Kipi ni bora na busara zaidi kati ya kuasili mtoto na kulea mtoto wa ndugu?

Hamjawaza options za kuchakachua?

- "Zamani" kama wife ana tatizo, unapewa mdogo wake au mke anaridhia mume kuoa mke mwingine. Bahati mbaya katika ukristo hili halikubaliki. Siku hizi naona wengi wa wanaume wanapiga nje na kupata mtoto kwa siri ama kwa uwazi.
- "Zamani" kama mume anatatizo, wazee wanatafuta namna ya mdogo mtu ama kaka anapewa shughuli ya kupachika mimba. Inaweza kuwa kwa siri bila mume kujua au mpango wa wazi ambao mume anajua. Mwisho wa siku lakini mtoto anakuwa wako. Siku hizi hii option ni ngumu, lakini kimantiki mimi bado naona ina busara ndani yake. Haiharibu ukoo.

NB: Nimeuliza tu ili kupanua mjadala na kuingiza vionjo vya african solutions, sijakushauri chochote. Infantry Soldier
 
Kutaka mwenzako mwenye uwezo wa kuzaa asizae ili muwe sawa ni ubinafsi uliopitiliza.

Ukijua huna uwezo wa kuzaa kaeni mjadili na mkubaliane.
Kama kila mmoja atamvumilia mwenzie ndio muamue hivyo.
Lakini kama mwingine ana hamu ya kuwa na watoto wa kiuno chake muache aende akazae huko.
Kama hakutaka kuwa na watoto angeenda kuwa padri au sister basi.
Hakuna mtu anayeoa au kuolewa ili aishi tu na mtu wanaangaliana.!!
pia kumbuka ndoa ni zaidi ya kuwa na watoto ujue?
 
Hii thread imenigusa sana. Nilioa 2010 miezi michache baada ya kuhitimu my MD nilifanys hivyo ili kuhifadhi dini yangu hivyo nilimuambia mke wangu tutumie uzazi wa mpango mpaka Maisha yatakapokuwa stable. Mwaka mmoja na nusu baadae mambo yalikaasawa na sasa tukawa tayari kupata mtoto hivyo tuliacha kutumia uzazi wa mpango. Mpaka 2013 hakuna cha mimba wala mtoto, mke wangu akaingia wasiwasi hivyo akanishauri twende hospitali tukapime. Matokeo ya vipimo vya hospitali yalionesha nina obstructive Azospermia hivyo sina uwezo wa kuzaa labda kwa IVF tena kwa kutumia sperm extraction.

Nilimpa chaguo make wangu ukitaka anaweza kuishi na Mimi au tutengane,tukajadili na familia yake tukakubaliana tuendelee kuishi lakini baada ya miezi mitatu ndoa ilianza kukumbwa migogoro ambayo ilipelekea kuachana Mara ya kwanza hiyo 2013 tukarudiana ndani ya mwezi huo tukaja kuachana tena 2014 na tukarudiana ndani ya mwezi huo,mwisho Nov 2016 make wangu aliniaga anaenda kwao na hakukua ugomvi wowote lakini alibeba karibu vitu vyake vyote karibia mabegi mawili wakati kawaida yake akienda kwao anabeba begi Dogo tu mgongoni.

Nilishangazwa sana na hiyo kitu huku nikijua uenda hiyo ikawa mwisho wa ndoa yetu. Baada ya wiki moja nimpigia simu ananidai talaka na yeye na familia yake hawataki nikanyage kwao kwa mazungumzo ya aina yoyote na hiyo talaka niitume tu kwa basi. Nilifanya hivyo na hiyo nilikuwa talaka ya tatu na kwa mujibu mafundisho Uislamu hatuwezi kurudiana tena.

Ninasomesha ndugu kama watano na hakuna hata mmoja anayethamini kile ninachomfanyia na Sheria ya Uislamu ni haramu kufanya adaptation.
Pole sana mkuu, Inshallah Mola atakuruzuku
 
Better to adopt than to raise somebody else's child. They can't be trusted and will never put total trust in you, any mistake you make regarding their wellbeing will be taken or viewed as mistreatment, even the act of scolding them may lead to resentfulness towards you.
Well said! Adopted children are likely to remain faithful, thankful and loyal to you permanently than other person's children. I've learned this lesson after rearing both, several being my closer relative's children and only two as adopted. It turned that all went back to their parents and are now more closer to them than me but the adopted are even closer to me than my blood children! And I sincerely trust them more than my blood children!
 
mkuu, una maana watoto wako wa kuwazaa mwenyewe hawakupendi ukilinganisha na hao watoto wa kuasili?
 
Nitaenda kuadopt mtoto kutoka orphanage center wale wadogo kabisa asiyezidi miaka mitano. Nitampa ubini wangu kama nikikubaliwa na kumlea kama mwanangu wa damu. Atakuwa wangu
Mkuu Kama ni mtu wa Imani basi Mungu akuongozee katika hili ni wazo zuri
 
Zote sawa ila nilisaidia watoto wa ndugu nikawa ninawalipia ada na kuhudumia elimu. Nilisafiri na mawasiliano yakawa mabovu, Christmas ikafika sijatuma pesa ya shopping. Wasianze kulalamika mtu mwenyewe hana mtoto sijui pesa anapeleka wapi. Nilisononeka lakini nilijikaza wakamaliza shule na kuagana nao
Poleeee,
Binadamu hatuna shukrani,ni kweli ukilea mtoto wa dungu baadae huwa inaonekana kama ni jukumu lako,unaanza kuwa unakosolewa na kuingiliwa kwenye malezi
 
hapa wengi naona mnaongelea tamthilia za bara la ulaya na asia ila kiuhalisia kwenye ndoa labda wote muwe wagumba ila ikatokea mmoja mgumba na mwingine anajua ana uwezo wa kuzaa au kuzalisha hapo inakuwaga shughuli kukubaliana.
angalau wanawake mara nyingi huwaga waelewa inapotokea mume wake hawezi kuzalisha, lakini ikitokea mwanaume anazalisha halafu mwanamke hawezi kuzaa mara nyingi wanaume huwaga hatutaki kuambiwa habari za adoption wala kulea mtoto wa mtu,dawa yake huwaga ni kuchepuka tuu
 
Muumba ana hekima zake, huwa kunakuwepo watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki na kuna wanandoa ambao hawajabahatika kupata mtoto au watoto na wengine wana uwezo wa kulea watoto zaidi na wa kwao, naona kulea yatima ni bora hasa akiwa yatima huyo ni katika familia, ama kulea mtoto wa ndugu nadhani si busara ikiwa wazazi wapo, kama utataka kuwasaidia hao watoto bora uwasaidiye hao ndugu zako kiuchumi ili watoto waweze kuishi na familia yao halisi kwani mapenzi ya wazazi hayana mbadala.
 
Ni jambo jema kufikiria hivyo na kuwa na plan B, na ni lipi bora hasa mtoto wa ndugu au adoption, option zote inategemea matokeo unayoyatarajia kutokana na maamuzi yako
1.Ukiwa unataka tu kulea na kusaidia ndugu wanaweza kuwa option nzuri, ingawa option hii inachangamoto ya kuingiliwa na familia husika ya ndugu, na ukiwa na ndugu wa lawama inaeeza kukuweka ktk mazingira magumu( Nimeongea kwa kuzingazia evidence nilizoziona), hii option huwa naiona ni nzuri ukiwa na mtoto mmoja au wawili then ukawa na ndugu wa kusaidia, ila tegemea mtoto anaweza kuondolewa ktk familia yako muda wowote.

2.Option ya kuadopt binafsi naiona nzuri zaidi, kwanza unampa fursa mtoto ambaye angeweza kukulia ktk vituo vya watoto yatima ambavyo sio mazingira rafiki sana ya makuzi, pili unapata fursa ya kumlea kulingana na mnavyoona inafaa, kwa namna yenu na imani yenu, na huyu mtoto mtakuwa naye maisha yenu yote tofauti na ndugu.
Changamoto za kuingiliwa ktk malezi hazipo, na mtoto anakuwa akitambua kuwa nyie ndio wazazi wake.
Kwangu hii ni better option
===
Mkuu nimependa uchambuzi wako hasa kuhusu kumchukua mtoto wa ndugu. Binafsi nimekutwa na mengi sana kuhusu ndugu nimeapa sitafanya tena kumchukua ndugu nikaenae. Kama msaada nitaupeleka huko waliko. Nimepoteza miaka mingi naipigania familia ya ndugu zangu lakini hapa nilipo nimenyoosha mkono.

Kwangu binafsi naona badala ya kwenda kwenye nyumba za yatima ukamchukua mtoto mmoja ukamfanya wako, ni vyema ukafikiria pia option ya kuangalia familia duni ambazo zinajitahidi kuraisi na kufika juu. Usichague wale ambao hawaoneshi jitihada. Nimewahi kumkuta mama lishe anasomesha watoto high school watatu kwa kuuza chakula ambapo ukiangalia unashangaa anawezaje. Ukimsaidia mtoto wa aina hii akifanikiwa atasaidia ukoo na familia yake kubwa. Mtoto ukimuadopt anakuwa mmoja tu kwako. hawa ni sawa na kuotesha mmea wenye kuzaa matunda kwa wengi. So nenda tandale or mbagala or kokote kule hata kijiji cha mbali kabisa sio kwenu tafuta mtu mwenye sifa za kusaidiika msaidie.

hili ndilo wazo langu mkuu.
Nangu mandokwa
 
Hii thread imenigusa sana. Nilioa 2010 miezi michache baada ya kuhitimu my MD nilifanys hivyo ili kuhifadhi dini yangu hivyo nilimuambia mke wangu tutumie uzazi wa mpango mpaka Maisha yatakapokuwa stable. Mwaka mmoja na nusu baadae mambo yalikaasawa na sasa tukawa tayari kupata mtoto hivyo tuliacha kutumia uzazi wa mpango. Mpaka 2013 hakuna cha mimba wala mtoto, mke wangu akaingia wasiwasi hivyo akanishauri twende hospitali tukapime. Matokeo ya vipimo vya hospitali yalionesha nina obstructive Azospermia hivyo sina uwezo wa kuzaa labda kwa IVF tena kwa kutumia sperm extraction.

Nilimpa chaguo make wangu ukitaka anaweza kuishi na Mimi au tutengane,tukajadili na familia yake tukakubaliana tuendelee kuishi lakini baada ya miezi mitatu ndoa ilianza kukumbwa migogoro ambayo ilipelekea kuachana Mara ya kwanza hiyo 2013 tukarudiana ndani ya mwezi huo tukaja kuachana tena 2014 na tukarudiana ndani ya mwezi huo,mwisho Nov 2016 make wangu aliniaga anaenda kwao na hakukua ugomvi wowote lakini alibeba karibu vitu vyake vyote karibia mabegi mawili wakati kawaida yake akienda kwao anabeba begi Dogo tu mgongoni.

Nilishangazwa sana na hiyo kitu huku nikijua uenda hiyo ikawa mwisho wa ndoa yetu. Baada ya wiki moja nimpigia simu ananidai talaka na yeye na familia yake hawataki nikanyage kwao kwa mazungumzo ya aina yoyote na hiyo talaka niitume tu kwa basi. Nilifanya hivyo na hiyo nilikuwa talaka ya tatu na kwa mujibu mafundisho Uislamu hatuwezi kurudiana tena.

Ninasomesha ndugu kama watano na hakuna hata mmoja anayethamini kile ninachomfanyia na Sheria ya Uislamu ni haramu kufanya adaptation.
===
Sio haram but taratibu zake ni kwamba mtoto anahaki ya kujua asili yake. huwezi kutumia jina lako kwake.
 
Zote sawa ila nilisaidia watoto wa ndugu nikawa ninawalipia ada na kuhudumia elimu. Nilisafiri na mawasiliano yakawa mabovu, Christmas ikafika sijatuma pesa ya shopping. Wasianze kulalamika mtu mwenyewe hana mtoto sijui pesa anapeleka wapi. Nilisononeka lakini nilijikaza wakamaliza shule na kuagana nao
but now!! ushajaaliwa wana?
 
ndo maana una lalamika sana.punguza mizigo
 
Mtoto wa ndugu atakusumbua mpaka ukome.

Kila mara utasikia malalamiko kwa babaye au mamaye ananitesa ananitesa hata umfanyie nini.

Bora u-adopt mara 100,000,000,000 kuliko kulea mtoto wa ndugu.
 
Back
Top Bottom