Kipandauso (migraine): Chanzo, Dalili, Tiba na jinsi ya kujikinga na tatizo hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipandauso (migraine): Chanzo, Dalili, Tiba na jinsi ya kujikinga na tatizo hili

Discussion in 'JF Doctor' started by Raia Fulani, Apr 9, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Huu ugonjwa upo sana na utambuzi wake ni mgumu. Naomba kupata empirical data na evidence kuhusu kipandauso pamoja na dawa (za kienyeji na kisasa) pamoja na wapi matibabu yanapatikana. Kuna mdau anahisi anacho.  ====== Majibu kutoka kwa Mzizi Mkavu ======

   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280

  Kuumwa na kichwa / kipandauso

  Maumivu ya kawaida ya kichwa huweza kutulizwa na dawa za kuzuia maumivu za aina ya Panadol au aspirini.Iwapo unahisi hayo maumivu kwenye kipji cha uso wako, mashavuni na sehemu zilizo karibu na macho zikifura, kuna uwezekano kuwa umeambukizwa sehemu za kukaza pumzi puani.Iwapo utashikwa na maumivu makali ya kichwa ambayo hayapoi, haikosi kuna uwezekano kuwa umeanza kushikwa na ule ugonjwa sugu wa kipandauso.
  Kipandauso (migraine) kina maumivu zaidi kuliko kuumwa kichwa kwa kawaida.Kipandauso huathiri upande mmoja wa kichwa na kuleta kisunzi,au kutaka kutapika.Iwapo unahisi kipandauso unaweza kuona vimulimuli kutokana na muangaza.Pia unaweza kuhisi maumivu makali kwenye jicho moja mara kwa mara.
  Ukipatwa na kipandauso, muone daktari wako akuchunguze ili akupe ushauri .Unapopatwa na kipandauso lala chini palipo na utulivu katika chumba kilicho giza kuzuia miale ya jua yanayosababisha kichwa kiume zaidi.
  Jaribu usinywe kakao, pombe ama kinywaji chochote kilicho na kakao.Hivi vinaweza kusababisha kipandauso, kunywa maji mengi kila siku.
  Utahitajika kumuona daktari ikiwa:

  • Unaumwa na kichwa na hakipoi kwa muda wa juma moja ingawa umemeza dawa za kuzuia maumivu.
  Utahitajika kwenda kwa chumba cha dharura ikiwa:

  • Una matatizo unapozungumza, au unasikia kizunguzungu, miguu haina nguvu. Kuna uwezekano kwamba umeanza kupatwa na ugonjwa wa pigo.
   
 3. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  wadau mke wangu ana matatizo ya kuumwa kichwa kwa miaka mingi, awali nilifikiri ni kwa sababu ya matatizo ya macho, Kweli alipimwa na baadae kupewa miwani. Sasa tatizo hilo limekuwa kubwa kiasi kwamba akitumia computer kwa muda fulani tu hali inajirudia kiasi kwamba hata kunyanyua kichwa inakuwa ngumu Wadau dawa gani nitumie maana kila hospitali ya hapa jijini ametibiwa lakini wapi. Msaada plzeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Zitto kabwe alipelekwa India kwa kuugua kipanda uso! mtafute ZZK akupe ushauri.
   
 5. a

  artorius JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole sana kwa matatizo,your wife needs to be assessed by a neurologist to make a proper diagnosis.Nenda muhimbili yupo na pia kcmc yupo.Epuka kutumia madawa bila kujua tatizo ni nini.
   
 6. M

  Masterproud JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 443
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kugundua chanzo cha tatizo ni hatua moja ya kulitatua. Mshauri apunguze matumizi ya computer au weka kioo maalum cha kupunguza mionzi ya screen, ama punguza screen contrast kidogo ya cp yako ama tumia LCD/ LED screens. Akifanya haya kidogo anaweza pata nafuu baadae
   
 7. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,167
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  Umejuaje km ni kipanda uso kabla ujaenda hospital?
   
 8. r

  raymg JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Use vasograin tabs....make sure umechunguza kwanza kama hana matatizo ya Pressure bcoz pia huumiza kichwa esp kama imepanda sana
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu Miwatamu pole kwa hayo matatizo ya shemeji yangu kuumwa na Kichwa Upande mmoja mimi nitachangia dawa yangu ya asili ni hii hapa :

  Grapes juice: Juice ya zabibu zilizoiva ndio dawa ya migrane, utumie kiwango kidogo cha juice hiyo atumia hadi atakapo ona kuwa amepata nafuu! Inshallah itamsaidia shemeji atumie kisha uje hapa unipe Feedback.

  [​IMG]

  Grape Juice Juisi ya Zabibu Dawa ya Ugonjwa wa Kipanda uso Migraine. Chanzo. MziziMkavu Mtafiti wa Dawa za Mitishamba.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280  • Severe migraines with visual disturbances, known as aura, are the second biggest risk factor
  • Only high blood pressure was a bigger factor
  • Findings come from 15 year study of 27,860 women
  [​IMG]

  Women who suffer from severe migraines accompanied by visual disturbances may be at an increased risk of

  heart attacks and stroke.
  Scientists have said only high blood pressure was a bigger indicator of a stroke or

  heart attack than migraines with aura, as the condition is known when accompanied by vision problems

  including flashing lights.
  The landmark 15-year study followed 27,860 women, of who 1,435 had migraine with aura.

  While previous studies have suggested migraine with aura is linked to a doubling of the risk of a stroke or heart attack, never before has it been named as the second biggest factor.

  Over the years there were 1,030 cases of heart attack, stroke or death from a cardiovascular ailment,

  according to the report from the American Academy of Neurology.


  Study author Dr Tobias Kurth said: 'After high blood pressure, migraine with aura was the second strongest single contributor to risk of heart attacks and strokes.

  'It came ahead of diabetes, current smoking, obesity, and family history of early heart disease.'


  Dr Kurth, of the Brigham and Women's Hospital in Boston and the French National Institute of Health, is also a fellow of the American Academy of Neurology.


  He said the risk for migraine-plagued women with aura was three times greater than for those with migraines that lacked this disturbance.


  A second study released by the same academy said women who had migraines with aura and took hormonal contraceptives were more likely to have blood clots.

  Both studies will be presented at the academy's annual meeting in March in San Diego, California.


  Source : http://www.dailymail.co.uk
   
 11. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2013
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa na tatizo hilo tangu 2003, kadiri siku zilivyokuwa zikienda mbele ndiyo tatizo lilikuwa likikuwa na kuwa hatari kwa afya yangu.
  Nimekuwa nikitumia sumatriptan 100 mg toka 2010, na Mwaka huu nimenadilishiwa dawa, dawa hizo ni jamii ya triptan, zinaitwa RIZACT-10. Nimetumia anti pain/pain killers Kama Panadol na Hedex mpaka nimechoka. Kuna Dr. Alinishauti nichome sidano za Botox kwani ndiyo treatments for chronic migraine, nilienda India, Apollo Hospital na kuchoma hizo sindano lakini hakuna nafuu yeyote toka nichome hizo botox mapema Mwaka huu. Nilienda India January 2013. Mpaka sasa bado natumia hizo RIZACT-10 lakini nafuu ni ya mda mchache tu.

  Wanajamvi naamini ninyi mnaweza kuwa msaada kwa huu ugonjwa wangu ulionisumbua kwa miaka 10 sasa. Kiswahili chake huitwa kipanda USO. Ki ukweli nimekuwa mimekuwa non productive kwa shughuli zangu za kila siku. Kila mda kichwa kinauma tena sana, wakati mwingine natapika sana mpaka nichome sindano za pain killer ndo napata nafuta. Yeyote anayejua dawa ya haya maumivu makali ya kichwa tafadhali nisaidieni tena kwa gharama yeyote kwani ninateseka sana. Tafadhali nisaidieni ndugu yenu ninsteseka mno na haya maumivu mskali ya kichwa.
   
 12. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2013
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,345
  Likes Received: 2,984
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mkuu.
  Ngoja Madokta waje lakini usikate tamaa
  ipo njia na tatizo litakwisha.
   
 13. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2013
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Hata mimi kilinisumbua sana lakni kimekwisha chenyewe! Ila nafikiri ni baada ya kuanzisha utaratibu wa kunywa sana Maji.
  Kabla ya hapo nikiona dalili fulani machoni najua ndiyo chenyewe nakunywa Panadol haraka kinakata, but dawa mpaka sasa sijajua.

  Kuna option nyingine nilikuwa natumia: Kutumia dawa za asili za Wamasai (zipo kwenye hali ya unga) ukinusa tu unapiga chafya na kinakata hapohapo. Kuna mtu aliniambia ukipiga chafya unastua mishipa ya kichwani na kuruhusu damu kutembea kwa urahisi (sina hakika sana na maelezo yake).

  Ngoja tusubiri wataalam
   
 14. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2013
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Adante ndugu yangu, kwakweli nahitaji msaada.
   
 15. tetere

  tetere JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2013
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 962
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ninawajua watu kadhaa waliowahi kupatwa na matatizo kama haya. nakiri kuwa wengi walitumia approach tofauti, ila wote (watu 6 wamepona).

  1. Tatizo la Allergy: rafiki yangu alikuwa na tatizo hili la migraine, baada ya kuwa ametumia dawa sana za maumivu akaja kugundua kuwa ilisababishwa na allergy. Akatibiwa na akapona.

  2. Mdogo wangu alikuwa na tatizo la kuumwa na kichwa sana. baada ya kula sana dawa za maumivu (yeye alishauriwa atumie steroids) lakini baadae hakupata nafuu. Alikwenda UK na wakagundua alikuwa na shida ya uvimbe kichwani, hii ilikuwa 1999. Akatibiwa kwa wiki 3, hajawahi tena kuumwa na kichwa.

  3.Jamaa yangu mwingine alikuwa na shida ya kuumwa na kichwa kisichosikia dawa, pamoja na maumivu ya kifua. Akatumia kila dawa lakini hakuwahi kupata nafuu. Lakini baadae alikuja kugundua alikuwa na rheumatic heart disease (a form of rheumatism).

  Uncle wangu (Civil engineer - mbishi!!!!!) alikuwa na maumivu ya kichwa kisichoisha. Yeye alikuwa UK, alitumia dawa zote lakini hakupata nafuu, baadae aliombewa kanisani, this is in 2007 na hakuwahi kuumwa tena na kichwa.


  Ndugu yangu nimeandika haya yoote nikiwa na lengo la kuonyesha kuwa wengi wamekuja gundua kuwa matatizo yao hayakuwa hicho walichofikiria mwanzoni. Na kama hutapata daktari akawa na muda na wewe (akakufanyia uchunguzi - a doctor who will explore all possibilities.

  Some of these problems has a very simple solution.
   
 16. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2013
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ubarikiwe kwa kunijuza hayo yote, naamini hata mimi ipo siku nitapona na kusahau.
   
 17. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2013
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wapi madaktari wa Jamii Forum?
   
 18. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2013
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,898
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  a
  hii inshangaza kidogo lakini ni kweli
  mwaka 1990 nilkuwa nasumbuliwa na kichwa cha ajabu sana !
  Nilkuwa siwezi kusoma kwa dk 30....akaja ndugu mmjoja akamwelekeza baba dawa! Baba alisita kwa sbb ya kidini lakini mama alimlainisha!
  Dawa yenyewe ni hivi.......!
  Aliambiwa akchimbe mzizi wa jeopatra au mbono kaburi atafuta mzizi uliolala...aukate ,then akanichanja kichwani kidogo na kunipaka utomvu wake .....afu akaurudisha ule mzizi pale alipoutoa na kuunganisha vile2 nakufukia!
  Masharti yake niliambiwa nisile kichwa cha mnyama yoyote
  tangu wakati ule sijawahi kusumbuliwa na hali hiyo tena
  hizi ndio dawa za kiafrika ni tukio ninalolitafakari mpaka leo!
  Je ni ushirikina au ni tiba ya kawaida !
  Ila yote tisa kumi nilipona na sikuona athari yoyote!
   
 19. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2013
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuna theories nyingi zinazoelezea pathophysiology(mechanism) ya jinsi tatizo hili linatokea,lakini hakuna hata moja iliyokubalika universally.Lakini pia hakuna dawa hata moja iliyothibitika kutibu/kumaliza tatizo hili universally.Ila kuna vitu kadhaa vinavyokubalika universally,juu ya ugongwa huu.

  1.Watalamu wote wanakubaliana kwamba hakuna uhakika wa nini hasa kinasababisha ugonjwa huu(kuna theory nyingi).

  2.Walamu wote wanakubaliana kwamba hakuna dawa ya uhakika inayotibu/inayomaliza tatizo hili kwa wagonjwa wote.

  3.Watalamu wote wanaclassify type 2 za migraine headache: Typical na Atypical-Typical migraine ina classical signs & symptoms("Zigzag silvery" vision dakika kadhaa kabla ya kichwa kuanza kuuma,Unilateral headache yaani kichwa kinauma upande mmoja wa uso,Kichefuchefu na mdomo kujaa mate au kutapika kabisa,photophobia yaani mgojwa hapendi kuona mwanga,kichwa kuuma kwa masaa hadi siku kadhaa kisha maumivu yanapotea kabisa) Kwa upande wa Atypical migraine,dalili hizo nilizotaja sio lazima zionekane zote kwa wakati mmoja.

  4.Watalamu wanakubaliana kuwa kichwa kikishaanza kuuma hakuna dawa yoyote ya kumeza ya maumivu inayofanya kazi vizuri.Hii ni kutokana na kwamba kunakuwa na slow down ya gut movement na decreased absorption tumboni(stomach & intestines).Dawa utameza lakini haitafanya kazi vizuri kama inavyotegemewa.

  5.Watalamu wanakubaliana kuwa kupona kwa maumivu hakutegemei dawa,kwa maana kwamba hata usipotumia dawa muda ukifika maumivu yanaondoka yenyewe.

  6.Kuna utafiti umeonesha kwamba kadiri umri unavyozidi kwenda,frequency ya attacks inapungua! Pia wengine wanasema hata intensity ya maumivu hupungua,ingawa hii haijakubalika sana.

  7.Hakuna data wala ushahidi unaoonesha kuwa migraine inaweza kupelekea mtu kupata uchizi,wala kifafa,wala kifo! Isipokuwa kuna taarifa za kuwepo idadi ndogo sana ya wagonjwa waliopata matatizo ya kuona ingawa bado haijathibitika kama ni kwa sababu ya migraine.

  8.Pia takwimu zinaonesha kuwa,ungonjwa huu unaanza kuonekana baada ya kipindi cha utoto kupita.Mara nyingi watu huanza kuupata ukubwani,na inaonekana wanawake wanaathirika kwa wingi kuliko wanaume kiuwiano.

  9.Pamoja na kwamba ugonjwa huu unaanza kuonekana zaidi ukubwani,lakini watalamu wanasema huu ni ugonjwa wa kurithi.Kwa hiyo ndugu yangu kama ndio hivyo,inawezekana tatizo hili lipo kwenye familia yenu! Mimi kwetu upo!

  10.Watalamu pia wanasema kwa kuwa hakuna uhakika hasa ni nini sababu ya tatizo hili,wanasema,upo uwezekano wa tatizo hili kupotea bila tiba yoyote ya maana.Hapa ndipo kidogo kuna ukakasi,maana wapo watu wameombewa wakapona,wapo waliotumia dawa za wamasai wakapona nk.,nk,nk. sasa huko siwezi kwenda zaidi!

  Kwa nini nimetoa mchango wangu hapa? Mimi pia ni mhanga wa tatizo hili tangu nikiwa na umri wa miaka 14.Binafsi mimi ni mwanachuo ktk chuo kikuu fulani cha udaktari hapa nchini.Na kiukweli,kwa jinsi ugonjwa huu ulivyonitesa,naweza kusema,ndicho kichocheo kikubwa kilichonifanya nisome kozi hii.

  Kwa sasa frequency imepungua sana;mwanzo nilikuwa napata attacks hata mara mbili hadi tatu kwa wiki,ila siku hizi ninaweza kukaa hadi miezi minne sijapata attack kabisa.Hata intensity nahisi imepungua tofauti na mwanzo;ingawa inawezekana labda ni kwa sababu nimeishazoea.Usually mimi maumivu huwa masaa 2-3 baada ya hapo nakuwa mzima kabisa na ninaendelea na shuguli zangu as usual.

  But all in all maumivu ni makali jamani,asikwambie mtu.Every shughuli is shut down;huwezi kufanya chochote.

  Nise tu pole kwenu ndugu yangu,maana na mimi naufahamu muziki huo!
   
 20. makavulaivu

  makavulaivu JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2013
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakushauri ukafanye kipimo cha CT Scan , kabla ya kufata shauri nyingi zitakuchanganya
   
Loading...