Kipanya: Bado yuko na biashara mpaka kieleweke

Kipanya: Bado yuko na biashara mpaka kieleweke

Athari yake ni kubwa kuliko hii, pesa ikichukuliwa yote na mchina maana yake hawa watu wa kati spending power yao inakufa. Mathalan kama alikuwa anataka kujenga nyumba ya kuishi hatawaweza tena, watakaoathirika ni mafundi ujenzi, wauza vifaa vya ujenzi, malori ya kubeba vifaa kwenda saiti, mama ntilie wanauza kwenye site etc.. pia hawa wamama na mafundi wanaenda kupunguza matumizi mitaani kwao kama maduka ya mangi etc and the impact goes on.

Ujasiriamali wao ukifa, wao na staff wao waliowaajiri mwanzoni wanakuja kupambania vibarua vilivyopo, chako kinaweza kuporwa etc.

Wachina bora waende kuwekeza sehemu ambazo tulikuwa tunaagiza badala ya kuzalisha mwanzoni kwani inaongeza fursa zaidi kwa Taifa kama kwenye viwanda vikubwa etc. Ila huku kwenye uchuuzi waache waswahili though na wenyewe wateremshe bei.
Tutafute namna nyingine ya kuongeza mzunguko wa pesa na si uchuuzi. Maana hizi bidhaa akiuza mchina au mbongo zote hela inaenda China, maana ndiko tunakozitoa. Kinachofanyika ni wabongo kuongeza cha juu kama madalali, hicho ndicho ambacho wewe unakiita kinaongeza spending power. Hao wholesalers wachukue hizo hela wakaunde viatu, mikoba, chupi, na vikorokoro vingine ambavyo tutaviuza hata kwa hao wachina. Hapo ndipo tutatengeneza ajira za kweli.
 
Ni rahisi sana kama huna biashara halaf una type nyuma ya keyboard.
Hayo ji maish ya watu, usiongee kirahis rahis
Mkuu, wafanyabiashara si wanapambana sana kwenda China kuchukua mzigo wao wenyewe? Kwa nini wasikae tu wasubiri supplier mmoja awauzie? Sio kuwa wanafuata wenyewe China ili kuongeza faida kwa kuwa wanapata mzigo direct?? Sasa iweje wao waone kufuata direct Guangzhou ni sawa ila mchina kuja direct kutuuzia huku mitaani sio sawa??
 

Attachments

  • IMG-20250320-WA0049.jpg
    IMG-20250320-WA0049.jpg
    16.3 KB · Views: 15
Ni mtu mpumbavu pekee ambae haioni athali ya wachina kuivamia nchi yetu na kuilaruwa kihun.

Mwaka Jana nilienda mkoani kwetu/kijijini nilishangaa kukuta wachina wanamuliki maeneo makubwa makubwa wanafanya uchimbaji madini, Kila sehemu zilizokuwa zikihisiwa Zina madini kipindi Cha nyuma sasa hivi machina yamechukuwa hayo maeneo yanachimba madini kwa fujo. Wananchi wa maeneo hayo shughuli zao kubwa ilikuwa ni kilimo lkn sasa hivi wametelekeza kilimo Kila mwanaume na kijana wanahangaika na vibarua vya ujira mdogo mno kwenye hiyo migodi ya wachina. Kwa sasa maeneo hayo Yana dhiki kubwa ya chakula yanii simu za njaa haziishi kumbe watu wametelekeza mashamba wako migodini.

Serikali isipotoka usingizini kudeal na Hawa wachina hakika taifa litaenda kupata hasara kubwa siku za mbeleni. Hii mnayoiona kariakoo ni Cha mtoto kama unandgu Yako yuko kijijini huko ndani ndani muulizie habari za wachina atakwambia, vijamaa vinafika sehemu ambazo huwezi kutarajia.watu wa mkoa wa Mara nadhani mnanielewa.
 
Waachen wachina mbona wahindi wanadunda tu na waungishana wao tu kwa deals kubwa huku wakikusanya kutoka kwa waswahili.
 
Mwaka Jana nilienda mkoani kwetu/kijijini nilishangaa kukuta wachina wanamuliki maeneo makubwa makubwa wanafanya uchimbaji madini, Kila sehemu zilizokuwa zikihisiwa Zina madini kipindi Cha nyuma sasa hivi machina
Wamekuta mamalaka zilizolala usingizi
 
Zamani chain ilikuwa na watanzania watatu.. mmoja anatoa mzigo China anapeleka Kariakoo, mwingine anaufata Kariakoo anaenda kuuza Tabora mjini na mwingine anachukua Tabora anaenda kuuza wilayani Sikonge..

Mchina sasa hivi anauza mwenyewe hadi Sikonge hivyo watanzania wote kati shughuli imekufa..

Faida kwa mnunuzi wa mwisho bei inaweza kupungua kidogo lakini hasara kwa hawa wafanyabiashara na Taifa kwasababu hii faida ya kati sasa nayo inaenda China badala ya kubaki kwa watanzania.
hapo nimekupata kiongoz
 
Kama tuna nia hasa ya kudeal na Wachina basi tuyafungie yale madubwi yao. Ule ndiyo utopolo. Ila kutaka kuwakataza wao kuleta bidhaa ambazo tulikuwa tunazifuata wenyewe China ni unafiki mwingi na ulaghai.
 
Tutafute namna nyingine ya kuongeza mzunguko wa pesa na si uchuuzi. Maana hizi bidhaa akiuza mchina au mbongo zote hela inaenda China, maana ndiko tunakozitoa. Kinachofanyika ni wabongo kuongeza cha juu kama madalali, hicho ndicho ambacho wewe unakiita kinaongeza spending power. Hao wholesalers wachukue hizo hela wakaunde viatu, mikoba, chupi, na vikorokoro vingine ambavyo tutaviuza hata kwa hao wachina. Hapo ndipo tutatengeneza ajira za kweli.
Hawa wachina wanaopigiwa kelele kila kukicha ni wachuuzi, wengi wao si wamiliki wa hivyo viwanda huko China. Si pesa zote zinaenda China akiuza mtanzania kwenye hii chain, tatizo la watanzania ni bei maradufu wanayoongeza.
 
Back
Top Bottom