Kipindi cha SKONGA, EATV. Kitendawili kinachohitaji Majibu

Subiri siku ukiambiwa wanayofanya kaka zao wa vyu vikuu ndio utachoka kabisa. Nimeyaona kwa macho yangu hadi nawaza wanangu niwafundishe mwenyewe maana hapa kuna maangamizi ya elimu.
 
Watu wa kwanza kulaumiwa ni wazazi then ndio makundi mengine yanafuatia.
Nakumbuka kipindi nipo shule ya msingi baba alikuwa anakuja na magazeti nyumbani(yale ya kujenga) na ni lazima tuyasome maana atatuuliza maswali. Na kipindi cha taarifa ya habari ni lazima tuangalie. Wakati mwingine anatuuliza maswali magumu kuhusu mambo yanayoendelea nchini lakini ilitusaidia kuwa na taarifa sahihi kwa wakati sahihi.

Watoto wa sasa hivi wanafuatilia mambo ya kipuuzi tu maana hawana muongozo. Hebu tuanze kwanza na kundi la wazazi wajikite ktk kutoa malezi sahihi kwa watoto wao.
 
Comrade, Umeshalamba mchuzi?.

Mishe za waso na Elimu ni zipi?. Na wenye Elimu ni zipi?.

Karibu tufunzane.
Mbona zipo mkuu, mfano nina dada angu kamaliza chuo.. Education lkn bada ya kutoajiliwa anatengeneza mikologo... Mwingin my braza WA kitaa amesoma education lkn yupo gerejin anaunga pancha za magarii... My blood braza kasoma agribusiness pale sua lkn anahangaika na vijiwe vya chips.... Mwenyew first year public relations and marketing lkn nawaza kuwa wakala wa mpesa kwa hela ya Boom... Sasa izi kazi zote zinafanywa na watu ambao hawana elim... Ko ile morali ya kusoma kwa wengin inapungua pia.. Labda jamaa amemanisha iv
 
Nimepitia public schools na huwezi nishauri kuja kuyachezea maisha ya mtoto wangu rehani katika shule kama hizo...

Mwanafunzi anafundishwa kufaulu na si kupata maarifa, wazazi hawaoni soni kufanya upuuzi mbele ya watoto wao, jamii inaona kuwa haina jukumu la kumkuza mtoto wa Fulani na waalimu nao hawana vigezo na hawapo nyuma katika kuwapumzikia wanafunzi kimapenzi

kiufupi elimu yetu imepitwa na wakati na wizara iliangalie hili..

1. Wizara ingeongeza bajeti katika kuboresha mazingira na si kuondoa malipo maana hapo ni sawa na kuongeza mshahara na matumizi kwa wakati mmoja ilhali unategemea impact...

2. Waalimu pia wamekuwa wengi hivyo ni muda muafaka wa kuanza mfumo wa interviews na mikataba ya muda ili kupata waalimu competent

3. Boarding schools ziongezwe na iwe must haswa kwa watoto wa kipato cha chini maana huko ndipo fukuto lilipo
 
Mkuu umeandika ukweli mtupu! nafikiri kunamahali kama taifa tumekosea, na kama ulivyosema "silaha uandaliwa wakati wa amani na si wakati wa vita" hvyo basi ni vizuri kutafuta ufumbuzi sasa kabla haijawa hatari zaidi huko tuendako, maana hao wanafunzi ndio walimu wabaadae, ndio madaktari, ndio viongozi, ndio watangazaji, ndio walinzi wa taifa wabaadae nk. tunapoelekea wauliza maswali watakuwa ni wao na wakujibu hayo maswali watakuwa ni haohao, "muuliza swali atauliza la kijinga na anayejibu atajibu ujinga" sasa sijui nani atamnyoosha mwenzie kama hivi tunavyojadiliana sasa
 
Mimi huwa nashikwa hasira sana napo tizama kipindi hicho, hasa session ya Q & A maana vijana wapo watupu...

Huwa najiuliza hivi serikali huwa inaangalia kipindi hichi? na kama inakiangalia wao kama wao wamechukua hatua gani mpaka sasa kwaajili ya kumkomboa mwanafunzi hasa katika shule za serikali....

Hivi tatizo ni mitaala au mbinu za ufundishaji au tatizo ni hii teknolojia ndo inawaharibu vijana wetu...
Naomba Hii thread angalau iwafikie wahusika...

Ila naogopa wasije kukuita mchochezi
 
Asante kwa kuliona hilo mkuu, ni masikitiko makubwa sana, mi nakumbuka miaka hiyo kuanzia darasa la tano tungeweza kutaja majina ya miji mikuu ya Africa yote, darasa la sita basi ni wafanyakazi wa ulimwengu, ungeweza kutaja zao la mpira linalimwa wapi, zao la kakao linalimwa wapi mpaka matumizi yake, maraisi wa nchi mbalimbali, mawaziri mpaka wakuu wa mikoa yote ya Tanzania, na kumbuka enzi hizo za 80's hakuna cha gazeti(kule vijijini) wala TV au simu, ila ukibahatika kupata gazeti basi hata kama limepita mwezi utalisoma kwa kujiongezea maarifa tena bila ya kulazimishwa, nyakati zimebadilika sana, enzi hizo walimu walipewa utukufu sana, mtoto wa mwalimu alikuwa ni kama prince, walimu waliifanya kazi hiyo kwa kuridhika na sio kama last option, idadi ya wanafunzi darasani iliendana sawia na nyenzo zilizopatikana hapo, darasa la watu 40 kila mmoja ana kitabu chake mpaka vile vitabu vya hadithi kama vya Bulicheka vilikuwepo, walimu walifundisha kuelewa na sio kufaulu mtihani mf darasa la watu 40 "wanachaguliwa" wawili tu kuendelea na sekondari ya serikali. Tatizo lililopo kwa sasa ni kwamba ualimu imekuwa ni last option kwamba mtu kakosa kote anasema ngoja niende ualimu, na akija huko waajiri/serikali inaangalia zaidi wingi kuliko ubora ni heri darasa zima lifaulu hata kama hawajui kusoma wala kuandika (mf drs la 7) kwa mfumo wa ku.shade. Pia tumejenga kizazi cha kurahisisha mambo, mitihani ya kushade, kukariri majibu (vitabu vya Nyambari). Mwalimu ametelekezwa na serikali mf tunakazania kujenga madarasa na wanafunzi kusoma bure, kitakachofuatia ni mtoto kujiongoza mwenyewe maana mwalimu ashakatishwa tamaa, ikifuatiwa na kauli kama "ukiona huwezi kufundisha acha kazi" hapa hatujengi bali tunabomoa, madarasa yamejaa sana, darasa la wanafunzi 200 mwalimu atasimamiaje? Nakumbuka drs la 1&2 tulikuwa na mtihani wa kusoma, sidhani kama inawezakana kwa drs kubwa kama hilo. Pia malezi yamechangia, kipindi kile mtoto alikuwa ni wa wote lkn kwa sasa mtoto ni wa mzazi wake tu, hata mwalim anaogopa kumuadhibu, ntaendealea baadae....
 
Wanafunzi wa miaka hii sijui vichwa vyao vina nini maana uwezo wao wa kuchakata mambo ni almost negligible wao wamewekeza zaidi akili zao kwenye kuvaa suruali za kubana mapaja kiukweli walimu wanakazi sanaaaa....
 
Kuna kipindi nilikuwaga Mwl wa muda, ila nilichoka watoto wa kizazi hiki hivi wazazi uawaoni haya. Niliacha ila nilikuwa nilishachoka na watoto wa like jamani sio kwa majanga Yale, watoto wa najua mambo ya kikubwa balaa
 
Teachers are discouraged by the community, teachers are paid less, what do you expect?. Lakini pia wanaidai serikali hela ya likizo, mishahara ,matibabu na masomo. Walimu hawana morality sijui ni mgomo baridi
Na wakitaka kuwanyoosha wananyoosheea vidole kuwa wamepiga watoto wao mara wafukuzwe.
Mwisho wa siku wanaamua kuacha liende
 
So sad Comrade!

Ukiitizama kipindi hiki kwa jicho la tatu utagundua mapungufu mengi mno kama ulivyojibainisha. Gharama ya Elimu ni ndogo sana ukifananisha na gharama ya Ujinga. That is the reality.

Wizara husika ina haja ya kulitazama hili kwa mapana sana. Kuna walakini mkubwa sana kwa wanfunzi wetu. Pia wazazi kwa ujumla tulitizame hili kwa ufanisi na udodosi wa hali ya juu sana. Tu-deal na sababu na si matokeo ya kufaulu na kuendelea mbele kwa mwanafunzi.

Namfikiria sana yule mgombe aliyesema.

Elimu.
Elimu.
Elimu.

Aliwaza mbali sana. Kunahitajika mapinduzi ya hali ya juu mno katika hili.
Siku hizi elimu haina amsha amsha, hakuna debate baina ya shule na shule yani imekosa hamasa ile ya zamani.
Watu tulikuwa tuna debate, tunachambua mambo leo utaskia fiesta mashuleni na after school bash..
 
Kuna siku mwanafunzi nadhani ni wa kidato cha tatu au pili, aliulizwa, mkusanyiko wa viti na meza pale sebuleni kwao, kwa jina moja kwa lugha ya english vinaitwaje? akasema vinaitwa vegetable.
HAHAHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHHA,
 
Umeandika kwa uchungu sana
Hapana Comrade!

Ujue kuna baadhi ya mambo yanaudhi mno?. Hivi mwanafunzi wa kidato cha Nne unashindwa vipi kutaja kirefu cha EAC?.

Kuwa Baba ni kazi rahisi sana. Kuwa mzazi ni kazi ngumu. Hivi ulishafikiria kilichotamkwa na Mtu fulani,

1, Elimu.
2, Elimu.
3, Elimu.

Usimfikirie aliyevitaja hivi vitu. Tuvijadili alivyovitaja. Hivi ujue alimaliza kila kitu?..

Nyerere alisema "Education for Liberation". Ujue kina Ndalichako hawaielewi hii Logi?.

Karibu mkuu. Kuna mtu humu huwa anadai wewe ndiye mimi (I'll tell u one time).
 
Watu wa kwanza kulaumiwa ni wazazi then ndio makundi mengine yanafuatia.
Nakumbuka kipindi nipo shule ya msingi baba alikuwa anakuja na magazeti nyumbani(yale ya kujenga) na ni lazima tuyasome maana atatuuliza maswali. Na kipindi cha taarifa ya habari ni lazima tuangalie. Wakati mwingine anatuuliza maswali magumu kuhusu mambo yanayoendelea nchini lakini ilitusaidia kuwa na taarifa sahihi kwa wakati sahihi.

Watoto wa sasa hivi wanafuatilia mambo ya kipuuzi tu maana hawana muongozo. Hebu tuanze kwanza na kundi la wazazi wajikite ktk kutoa malezi sahihi kwa watoto wao.
Comrade espy , I Salute You.

Ahsante kwa uchambuzi na tafakuri binafsi. You really nailed It. Ipo haja ya watu kuwa Wazazi na siyo kuwa Baba wala Mama.

Nimesema hivyo kwakuwa. Kuwa Baba/Mama ni kazi rahisi sana. Kuwa Mzazi ni issue deep kidogo. Ni kuhusu kufunza, kulea kwa misingi chanya, kuelekeza, kumsaili mwana na pia kumdodosa na kadhalika. Huku ndiko kuwa Mzazi.

Wengi ni Baba/Mama na siyo wazazi. Kumbuka waswahili wanakamilisha hili kwa semi nyingi sana. Kulea si kazi, kazi kumlea mwana. Kuwa baba si kazi, kazi kuwa baba mzazi. Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo etc etc..

Nje ya hapo, ni dhana fulani tu ya Kiafrika ambayo kila Mtu mwenye mbegu ana uwezo wa kuzalisha na kibarua kuishia hapo. Hajui na hafuatilii lolote.

Wazazi watimize majukumu kwa watoto.
 
Back
Top Bottom