Kipi cha kujivunia sisi watanzania Kimataifa?

Kipi cha kujivunia sisi watanzania Kimataifa?

Tunaye aliyewahi kuwa rais na kuvunja record ya safari duniani
 
sisi ni waongo sana tunadanganya hata pasipohitajika!
 
Ukombozi wa bara la Africa, kumwondoa nduli Idi amini, kukomboa kisiwa cha nzuwani napia kuwafurumusha M23 na
Kiswahili.
 
Nchi ipo kisiasa zaidi pesa nyingi inapotelea huko!tunashindwa andaa academy za soccer!,,,leo nilitazama wabunge wakiapishwa aisee wale wabunge ni wengi mno!tungepunguza kundi la wabunge iwe wasizidi 100,wafutwe wakuu wa wilaya,wafutwe manaibu waziri tubaki na waziri tu...na waziri asiwe mbunge

Ndio kwanza wameongeza majimbo kwa ajili ya ulaji.
 
Mara nyingi, jinsi mlivyo pangika kijamii na kiuchumi, basi na michezo itaambatana hivyo hivyo. Kama kuna ukiritimba kwenye mfumo wa nani awe mahala gani ,uvivu wa kutaka kutoa jambo jipya kwa jitihada pekee kama wanasayansi, rushwa,kukosa uzalendo, ubinafsi, upendeleo, ufisadi, kupenda starehe kuliko uwezo halisia, uvivu basi unatinga mpaka kwenye michezo yenu. Ndio maana magufuli nyaraka zake zinasema Idara zishikwe na watu wenye taaluma husika Bila upendeleo. Huko mitaani bado kuna wachezaji wazuri lakini hatujui wako wapi tena

Well said mkuu.
 
Pembe za ndovu kupita julius nyerere airport kutoonekana na kukamatwa Uswiss hakuna taharifa tena,biashara ya twiga, Unga,passport kutoka kirahisi na wageni kuzitumia kwa matumizi haramu...
 
Kwenye michezo kiujumla hatumo, sio mpira wa miguu wala riadha.YAani sisi wa kupigwa 7-0.

Kwenye maendeleo hatumo, bado ni maskini wa kutupwa na hata baada ya miaka 54 ya uhuru, Uchumi wetu ni hali tete.

Kwenye haki na demokrasia hatumo, Rejea uchaguzi mkuu uliopita.

Sasa swali langu kwenu Watanzania wenzangu, nini cha kujivunia kwenye jumuiya ya Kimataifa sisi kama Watanzania?

HaIwezekani kura za wagombea zizidi idadi ya wapiga kura alafu tushinde,itakua ni miujiza!
Siku ambayo tutaweza kumanage rasimali zetu kwa mendeleo yetu ndio siku tutafanya vizuri kimichezo,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni
 
Mkuu tuna kipindupindu karibu nchi nzima! Hicho ni cha kujivunia kwa sababu wakitaka strain mbalimbali za vimelea vya kipindupindu basi watazipata hapa Tz
 
HaIwezekani kura za wagombea zizidi idadi ya wapiga kura alafu tushinde,itakua ni miujiza!
Siku ambayo tutaweza kumanage rasimali zetu kwa mendeleo yetu ndio siku tutafanya vizuri kimichezo,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni

heko mkuu.
 
Diamond platinum

Nilitegemea hili,hata hivyo ukitaka kujua sisi tunaongoza katika nini subiri uje kutajiwa jina la msanii mwingine wa kushindana na huyo,MAJUNGU.
 
Back
Top Bottom