Kipandauso (migraine): Chanzo, Dalili, Tiba na jinsi ya kujikinga na tatizo hili

Nakushauri ukafanye kipimo cha CT Scan , kabla ya kufata shauri nyingi zitakuchanganya
Niliwahi fanya regent hospital na Apollo hospital India, kote huko sikukutwa na tatizo lolote, madaktari waligundua kuwa ni hiyo migraine niliieleza hapo awali.
 
Kuna theories nyingi zinazoelezea pathophysiology(mechanism) ya jinsi tatizo hili linatokea,lakini hakuna hata moja iliyokubalika universally.Lakini pia hakuna dawa hata moja iliyothibitika kutibu/kumaliza tatizo hili universally.Ila kuna vitu kadhaa vinavyokubalika universally,juu ya ugongwa huu.

1.Watalamu wote wanakubaliana kwamba hakuna uhakika wa nini hasa kinasababisha ugonjwa huu(kuna theory nyingi).

2.Walamu wote wanakubaliana kwamba hakuna dawa ya uhakika inayotibu/inayomaliza tatizo hili kwa wagonjwa wote.

3.Watalamu wote wanaclassify type 2 za migraine headache: Typical na Atypical-Typical migraine ina classical signs & symptoms("Zigzag silvery" vision dakika kadhaa kabla ya kichwa kuanza kuuma,Unilateral headache yaani kichwa kinauma upande mmoja wa uso,Kichefuchefu na mdomo kujaa mate au kutapika kabisa,photophobia yaani mgojwa hapendi kuona mwanga,kichwa kuuma kwa masaa hadi siku kadhaa kisha maumivu yanapotea kabisa) Kwa upande wa Atypical migraine,dalili hizo nilizotaja sio lazima zionekane zote kwa wakati mmoja.

4.Watalamu wanakubaliana kuwa kichwa kikishaanza kuuma hakuna dawa yoyote ya kumeza ya maumivu inayofanya kazi vizuri.Hii ni kutokana na kwamba kunakuwa na slow down ya gut movement na decreased absorption tumboni(stomach & intestines).Dawa utameza lakini haitafanya kazi vizuri kama inavyotegemewa.

5.Watalamu wanakubaliana kuwa kupona kwa maumivu hakutegemei dawa,kwa maana kwamba hata usipotumia dawa muda ukifika maumivu yanaondoka yenyewe.

6.Kuna utafiti umeonesha kwamba kadiri umri unavyozidi kwenda,frequency ya attacks inapungua! Pia wengine wanasema hata intensity ya maumivu hupungua,ingawa hii haijakubalika sana.

7.Hakuna data wala ushahidi unaoonesha kuwa migraine inaweza kupelekea mtu kupata uchizi,wala kifafa,wala kifo! Isipokuwa kuna taarifa za kuwepo idadi ndogo sana ya wagonjwa waliopata matatizo ya kuona ingawa bado haijathibitika kama ni kwa sababu ya migraine.

8.Pia takwimu zinaonesha kuwa,ungonjwa huu unaanza kuonekana baada ya kipindi cha utoto kupita.Mara nyingi watu huanza kuupata ukubwani,na inaonekana wanawake wanaathirika kwa wingi kuliko wanaume kiuwiano.

9.Pamoja na kwamba ugonjwa huu unaanza kuonekana zaidi ukubwani,lakini watalamu wanasema huu ni ugonjwa wa kurithi.Kwa hiyo ndugu yangu kama ndio hivyo,inawezekana tatizo hili lipo kwenye familia yenu! Mimi kwetu upo!

10.Watalamu pia wanasema kwa kuwa hakuna uhakika hasa ni nini sababu ya tatizo hili,wanasema,upo uwezekano wa tatizo hili kupotea bila tiba yoyote ya maana.Hapa ndipo kidogo kuna ukakasi,maana wapo watu wameombewa wakapona,wapo waliotumia dawa za wamasai wakapona nk.,nk,nk. sasa huko siwezi kwenda zaidi!

Kwa nini nimetoa mchango wangu hapa? Mimi pia ni mhanga wa tatizo hili tangu nikiwa na umri wa miaka 14.Binafsi mimi ni mwanachuo ktk chuo kikuu fulani cha udaktari hapa nchini.Na kiukweli,kwa jinsi ugonjwa huu ulivyonitesa,naweza kusema,ndicho kichocheo kikubwa kilichonifanya nisome kozi hii.

Kwa sasa frequency imepungua sana;mwanzo nilikuwa napata attacks hata mara mbili hadi tatu kwa wiki,ila siku hizi ninaweza kukaa hadi miezi minne sijapata attack kabisa.Hata intensity nahisi imepungua tofauti na mwanzo;ingawa inawezekana labda ni kwa sababu nimeishazoea.Usually mimi maumivu huwa masaa 2-3 baada ya hapo nakuwa mzima kabisa na ninaendelea na shuguli zangu as usual.

But all in all maumivu ni makali jamani,asikwambie mtu.Every shughuli is shut down;huwezi kufanya chochote.

Nise tu pole kwenu ndugu yangu,maana na mimi naufahamu muziki huo!

Ndugu bandiko lako limenitia moyo sana. Asante kwa bandiko nzuri. Naamini hata mie ipo siku nitapona huu ugonjwa wa ajabu.
 
Wapi madaktari wa Jamii Forum?
Mkuu Dogo Tundu Achana na kutumia Dawa za kizungu tumia dawa yangu ya Asili ya Ugonjwa wa Kipanda Uso Migraine : kuumwa na Kichwa Upande mmoja mimi nitachangia dawa yangu ya asili ni hii hapa :

Grapes juice: Juice ya zabibu zilizoiva ndio dawa ya migrane, utumie kiwango kidogo cha juice hiyo atumia hadi atakapo ona kuwa amepata nafuu! Inshallah itamsaidia shemeji atumie kisha uje hapa unipe Feedback.

Grape Juice Juisi ya Zabibu Dawa ya Ugonjwa wa Kipanda uso Migraine. Chanzo. MziziMkavu Mtafiti wa Dawa za Mitishamba.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Dogo Tundu Achana na kutumia Dawa za kizungu tumia dawa yangu ya Asili ya Ugonjwa wa Kipanda Uso Migraine : kuumwa na Kichwa Upande mmoja mimi nitachangia dawa yangu ya asili ni hii hapa :

Grapes juice: Juice ya zabibu zilizoiva ndio dawa ya migrane, utumie kiwango kidogo cha juice hiyo atumia hadi atakapo ona kuwa amepata nafuu! Inshallah itamsaidia shemeji atumie kisha uje hapa unipe Feedback.

Grape Juice Juisi ya Zabibu Dawa ya Ugonjwa wa Kipanda uso Migraine. Chanzo. MziziMkavu Mtafiti wa Dawa za Mitishamba.

Ndugu MziziMkavu, nimeona na kufatijika na bandiko lako, sasa hiyo juice naipata wapi? Pia namba nipm namba yako ili nifanye mawasiliamo na wewe moja kwa moja, kwa ushari zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kuna mtu akipatwa na hiyo hali yeye huwa anatumia oxygen, embu siku ukiumwa nenda hospital na uwaombe tu wakuvishe mask uvute hiyo hewa uone kama nawe itakusaidia, na kama itakusaidia itabidi ununue mask na mtungi wa kuifahia hiyo hewa ukae nao nyumbani na huku ukiendelea kutafuta dawa itakayokuponya kabisa, oxygen ni kwa ajili ya kuondosha maumivu tu yajapo, pole sana mkuu ni ugonjwa unaotesa sana.

Ndugu MziziMkavu, nimeona na kufatijika na bandiko lako, sasa hiyo juice naipata wapi? Pia namba nipm namba yako ili nifanye mawasiliamo na wewe moja kwa moja, kwa ushari zaidi.
 
Nakushauri ukafanye kipimo cha CT Scan , kabla ya kufata shauri nyingi zitakuchanganya

Unadhani CT scan itaona nini mkuu? Maana mpaka sasa hakuna theory iliyokubalika globally hasa Migraine inatokeaje. Unafikiri wao hawajapata wazo la kutumia CT scan?
 
Du,ungekuwa unaleta post kama hizi za kusaidia jamii ungekuwa mbali sana.Anyway mambo mengine ni imani.Ila du chumvi?!
 
Wadau,kuna mzee hapa amesaga chumvi ya mawe ameloweka kwenye maji kukiwa na kitambaa.Amechukua kitambaa amekiweka pajini

MAAJABU YA CHUMVI
Stori kuhusu chumvi:

Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi. Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.

Tunaambiwa chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho bora kwa afya zetu.

Ukweli kuhusu chumvi:

Mpaka zama za pili za mawe (middle stone ages), hakuna chumvi iliyokuwa mbaya. Waharifu waliuliwa gerezani kwa kupewa chakula bila chumvi, iliwasababishia kifo cha taratibu.

Miaka 2000 iliyopita, chumvi ilitumika kama hela. Dhahabu na Chumvi vyote vilikuwa na thamani sawa. Neno 'salary' (mshahara) linatokana na neno 'salt' (chumvi).

Hapa kwetu Tanzania, watu hutumia msemo, 'Nimekula chumvi nyingi' kumaanisha kuishi miaka mingi.

Katika siku hizo za kale, chumvi ilitumika pia kuhifadhia vyakula. Siku hizi tunatumia rifrijereta, kwa hiyo chumvi chache inahitajiwa isipokuwa kwa matumizi machache ya kusokotea nyama.

Wanyama wote wenye damu moto, lazima wawe na chumvi ili kuishi. Ubongo wa binadamu pamoja na uti wa mgongo, vimo katika mfuko wa maji chumvi uitwao 'cerebrospinal fluid (csf)'. Umajimaji huu huzunguka sehemu zote za ubongo na uti wa mgongo.

Sote tulitumia miezi tisa kuishi katika mifuko ya uzazi ya mama zetu inayoelea kwenye maji chumvi (amniotic fluid).

Machozi yetu ni chumvi na tunatokwa na jasho ambalo pia ni chumvi. Mifupa yetu ina uwazi katikati yake (uboho) ambamo seli za damu hutengenezwa. Uboho huu umefunikwa na tabaka nyingi za chumvi kalisiamu kama vile kamba inavyoshikizwa pamoja. Kowa chumvi (salt crystals) zinashikizwa pamoja na kalisiamu, na kowa hizi ndizo zinazoifanya mifupa yetu kuwa imara, na siyo kalisiamu pekee.

Mifupa inamiliki asilimia 27 ya chumvi yote mwilini. Wakati mwili unahitaji chumvi zaidi, huikopa toka mifupani, jambo hili likitokea, kalisiamu huondolewa pamoja na chumvi na kuifanya mifupa kuwa miembamba, laini na midhaifu.

Chumvi imeundwa kwa Sodiamu na Klorini, kwa pamoja inaitwa; 'Sodiamu Kloridi' (Na Ci).

Sodiamu ni metali laini yenye chaji chanya (+), wakati Klorini ni gesi yenye chaji hasi (-) ambayo hubadilika kuwa katika hali ya umajimaji inapoongezewa shinikizo.

Klorini ni gesi au umajimaji, lakini kwa namna fulani wakati dunia imeumbwa, klorini ilibadilika kuwa ngumu pamoja na sodiamu na madini mengine. Unaweza kuisaga chumvi na kuwa katika unga, klorini bado itabaki na sodiamu.

Klorini katika hali ya ugumuugumu, huitwa Kloridi.

Chumvi tutumiayo siku hizi inatoka katika bahari, maziwa, mito au katika migodi ya chumvi. Zaidi ya sodiamu na klorini, chumvi yote kwenye sayari yetu huja pamoja na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake!.

Kwa hiyo tunaweza kuona ni jinsi gani madini hayo yalivyo na umhimu kwetu, la sivyo yasingeshikamanishwa na chumvi. Kwa sababu ya thamani yake kibiashara, madini hayo huondolewa ili kutengeneza faida kubwa.

Mwili wa binadamu una uwezo wa kuienguwa klorini kutoka katika sodiamu kadiri inavyohitajika. Damu yetu huihitaji klorini kama zifanyavyo ogani zingine ndani ya miili yetu.

Tumbo huitumia klorini kutengeneza haidrokloriki asidi inayohitajika ili kuuwezesha mfumo wa umeng'enyaji chakula kufanya kazi vizuri.

Miili yetu pia huitumia sodiamu kloridi kama chumvi kuufanya ubongo, uti wa mgongo, machozi, mifupa, tezi za jasho, ogani na damu kufunikwa na chumvi.

Mwili unanufaika pia kutoka katika madini mengine yaliyomo katika chumvi ili kuuweka katika hali ya ualikalini na afya.

Ni kama na vile kwa kunywa maji kuzidi kunaweza kumuua mtu (hyponatremia), vivyo hivyo kwa kutumia chumvi kuzidi, kunaweza sababisha; uvimbe, kuharisha na kifo.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile 'aluminium silicate' huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Sodiamu iliyozidi inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vingi vyenye viongezi (additives) vya sodiamu. Sodiamu siyo chumvi, chumvi ni sodiamu-kloridi. Sodiamu bikaboneti, sodiamu benzoeti na monosodiamu glutameti (msg) ni baadhi ya viongezi hivyo.

Sodiamu, potasiamu na kloridi ni elektrolaiti (madini maalumu) ambayo huyeyuka katika maji na kubeba chaji za kiumeme na kuzipeleka sehemu zozote za mwili kuliko na maji. Madini haya yenye chaji za kiumeme yana uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya seli kwa uhuru wote, huku yakipeleka lishe ndani na kubeba nje taka na maji yaliyozidi ili kuiacha seli katika hali yake ya usawa (balanced cell).

Wakati huo huo, kadiri elektrolaiti hizi zikitembea ndani na nje ya seli na kufanya mabadiliko yake, usawa maalumu wa Potasiamu ndani ya seli lazima utunzwe kwa kiasi maalumu cha sodiamu na kloridi ili kuishikilia potasiamu ndani katikati ya seli.

Elektrolaiti zinapatikana kwenye majimaji yote mwilini na hubeba mapigo (impulses) kwenye neva zetu. Kitendo hiki huusaidia moyo na kiwambo cha moyo (diaphragm) kusinyaa na kulegea.

Elektrolaiti hubeba Glukozi (damu yenye sukari) na kuipeleka ndani ya seli baada ya Insulini kufungua milango kwa ajili ya sukari kuchukuliwa.

Elektrolaiti pia huwasha pampu za kuzarishia nguvu ziitwazo kwa kitaalamu 'Cation pumps' ambazo huzarisha umeme ambao huifadhiwa kwenye beteri zijulikanazo kwa kitaalamu kama 'mg Adenosine Triphosphate (mgATP)' na 'mg Guanosine Triphosphate (mgGTP)' za mwili.

Ikiwa mtu atapungukiwa kwa kiasi kingi cha Elektrolaiti hizi kutokana na kuharisha au kwa sababu ya dawa za kukojosha (diuretics), anaweza kuwa mgonjwa sana na itamlazimu kwenda hospitali kupewa elektrolaiti hizi katika mfumo wa dripu (intraveneous fluid, IV), kama vile; maji chumvi (saline solution), maji sukari (dextrose fluid) na madini.

Siku hizi vinywaji vyetu vingi baridi vinaongezwa kafeina ambayo ni kikojoshi kinachoyalazimisha maji kutoka ndani ya mwili na kutusababishia upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, hakuna kinywaji ambacho ni mubadala wa maji.

Wanasayansi na madaktari bado hawaelewi ni kwa jinsi gani chumvi huyeyuka ndani ya maji au ni kwa vipi iwezavyo kuendelea kuwa na hali ya uchumvi na uchumvi. Wanasayansi na wanakemia wana baadhi za nadharia, lakini bado hawajaweza kuzithibitisha. Bado imebaki kuwa ni fumbo (mystery).


BAADHI YA KAZI ZINGINE MHIMU ZA CHUMVI MWILINI:

  • Chumvi huyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli. Inarekebisha uwiano sawa wa kiasi cha maji yaliyopo nje ya seli. kuna bahari mbili za maji ndani ya mwili, bahari moja imejishikiza NDANIya seli, na bahari nyingine ya pili imejishikiza NJE ya seli. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa ujazo wa maji uliopo baina ya bahari hizi mbili, na usawa huu unawezeshwa pekee na chumvi, chumvi ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi.
  • Chumvi husaidia kuondoa dalili za mfadhaiko (stress).
  • Figo hazitaweza kufanya kazi zake vizuri bila chumvi.
  • Kukata tamaa na matatizo ya kisaikolojia, vitaondolewa kwa kuchukuwa chumvi zaidi, kula mlo kamili na kufanya mazoezi ya kutembea.
  • Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanaweza kurudishwa katika hali yake ya kawaida kwa kuchukuwa kipande cha chumvi na kukiweka mwishoni mwa ulimi na kukifanya kiyeyuke.
  • Mifupa inapata uimara wake toka katika chumvi, na siyo katika kalisiamu pekee.
  • Je wewe ni mwanaume na unashindwa kuhimili kusimama? unahitaji chumvi zaidi na kunywa maji halisi zaidi.
  • Kuichukuwa chumvi na kunywa maji kabla ya mazoezi, kutakusaidia kupumua vizuri na kutokwa na jasho chache.
  • Matatizo ya kibofu cha mkojo na upotevu wa mkojo wa makusudi, vingeweza kurekebishwa kwa kuongeza chumvi zaidi kwenye mlo wako.
  • Dalili za maumivu ya jongo (Gout) zinaweza kuzuiwa kwa kutumia chumvi.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia kuvimba kwa mishipa na vena kwenye miguu.
  • Kwa sababu tunapata potasiamu karibu katika kila chakula tunachokula, chumvi inatakiwa kuongezwa katika milo yetu, hii itairuhusu miili yetu kuhimili usawa sahihi wa maji kati ya bahari ya ndani na ile ya nje ya seli.
  • Chumvi ni mhimu ili kuondoa asidi iliyozidi kwenye seli, hasa seli za ubongo.
  • Chumvi ni mhimu kwa ajili ya kusawazisha kiasi cha sukari kwenye damu, hivyo kuzuia ugonjwa wa kisukari.
  • Chumvi ni mhimu katika uzarishaji wa nguvu umeme itokanayo na maji katika seli zote za mwili.
  • Chumvi ni mhimu katika mawasiliano ya neva na ufanikishwaji wa taarifa wakati wote seli za ubongo zinapofanya kazi tangu kuzaliwa hadi kufa.
  • Chumvi ni mhimu katika umeng'enywaji wa chakula na madini kwenye utumbo mdogo (intestinal tract).
  • Chumvi ni mdhibiti madhubuti dhidi ya histamini.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia mikakamao ya mishipa (cramps).
  • Chumvi ni mhimu katika kusafisha makohozi na kubana kwa kifua.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia uzarishaji wa kuzidi wa mate katika kiwango kwamba yanatoka nje ya mdomo wakati umelala, kitendo hiki cha kutoa mate (udenda) wakati umelala ni dalili ya upungufu wa chumvi mwilini.
  • Chumvi ina umhimu mubwa katika uimarishaji wa mifupa. Ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya upungufu wa chumvi na maji mwilini.
  • Chumvi ni mhimu katika usafishaji wa makohozi mapafuni na maji yaliyogandamana hasa kwa watu wenye pumu, ikiwa inakulazimu kusafisha koo kila wakati, ni dalili kuwa umepungukiwa chumvi.

CHUMVI KIASI GANI?:
Dr.Batmanghelidj anashauri; ¾ (robotatu) gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji (16 ounces), au nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji, au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji tunayokunywa. Hiki ni kiasi kizuri kwa kuanzia na siyo kanuni, tafadhari tumia aina ya kijiko kilichotajwa hapo juu kwa vipimo sahihi.

Ukiona viwiko, vidole au kope za macho zinavimba, usitumie chumvi kwa siku 2, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena.

NAMNA ZA KULA CHUMVI:
Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.

Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.

Unaweza pia kunywa nusu ya maji unayotaka kunywa, kisha utamungunya taratibu chumvi mdomoni kama ulavyo pipi, na kisha umalizie nusu ya maji iliyobaki.

kuichanganya chumvi pamoja na maji ya kunywa si wazo zuri sana.

Muhimu: Tumesema chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini madini mengine zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake, lakini hatuwezi kubeza umhimu wa madini joto (iodine) kwa afya ya mwili, ikiwa ni hivyo basi, tunashauri kwa wale ambao hawana vyanzo vingine vya madini hayo ya joto kutumia chumvi zote mbili yaani robo tatu ya matumizi yawe chumvi ambayo haijasafishwa na robo nyingine iwe ile iliyosafishwa ili kuepuka kupungukiwa madini hayo mhimu. Tunasisitiza katika chumvi hiyo iliyosafishwa hakuna kingine kilicho mhimu zaidi ya madini hayo joto ambayo yanaweza kupatikana pia kwa kula vyakula vingi vya baharini (sea foods).


Mchungaji Stan Moore wa kanisa la Woods of life fellowship la Pembrook Florida nchini Marekani anasema aliuona ukweli kuhusu tiba kwa kutumia maji aliposoma biblia wafalme wa pili 2:19-22.
 
Mkuu Fadhil Paulo umenikuna sana juu ya mada hii.Sijajua mada ya Crispin hapo juu kuhusu kutibu kipanda uso.Vipi ikoje?
 
Ndugu zanguni nisaidieni kunifamisha dawa ya ugonjwa wa kipanda uso,kwa sababu huu ugonjwa unanisumbua sana na naumwa nikiwa katika hali ya hasira, njaa,shibe kupitiliza na mawazo nisaidieni jamani nateseka sana.
 
pole sana ndugu yangu nilikuwa na tatizo kama lako ila kuna mzee alinichanja dawa miaka kama 10 iliyopita hadileo sijasumbuliwa huyo mzee alikuwa anaishi vingunguti sijui kama bado yupo
 
Kipandauso ni moja ya madhara ya msongo wa mawazo unaotokana na mapenzi (utapiamlo wa tendo la ndoa). Hili huwapata zaidi wanawake kwa kuwa hawana maamzi zaidi juu ya kipimo wanachopata kwenye tendo la ndoa, yaani mwanamke anaweza kuwa anahitaji mf round 3 mwanamme akawa ni mvivu. Moja ya dawa mhimu ya kipandauso ni kufanya tendo la ndoa kwa standards, kwa namna ambayo ifikie kusema huna presha za tendo la ndoa, hutaki acha.
 
Ndugu zanguni nisaidieni kunifamisha dawa ya ugonjwa wa kipanda uso,kwa sababu huu ugonjwa unanisumbua sana na naumwa nikiwa katika hali ya Hasira,njaa,shibe kupitiliza na mawazo nisaidieni jamani nateseka sana.
Mtambuzi Njoo utoe tiba huku. Pole sana.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zanguni nisaidieni kunifamisha dawa ya ugonjwa wa kipanda uso,kwa sababu huu ugonjwa unanisumbua sana na naumwa nikiwa katika hali ya Hasira,njaa,shibe kupitiliza na mawazo nisaidieni jamani nateseka sana.

Wasiliana na Zitto
 
Last edited by a moderator:
Dawa ya Maradhi ya Kipanda Uso Migrane: Grapes juice: Juice ya zabibu zilizoiva ndio dawa ya migrane, utumie kiwango kidogo cha juice hiyo atumia hadi atakapo ona kuwa amepata nafuu! Inshallah itamsaidia shemeji atumie kisha uje hapa unipe Feedback.

JUISI YA ZABIBU.jpg

Grape Juice Juisi ya Zabibu Dawa ya Ugonjwa wa Kipanda uso Migraine. Chanzo. MziziMkavu Mtaalam na Mtafiti wa Dawa za Mitishamba.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom