Kipindi Bora zaidi cha Television na Radio Tanzania...

Todito

Senior Member
Feb 6, 2013
154
357
Wakuu habari za leo?

Nimepata mtafaruku wa moyo sana leo kuwaza ni kipi kimewahi kua kipindi bora zaidi cha Radio na Television hapa nyumban Tanzania.

Kwa upande wa Television kwangu vipindi bora zaidi ni÷
1) Bongo Star Search ya Madam Rita
2) Ze Comedy ya kina Masanja EATV
3) Mkasi wa Salama Jabir na AY

Upande wa Radio
1) Kipusa Abdalah Majura, Radio One
2) African Beat, Dee Seven Kiss Fm
3) XXL, B-Dozen, Clouds Fm

Maoni yako tafadhali...

Tutumie uzi huu kutaja vipindi bora kwako upande wa Tv na Radio tuwatie moyo waliobuni.

Karibu.
 
Mimi nakumbuka enzi hizo nasikiliza RTD fashion ya radio ilikuwa ni zile wanaita RADIO MKULIMA na brand names zake zilikuwa ni NATIONAL Panasonic ama PHILIPS. Mzazi alikuwa anainunua RTC (yale maduka ya uma).Tukirudi katika vipindi, navikumbuka sana vipindi vifuatavyo ambavyo bila shaka mdau utakubaliana na mimi vilikuwa maarufu kutokana na zile nyimbo za utangulizi kuashiria kipindi kuanza ama kumalizika.

1. Sikiliza Bwana Umeme... (Bwana Umeme) - Kile kipindi cha TANESCO cha kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya umeme.

2. Starehe na BP - Uncle Julius Nyaisanga (R.i.P) alikuwa anakimudu vyema kabisa.

3. Kahawa ni Mali - Namkumbuka sana yule mama wa kiashirio cha kipindi akitamka hayo maneno kwa rafudhi ya kichaga.

4. Jifunze Kiswahili Fasaha - sina uhakika kama nimeandika vyema tittle yake lakini kilikuwa ni kile kipindi kizuri kilichobuniwa kuhamasisha watu kuzungumza kiswahili katika harakati ya kuwaunganisha watu wa mikoani na wa Bara. Nakumbuka kiashirio chake kuna sehemu inasema.. na mikoani... ni kiswahili chatumika.....Bila kusahau vipindi kama..

5. TTCL Simu kwa Maendeleo.

6. Serikali za Mitaa.

7. Afya yako /Afya ya jamii " sikumbuki vyema title ila nakumbuka kiashiria cha kipindi ulikuwa ni wimbo mmoja anaimba Kept John Komba (R.i.P) na kundi lake wakati ule.

Ukija vipindi vya week ends

1. Club Raha leo Show.
2. Mama na Mwana namkumbuka mtangazaji Edda Sanga alikuwa anakimudu vyema kipindi na zile hadithi za "Adili na Nduguze", "Kisa cha Mfalme Juha", ile hadithi ya watoto wa mfalme wanakwenda kutafuta wachumba wa kuoa... n.k
Wakati ule radio ilikuwa na msaada mkubwa kuelimisha jamii nzima (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara) kuhusu mambo mbali mbali na watu walikuwa wanafuatilia sana.
 
Asante sana,kumbe ww ni muhenga mwenzangu
 
Nyimbo bora duniani- RFA
Mtangazaji Lazaro Matalange
Cruise alikuwa anaifanya Steve Kabuye
Kiss colabo ya ezden the rocker.
Baada ya hapo vpnd vya siku hizi vya kawaida saaana.
 
Back
Top Bottom