Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,077
Katika ulimwengu wa watu waliostaarabika, ni aibu kubwa na kukosa nidhamu kwa kiwango cha juu kama mtu ukishindwa kutimiza ahadi yako mwenyewe, uliyoitoa kwa hiari yako mwenyewe bila ya kulazimishwa na mtu yeyote. Anayeshindwa kutekeleza ahadi yake mwenyewe, huyo amekosa nidhamu kwa nafsi yake mwenyewe.
Tukumbushane: Rais Samia na Serikali yake iliwaahidi Watanzania kuwa tatizo la umeme linaishia mwezi January 2024, na kwamba neema ya upatikanaji umeme wakati wote, umeme wa uhakika itaanza mwezi February 2024, kwa sababu mlango mmoja wa bwawa la Mwalimu Nyerere utafunguliwa. Akaongeza kuwa ziada kubwa ya umeme itapatikana kuanzia mwezi March 2024 watakapofungua mlango wa pili wa bwawa la Mwalimu Nyerere.
Leo ndiyo tarehe 1 mwezi February 2024, na kwa ahadi ya Rais na Serikali yake ndiyo tumeingia mwanzo wa kipindi cha neema kitakachotufanya tuyakumbuke masuala ya mgao wa umeme kuwa historia.
Naomba tupeane taarifa juu ya upatikanaji wa umeme kwa nchi nzima kuanzia leo, kupitia uzi huu ili tujue kuwa Rais wetu ni mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu au la. Na kisha apongezwe kwa kutokomeza tatizo sugu la umeme au tumlaani kwa kutudanganya.
Tutambue kuwa yeyote anayefifisha au anayeshindwa kulihakikishia umeme wa uhakika Taifa, analiangamuza Taifa. Maendeleo ya nyanja zote yanategemea uwepo wa nishati ya uhakika ya umeme.