Kipanya leo!!

kipanya_30_-_03_-_2012_20120330_2086612363.jpg
Kazi ipo mwaka huu mpaka kieleweke!!!!
 
kwakweli kwa hali ya kawaida unaweza ukacheka lakini huo ni ujumbe mzito sana hasa kwa viongozi wetu tusione kama kipanya anafurahisha tu wasomaji lakini katuni yake inatoa ujumbe mkubwa sana kwetu wadau.
 
Hiyo ndio Tanzania; Tuna utajiri wa Gesi, madini ya thamani, vivutio vya utalii, ardhi yenye rutuba.....


Lakini bado tunaomba misaada nchi za nje, wananchi wanaishi kwa shida.

Katika Afrika Mashariki..... Tanzania ni nchi tajiri kuliko zote lakini ndio yenye wananchi wa hali ya chini wanaoishi kwa kipato cha chini ya Dola moja kwa siku....kuliko zote.

Mkuu wa kaya anaenda kuomba misaada nchi za Ulaya. .. ni aibu kubwa sana kuliko aibu zote Duniani.




MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hii ni kweli tu, kipanya hajaongopa, ni aibu kweli kwa rais wetu kuwa ombaomba, wakati nchi ina rasilimali lukuki, tatizo ni uongozi jamani, mpaka lini mambo haya.
 
Kwa wenzetu wa chama tawala wanakuambia huo ni upepo tu,pia kwa sasa rais yuko bize anapanga ratiba nchi za kutembelea kuomba misaada
 
mh! hii kali kweli na bado hatapata kokote kwani ata haendako urudi na shuti tuuu..... naona 2015 ipo mbali kwel hili watanzania tufaidi rasilimali zetu naipenda tanganyika na ninaichukia tanzania....
 
Yaani hapa ndipo huwa nafikiria mara mbili viongozi wetu huwa wanajisikiaje kuombaomba halafu wanaishia kufisidi hicho walichoomba!!!!Ni aibu na inatulazimu kama watanzania kuchukua hatua maana ni aibu yetu sote
 
"Ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi bora" in this quotation we lack Uongozi bora. Ili uwe kiongozi bora unahitaji akili, busara na kujitambua (self awareness). We are being led by people who have traces of all three. Kiongozi bora ni yule ambaye Watu wanamtaka aongoze na sio yeye anayetaka kuongoza. Viongozi tulionao wananunua uongozi. Matokeo tumekua kama mambumbu waliotajwa na Nyerere wanaobadilishana kichupa kwa almasi na wanabaki wakicheka kama mazuzu. Am just angry I would rather have a cold alcoholic drink and forget about being led by ****** with questionable moral values.
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom