Kipi utaweza kukibadili....maumbile au tabia?

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,259
117
JF nashukuru kwa michango yenu!
Hilo swali nimekua nalisoma mara kwa mara kwenye maandiko mengi sana.
Kwako wewe unachangia vipi?
Tunawasilisha!
 
Yote yanawezekana kubadili...
Kama mhusika wa hayo mabadiliko ameridhia basi hakuna kinachoshindikana.
 
hili swali limekua na upana zaidi.
1-utakuta me/ke ameamua kuanzisha jambo ambalo atashauriwa kua si zuri jambo hilo...lakin kwa kua anayo mawazo yake na matumain yake...hatokubal kufuata ushauri huo.
2-tatizo litapomfika ataanza kuomba msaad mbali ,bali ili aepukane na matatiz hayo.
3-Imekuaje kati ya hayo mambo kwanza ule utashi wake au uamuzi wake.
Pili vipi aombe msaada baada ya kuamin alichokua ameamua hakikua sahihi.
 
Tabia inaweza kubadilika tena kwa kiwango kikubwa. Maumbile nayo yanabadilika ila kubadilika kwake ni kuongezeka au kupungua sio kubadilika kutoka ke kwenda me. Umeelewa maalim?
 
nasoma humu kuhusu tabia / maumbile kuyabadili...naona sijafaham undani wake ...wekeni ufafanuzi jaman.
 
tabia ipi itabadilika?
Maumbile nimewahi kusikia kuongezwa esp kwa akina dada wanaotafuta mambo mapya!
Japo nlisikia marhuum Wacko jack nae alitaka wambadilishe....nisaidie Husninyo vile utaweza!
 
Tabia inabadilika tena sana maana wote tunajifunza kutokana na makosa vile unavyojua kosa na ukaona kuwa ni kosa na ndipo unaporekebisha kwa hiyo unakuwa umebadili tabia.

vile vile tunaenda kanisani na tunapoomba msamaha kwa Mungu kuwa utusamehe makosa yetu kama sisi nasi tunavyowasamehe wale waliotukosea maana yake pia ni kubadilisha tabia zetu ziwe za uadilifu na kumpendeza Mungu na wanadamu pia, zisiwe za machukizo machoni pa Bwana Mungu.

Maumbile kuyabadili; hapa kwa mtizamo wangu ni kuwa unachotaka kubadilisha ni nini na kwa sababu gani? Maana kuna maumbile ya ugonjwa mfano mtoto amezaliwa ana kilema kinachorekebishika kwa daktari hapa ni kuwa unabadili lile umbile lake la ugonjwa na kumweka katika umbile la kawaida ambalo MUUMBA alikusudia awe nalo. Ila kubadili maumbile kama hao watu wazima wanaotumiwa dawa za kichina kisa hawataki kuwa na maumbile yale Muumba alowaumba nayo ni dhambi na hairuhusiwi.
 
Kuhusu kubadili maumbile ni rahisi sana kuna upasuaji mwanaume anaweza fanyiwa akawa mwanamke hivyo hivyo mwananmke akawa mwanaume. Pia kuna plastic surgery unaweza fanya sura yako iwe utakavyo. Tabia pia unaweza kuibadilisha kama wewe hupigi Campari,Smirnoff, au Malibu jaribu kuanza kupiga utaona tabia yako inarudi kinyume nyume.
 
Back
Top Bottom