SoC03 Kipato cha kila siku ni kitendawili cha maisha

Stories of Change - 2023 Competition

KABOYATU

New Member
May 8, 2023
3
2
Naam: Kiswali lugha adhimu iliyotukuka kwa semi za wahenga, nahau, methali, hadithi na vitendawili, Mmmh wataka kujua! nisikusimulie sana leo, kuna kitendawili kisemacho "Tega ni kutege" na jibu lake likawa " mwiba" Hahaaa😂 Sote twafahamu kuwa mwiba unachoma , wachoma wapi na saa ngapi? ajua aliyechomwa🙌

Maisha na matukio yake wakati mwingine huwa mwiba mkali na wenye maumivu makali sana😭, Katika mambo yote lililokubwa linaloweza kuukazia mwiba na maumivu yake ni ukosefu wa kipato cha kila siku🕊, miaka kadhaa iliyopita kule kijijini tuliumia na njaa huku mifugo ikifa kwa ukame faraja na matumaini yakiwa kusubiri mvua ili kuotesha mazao, watu walipoteza maisha kwasababu ya kukosa matibabu kwa kuwa fedha za matibabu hazipo na wasichana kuozesha bila kujali umri ikiwa ni faraja kwamba watapunguza utegemezi nyumbani lakini pia mahari inayolipwa kuwa sehemu ya kupunguza ukali wa mwiba maisha.

Naam!🎶bado upo na mie?💔🎙mmmh japo wakujichoma hauna pole , matibabu ni lazima ili uweze kusonga, wahenga wanasema "usiseme twafa sema nafa" japo tulikua tukiumia sisi lakini nje ya mipaka ya mkoa kulikua biashara mbalimbali ambazo ziliweza kupatia watu kipato, kisha kwenda mbali zaidi na kununua chakula.

Vijana tulikwenda katika maeneo hayo, na kujituma zaidi ujenzi, uvuvi, ujasiliamali, tukaweza kuikomboa jamii yetu, katika kipindi kigumu, lakini pia ikawa mwanzo mzuri wakuona furusa na kuinjengea jamii yetu maarifa na mzunguko bora wa kipato.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom