Kipima joto cha itv cha toa mwelekeo

Naomba magazeti kama Mwananchi waazishe kura ya maoni. Tuone hao wajinga watasema wasomaji si wapiga kura?
 
Hatimaye wananchi wamewaumbuwa wale waliotaka kuwaaminisha kuwa ahadi ya kutoa Elimu na Afya Bure kuwa Haiwezekani..!!
Waliosema inawezekena ni Asilimia 81%. Hila za CCM kwisha kabisa....!
2010 HATUDANGANYIKI...!

Nilitaka majibu yawe hivi; nimependa sana na nimeona sasa sera za Dr Slaa ziko mioyoni mwa watu sasa maana mitego yote anaelekea kumaliza kuiruka
 
hivi hiyo 19% waliosema haiwezekani ni kina nani?? Ni watanzania kweli? Na wana akili timamu kweli? Wanafanya kazi gani? Hawana familia ndugu au majirani ,? Hawana dini? Au kwenye dini zao wanaabudu wenyewe? Mi nashindwa kuelewa jamani.
Aaaaaa!! Mantu angi ni marundu kabisa mi naherwa!! Aaaaaaa
 
It is now high time to test ahadi kubwa kubwa za muungwana in the same waters - Kipimajoto " JE SERIKALI YA JK INAWEZA KUIFANYA KIGOMA DUBAI?" AU JE INAWEZEKANA KUJENGA BARABARA YA LAMI KUUZUNGUKA MLIMA KILIMANJARO????
 
Freetown heshima mbele!!!!

Ni aibu na upuuzi kulinganisha uchumi wa Kenya na wa Tanzania.... angalia wenzetu walivyotikishwa na issue ya Kibaki na Raila... lakini uchumi ulisimama imara... angalau uchumi wao ulivyotikiswa na issue ya mafuta na mtikisiko wa uchumi dunianai lakini bado uchumi ukawa imara.

In short... our priority sasa hivi ingekuwa kuhudumia uchumi kwanza usimame ndio tuongelee huduma za jamii kwa wingi...

Sasa angalia bado njia kuu za uchumi ziko duni, bandari, reli, angani, barabara mifumi ya kisheria ya biashara (legal framework).

Lakini wanasiasa wetu kwa sababu wanajua sisi wajinga... wanaahidi sehemu ambazo tutawapigia makofi...

In short i don't agree with any candidates kwenye hili.... matokeo yake hawa wanataka tuwe ombaomba daima milele.... NO to KIKWETE NO to LIPUMBA and NO to SLAA.

my rule of thamb "Economic Services" first then "Social Services"; hao wengine wanaoweza ni kwa sababu ya kutumia hii rule kwanza.

Sera za huduma za jamii bure ni changa la macho kwa Watanzania... it is the only brigde to take opposition to the front seat... thus why they use it, it is not b'se they believe in it.

1. Mtu anakuambia tutauza ndege ya Rais kutoa elimu bure... ndege ya Rais moja ita-handle running cost za wizara ya elimu kwa muda gani?

2. Mtu anasema nchi ina rasilimali nyingi... upuuzi... yaani madini ambayo hayajachimbwa tayari umeweka kwenye bajeti ya matumizi

3. Mtu anasema tutarekebisha mikataba... unajua kwa sheria za kimataifa mikataba iliyoko ni halalili?

Please nyie mnaopenda urais... acheni kutudanganya.,

Mods ! Tafadhali naombeni huyu jamaa muban na kublok: kapandwa na uchizi ,poit zake hata watoto wa primary wanaweza kumpiga mawe.
 
kWA WALE WANAOFUATILIA KIPIMA JOTO CHA ITV JANA WALIKUWA NA MADA AMBAYO IMEANZISHWA NA INASIMAMIWA NA MGOMBEA URAIS WA CHADEMA SI MWINGINE NI DR W SLAA MWANA WA MPISHI ALIYESOMA BURE ENZI ZA MWALIMU. MADA HIYO NI ELIMU BURE SHULE YA MSINGI HADI FORM SIX NA WALE WATAKAO FAULU KWENDA CHUO KIKUU PAMOJA NA HUDUMA ZA AFYA BURE JE INAWEZEKANA? ASILIMIA 81% WAMESEMA NDIYO. HII INAONESHA WATANZANIA WANATAKA KUMCHAGUA SLAA WAPATE HUDUMA HIZO BURE.

JANA AKIHIJIWA MOSHI FM KWA TAKRIBANI 90 MINUTES SLAA ALISEMA CCM HAWAKO MAKINI KWANI CHAI NA VITAFUNWA VYA VIGOGO HUTENGEWA BAJETI KUBWA KULIKO BAJETI YA WIZARA YA MAJI YAANI 30 BILIONI WAKATI BAJETI YA MAJI NI 29 BILIONI.
PIA KULINGANA NA TUME YA JAJI LEWIS SERIKALI HUPOTEZA SH 700 BILIONI KILA MWAKA KWA MISAMAHA YA KODI KATIKA MIGODI YA MADINI. JE TUKISIMAMIA VIZURI MAPATO NA MATUMIZI KWANINI TUSISOME NA KUPATA HUDUMA ZA AFYA BURE?
 
hata mimi nilifurahia sana matokeo ya utafiti huo, nawapongeza ITV maana hawajaficha kama taasisi zingine, sasa nimeamini kumbe
tupo wengi na inawezekana, nikusahihishe kidogo ni asilimia 87 ndo walisema ndio, tuendelee kuchanja mbuga..
 
hata mimi nilifurahia sana matokeo ya utafiti huo, nawapongeza ITV maana hawajaficha kama taasisi zingine, sasa nimeamini kumbe
tupo wengi na inawezekana, nikusahihishe kidogo ni asilimia 87 ndo walisema ndio, tuendelee kuchanja mbuga..

Nilifurahi kuona hivyo kwenye TV hv kwanini ccm wanaona haiwezekani na wanachi tunaona inawezekana!??
 
Nami pia nilifurahi sana kuona yale matokeo ya kipima joto cha jana. Angalau watu wameamka na kuelewa mbivu na mbichi.
 
Nilifurahi kuona hivyo kwenye TV hv kwanini ccm wanaona haiwezekani na wanachi tunaona inawezekana!??

ni kwa sababu viongozi wa ccm ni mbumbumbu, walafi-mafisadi na upeo wao wa kufikiri umeshafikia ukomo. Hata wakipewa matrilioni ya dola hawawezi kuzipangilia vyema. Na wakiendelea kutawala hata kwa miaka 100 ijayo hali haitabadilika kuwa bora bali nchi itaendelea kuharibika kwa kiwango cha hali ya juu sana.
 
ni kwa sababu viongozi wa ccm ni mbumbumbu, walafi-mafisadi na upeo wao wa kufikiri umeshafikia ukomo. Hata wakipewa matrilioni ya dola hawawezi kuzipangilia vyema. Na wakiendelea kutawala hata kwa miaka 100 ijayo hali haitabadilika kuwa bora bali nchi itaendelea kuharibika kwa kiwango cha hali ya juu sana.

In Bold WABINAFSI!
 
Jamani tuweni wakweli na tusishabikie tu kila jambo. Sera ya chadema ni elimu bure kuanzia msingi hadi form 6.

Sera ya cuf ni elimu bure kuanzia msingi hadi vyuo vikuu.

Sasa unaposema kua mada hii imeanzishwa na dr slaa mimi inabidi nikuulize hivi kwani ni chama kipi kati ya cuf na chadema ambacho kilitoa au ( kilizindua) ilani yao kwanza? Bila shaka ni cuf.

Kwa hivyo hiyo asilimia iliyokubali hicho kipima joto haimaanishi kumuunga mkono slaa bali wanamuunga mkono lipumba. Jaribu kusoma hilo swali la kipima joto halafu soma na ilani za vyama utaona kua linakwendana na ilani ya chama gani.
 
binafsi napinga elimu ya bure... Huku nikurudisha watu nyuma... The priority now should be improving quality of education... Hizi elimu za bure will endup getting nothing.

Napenda wanasiasa wakweli.

"kila mtu ataubeba mzigo wake mwenye" - c. D. Msuya.
yawezekana ukawa uko sahihi kwa mtazamo wako. Lakini sisi tulisoma bure na elimu tuliyopata ni bora, kwa sasa sio bure na elimu ni ya kusuasua, SI UMESIKIA TAARIFA YA WATAFITI MAJUZI KUHUSU ELIMU YA MSINGI. Hautaki habari njema ila unataka udanganywe ndipo ukubali ndg yangu aaah, samahani mheshimiwa,maana ndivyo mnavyotaka kuitwa siku hizi, enzi zetu ilikuwa ni ndugu; juzi nimemsikia mgombea wa chama tawala anasema ametekeleza ahadi kwa asilimia mia, halafu watu wanashangilia, sijui ni upunguani, uzezeta au Watanzania tumelogwa na kupofushwa macho, tunaoelewa tunaona na tunajua barabara ambazo rais mtaafu Mkapa alisema ifikapo 2006 zitakuwa zimeisha, leo hii 2010 niandikapo ujumbe huu hazijaisha, lakini Ben pesa aliacha, kwa nini hazijaisha majibu ni ngonjera mpaka asb; watu wanakula mpaka chakula cha wagonjwa kwa ulafi wao, leo wanaokataa elimu na afya bure wao wenyewe walisoma bure enzi za Mwl. NYERERE walisafirishwa bure na serikali . Elimu ilisimamiwa kwa umakini wa hali ya juu. Enzi zetu ilikuwa fedheha kusoma private school, kusoma shule za serikali ilikuwa ni ujiko. lakini sasa ccm wamechakachua shule za serikali leo kusoma private ni heri. shule za kitaifa leo limebaki jina kila kitu ktk shule hizo taabu tupu. Tunataka mtu atakayesema inatosha.

Naomba ondoa kichwani mwako neno haliwezekani kwani lisilowezekana kwako kwa mwingine linawezekana.

Nawaomba watanzania wenzangu (kasheshe and ccm members inclusive) tuwape wapinzani nafasi ya utawala, wakishindwa we vote them out. I think this is the dew time to put ccm aside and let us put someone else to the chair and see his performance.

We have to change our mind set. Ama sivyo tutaendelea kulia na tusisahau fimbo za ccm zinatuchapa wote hasa sisi raia wa kawaida.

Nimezaliwa tanzania, nimekulia tanzania, nitafia tanzania na kuzikwa tanzania muda wangu ulipangwa na mungu utakapofika hapa ndio kwetu

naipenda tanzania nawapenda watanzania
 
Back
Top Bottom