima pengo lionekane.

USHAURI.

Wazazi, walezi, kaka, dada na kadhalika waelekeze nguvu za ziada kwa walengwa (wanafunzi) kwa kuwawezesha kuwekeza zaidi katika Maarifa ikiwa ni pamoja na kuwasimamia vizuri katika matumizi yao ya muda. Kwenda katika sinema zisizo na tija, vibanda vya luninga, Kuzidisha michezo, kutazama luninga sana ni moja ya mambo ya kukatazwa na mwenye dhamana kwa mwanafunzi.

Ni vyema mwanafunze apate utulivu wa akili (Calmness of mind) walau kila siku ili ajiboreshe zaidi na zaidi. Kushughulika na mambo mengi yaso na tija ni kuuharibu ubongo wa mwanafunzi na madhara yake ni makubwa sana kwa siku za usoni.

Tuache kujenga Baa majumbani na badala yake walau tujikite katika ujenzi wa Maktaba (Library) kwa ajili ya kujisomea na kuongeza wigo mpana wa Uelewa kwa wanafunzi wetu na kujenga Taifa la wasomi wanaojitanua kimawazo.

Wanafunzi wanunue/ wanunuliwe vitabu vya kujisomea (Kiada na ziada). Siyo ununuzi wa vitabu vya mitaala ya shuleni tu. Vitabu nje ya mitaala (Riwaya, Tamthiliya, Ushairi nk). Mkusanyiko wa maudhui yapatikanayo katika vitabu vya Ushairi, Riwaya na Tamthiliya huweza kuwa na mchango chanya kwa wanafunzi kuliko magazeti ya udaku pamoja na vitabu visivyowajenga kimaarifa.

Hapa najua wengi watazungumzia gharama (cost) za vitabu ila ukweli ni kwmaba, Tatizo siyo gharama ya kitabu. Tatizo ni gharama atakayoilipa mwanafunzi kwa kutokusoma kitabu. Sisi ni matokea ya yale tunayojifunza kwahiyo kama huna wigo mpana wa mambo basi wewe si chochote. Na kwa mujibu wa tafiti "Maarifa unayoyajua sasa yatakuwa yamepitwa na wakati baada ya miaka miwili hadi mitatu". Kila uchwao tujifunze na kujifunza tena.

Mithali 4 : 13
"Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako."
Proverbs 4:13
"Hold on to instruction, do not let it go; guard it well, for it is your life."

One Thing; #Be Wise with your comment(s).
Mkuu huwa siwezi kutazama hiki kipindi nikamaliza, nachefukwa na kusikia uchungu mno! Kinatupa uhalisia wa aina ya elimu tuliyonayo na ubora wake (kwenye shule za umma) halafu natazama na ushindani uliopo kwenye hii dunia na hapa kwetu EA, nabaki kusikitika MNO. Kipindi huniacha na tafakari moja tu kwamba ELIMU NI GHARAMA KULIKO TUNAVYOFIKIRI NA TUNAVYOAMINISHWA KUFIKIRI. Hakuna ELIMU BURE dunia hii, it is rather FREE OF KNOWLEDGE. Tulisoma shule hizo pia lakini hali haikuwa mbaya hivi, kuna tulipikosea na hatutaki kuamini kama tunakosea.
 
Jaslaws

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Messages
5,575
Likes
2,923
Points
280
Jaslaws

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined May 31, 2011
5,575 2,923 280
Wanafunzi wa secondari hizi za public kiingereza hawakijui kabisa,huwa najiuliza hawa nasomo ya darasani wana ya master vip..!?tufanye kazi tusomeshe watoto wetu shule nzuri,hizi za public Ni shida sana
 
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
1,518
Likes
1,984
Points
280
Dahafrazeril

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
1,518 1,984 280
Mkuu huwa siwezi kutazama hiki kipindi nikamaliza, nachefukwa na kusikia uchungu mno! Kinatupa uhalisia wa aina ya elimu tuliyonayo na ubora wake (kwenye shule za umma) halafu natazama na ushindani uliopo kwenye hii dunia na hapa kwetu EA, nabaki kusikitika MNO. Kipindi huniacha na tafakari moja tu kwamba ELIMU NI GHARAMA KULIKO TUNAVYOFIKIRI NA TUNAVYOAMINISHWA KUFIKIRI. Hakuna ELIMU BURE dunia hii, it is rather FREE OF KNOWLEDGE. Tulisoma shule hizo pia lakini hali haikuwa mbaya hivi, kuna tulipikosea na hatutaki kuamini kama tunakosea.
So sad Comrade!

Ukiitizama kipindi hiki kwa jicho la tatu utagundua mapungufu mengi mno kama ulivyojibainisha. Gharama ya Elimu ni ndogo sana ukifananisha na gharama ya Ujinga. That is the reality.

Wizara husika ina haja ya kulitazama hili kwa mapana sana. Kuna walakini mkubwa sana kwa wanfunzi wetu. Pia wazazi kwa ujumla tulitizame hili kwa ufanisi na udodosi wa hali ya juu sana. Tu-deal na sababu na si matokeo ya kufaulu na kuendelea mbele kwa mwanafunzi.

Namfikiria sana yule mgombe aliyesema.

Elimu.
Elimu.
Elimu.

Aliwaza mbali sana. Kunahitajika mapinduzi ya hali ya juu mno katika hili.
 
Mirlz B Matthew

Mirlz B Matthew

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2011
Messages
946
Likes
969
Points
180
Mirlz B Matthew

Mirlz B Matthew

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2011
946 969 180
Inauma sana watoto wa miaka ya 97 hadi. leo hii yani kichwani hamna kituu bali kuiga umagharibi ndo wanaweza,kusikiliza na kuangalia vitu vya ajabu ndo wanapenda mfano hizi tamthilia zao zimejaa vitu vya ajabu....ubishi umewajaa,kila kitu wanajua wao ukimuelekeza hivi anafanya tofauti hata walimu wao darasani wanapataga shida sana kuwaelekeza dah.....!na wanalelewa kiajabuajabu ukimuelekeza kitu kwa nia njema tu mzazi wake atakutolea povu na mwisho utaambiwa zaa wako..
 
Forum statistics

Threads 1,237,614
Members 475,671
Posts 29,294,434