Kipi kitaleta unafuu Mgogoro wa Zanzibar?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwa hali ilivyo hivi sasa Zanzibar kwa kuzingatia matamko yanayotolewa na vyama viwili hasimu inaonesha bado jitihada za kujinasua na mgogoro hua hazijafikia tamati.

Je, wewe kama mpenda demokrasia na amani unafikiri kipi kikifanyika hali itatulia na hakutakua na minong'ono ya hapa na pale kwa maslahi ya taifa la Zanzibar pamoja na kuendelea kulinda hadhi ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

1.Kumalizia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa October 25 ili Mshindi atakayepatikaña atangazwe na aapishwe?

2.Kurudiwa tena kwa uchaguzi chini ya tume mpya ya uchaguzi itakayohusisha wasimamizi wa kutoka nje na mshi kll.ndi atakayepatikaña atangazwe na kuapishwa?
 
Njia ni moja tu, nayo iko wazi sana. Mshindi wa uchaguzi wa October,25 atangazwe mshindi. Wazanzibar walishaamua nani wakuwaongoza ila Jesha na genge lake wakafanya uhuni tena uhuni mkubwa kabisa.
 
Hakuna sheria ya kurudia uchaguz.Tume ilitakiwa kutangaza matokeo kama walivyoyapata kutoka kwenye vituo.then mgombea ambae hatokubaliana na matokeo ndio aende mahakamani.kama utaratibu unavyoeleza.sasa huyo Jecha anaposema uchaguz haukua huru na wa haki kwan na yy alikua mgombea?
 
hakuna njia cha kufanya zaidi ya kumtangaza aliyeshinda na kuapishwa nawapongeza sana CUF kwa msimamo wao wameshaonyesha mpaka sasa.
Hivi demokrasia ni ccm kushinda tu?
 
kitakacholeta unafuu ni wao kuchinjana kwanza, alafu wakimaliza ndio watajua nini cha kufanya
 
Arudishiwe muasisi wa maelewano Amani karume urais wa Zanzibar cuf na Ccm wakae pembeni watatuumiza muda si mrefu. Ninaamini maelewano hayapo na hayatakuwepo
 
Back
Top Bottom