Mbunge Chiwelesa Awasha Moto Bungeni: Wananchi Wananyanyasika Visomo Vyenu Vinawatesa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mhe Eng Ezra John Chiwelesa mapema Leo Feb 08, 2024 akichangia Bungeni amenukuu maneno kutoka katika Biblia Takatifu yanayompa binadamu mamlaka ya kutawala viumbe wote wa majini na wanyama wa mwituni Kishan akasema kuwa wananchi wengi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi na mapori tengefu hususani katika Jimbo la biharamulo wananyanyasika na kuteseka ikiwemo kunyang'anywa Mali zao kama vile Mifugo, kuni, baiskeli ama pikipiki na kupata kipigo pale wanapokutwa karibu na maeneo hayo hii ni kutokana na Sera mbalimbali zinazotungwa na wataalamu bila kuzingatia uhalisia wa maisha na mahitaji ya wananchi.

"Mhe mwenyekiti wananchi wanateseka Sana yani Mwananchi wa kijijini tena mwanamke akikutwa na kuni Tu pembezoni mwa mapori tengefu ananyang'anywa kuni na baiskeli yake, hivi mnataka huyu mwananchi atumie nini kupikia chakula wakati nishati pekee anayoitegemea NI kuni? Kama mnaweza Serikali itupatie njia mbadala ili wananchi wa vijijini wasitumie kuni" alisema Mhe Chiwelesa

Katika hatua nyingine Mhe Chiwelesa ameiomba Serikali na Mawaziri kuwasikiliza zaidi wabunge ambao Ni wawakilishi wa wananchi na si kusikiliza ripoti tu ambazo mara nyingi huwakandamiza wananchi huku zikiacha kusema manyanyaso ya wananchi hususani wafugani na wale wanaoishi vijiji vinanavyopakana pembezoni mwa hifadhi.

Aidha Mhe Chiwelesa aishauri Serikali kujenga uzio wa umeme (Electrical Fence) ili kuwazuia wanyama wa hifadhi kama Tembo kuingia katika maeneo ya wananchi na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mali zao. "M awaambia wananchi wapande pilipili ili kuwazuia tembo wasiingie vijijini mwao lakini bado mnawazuia wasifanye shughuli yoyote ndani ya Mita 500 akikutwa anakamatwa kaingia hifadhi hizo pilipili wazipande wapi?" Alisema Mhe Chiwelesa

Mnyamwezi Yuko kazini 🇹🇿🇹🇿🇹🇿

#bungetanzania
#tuliackson
#ezrachiwelesa
#innocentbashungwa
#neemarugangila
#olivasemguruka
#serikaliyaccmkazini
 

MHE. CHIWELESA AWAWASHIA MOTO MAWAZIRI ATIMBA NA BIBLIA BUNGENI ASOMA MAANDIKO, MNATAKA WANANCHI WA VIJIJINI WAPIKE KWA KUTUMIA NINI KAMA MNAWAZUIA KUTUMIA KUNI. WANANCHI WANANYANYASIKA VISOMO VYENU

Mnyamwezi Yuko kazini 🇹🇿🇹🇿🇹🇿

#bungetanzania
#tuliackson
#ezrachiwelesa
#innocentbashungwa
#neemarugangila
#olivasemguruka
#serikaliyaccmkazini
Kakutuma?
 
Back
Top Bottom