Kwa kweli ukishakuwa ndani ya si si emu hata elimu inapotea. Huyu Dr nimemsikiliza na utadhani amemaliza tu darasa la saba jinsi anavyochambua masuala. CCM imeua uwezo wa kufikiri wa wasomi wetu. Dr Chegeni umejiabisha sana. Huyu jamaa baada ya kubwagwa kwenye kura za maoni jimbo la Busega aliisusa ccm, akatishia kuingia chadema. JK alipoenda Mwanza jamaa akasusa na hakwenda kumpokea, jk akaagiza atafutwe kwa nguvu, halafu tunaambiwa wakawa na mazungumzo ya faragha. Leo tunasikia kuwa ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya ccm. Inavyoonekana jk ameshamwahidi cheo mara aingiapo madarakani. Hivi ndivyo "wasomi" wetu walivyo.
Hivi huyu uDK wake ipo kwa msemakweli? naona anashindwa kujibu swali????
Wadau kwa wale waliocheki Taarifa ya habari ya ITV ya leo saa mbili usiku waliona kuwa swali la Kipima Joto cha kesho 22/09/2010 ni "AHADI YA ELIMU NA AFYA BURE INATEKELEZEKA?"
Hii ni moja kati ya sera za CHADEMA na viongozi wa CCM wamejitahidi sana kuwaaminisha watanzania kuwa ahadi hii ya uongo. Jana katika mdahalo ule wa EATV ambapo JF founder alihudhuria, Isaack Gamba aliizungumzia na akawa anataka kuwaminisha watanzania kuwa hili haliwezekani. Je hawa ITV watakuwa tayari kutoa habari zitazowapa credit CHADEMA ikiwa wengi watasema ndio??
Sitashangaa kama wakituonyesha wanaohoji watu waliowaandaa, then watu wote wakasema hilo haliwezekani na overall matokeo yakaonyesha kuwa ahadi hiyo haitawezekana lengo likiwa ni kuichafua CHADEMA.
My take: Madamu wameanza kuwahoji wananchi kuhusu ahadi za wagombea, Kipimajoto kijacho nawashauri kiwe "AHADI YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA NGARA,BANDARI MBEYA, NA KIGOMA KUWA DUBAI INATEKELEZEKA"
Wasiwasi wangu who is going to Vote!! and who is choosing who has to Vote??
Hiyo ni habari njema tunataka kuona mabadiliko mwaka huu! naomba wananchi wasidaganyike kama mimiHatimaye wananchi wamewaumbuwa wale waliotaka kuwaaminisha kuwa ahadi ya kutoa Elimu na Afya Bure kuwa Haiwezekani..!!
Waliosema inawezekena ni Asilimia 81%. Hila za CCM kwisha kabisa....!
2010 HATUDANGANYIKI...!