KIOO CHA MAAJABU...MAGIC MIRROR by SAMM

KIOO CHA MAAJABU...MAGIC MIRROR by SAMM

Parata

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
3,090
Reaction score
693
Kwa ufupi...
Kutoa ahadi ni rahisi lakini kutimiza
ahadi ndio tatizo! Nice, binti mrembo
mtoto kigogo wa benki kuu tawi la
Mwanza, anampa ahadi mpenziwe
Robert ya kuwa atampenda milele,
haijalishi ni katika mazingira gani.
Robert anatoka katika familia ya
maisha ya kati na analelewa na baba
yake mdogo baada ya baba yake
mzazi kufariki. Lakini ahadi ya Nice
inaingia dosari baada ya uhusiano
wao kupata upinzani mkali toka kwa
wazazi wa pande zote mbili...
SEHEMU YA KWANZA:
"happy birthday to you, happy
birthday to you, happy birthday,
happy birthday, happy birthday to
you." sauti za furaha zilikuwa
zikiimba na kufuatiwa na vigelegele,
nderemo na vifijo kumpongeza binti
mwenye sifa zote za kumfanya
mwanaume amgeukie mara mbili
mbili, Nice Mbawala! Kila mtu ama
alimpa mkono, alimkumbatia ama
alimbusu shavuni kuonesha
kumpongeza! Kila mtu alionesha
furaha!
Katika kona moja alisimama kijana
alievalia nadhifu, suruali nyeusi,
shati la pinki na tai nyeusi ya
kipepeo, mkononi alikuwa na glasi ya
wine, usoni hakuonesha kuwa na
raha!
Wakati ukumbi unalipuka kwa vifijo,
yeye alikuwa kimya kabisa kasimama
tuli! Akaitua glasi iliyokuwa na nusu
mvinyo na kutoka nje ya ukumbi huo,
akaelekea katika bustani na kuketi juu
ya bembea akionekana mwingi wa
mawazo!
Baada ya muda Nice alitokea mlango
na kuangaza nje, alipomuona kijana
yule akaelekea alipo, "mbona
umekimbia sherehe yangu jamani?"
akalala akiketi katika bembea
pembeni yake. Kijana akatoa
tabasamu hafifu bila kujibu kitu. Nice
akamtazama na kumuonea huruma,
akapeleka mkono na kumshika bega,
"Robert usiwaze sana, ni mipango ya
Mungu, sote tunapita!"
Robert au Roby kama Nice mwenyewe
alivyopenda kumwita, alijikuta chozi
likimdondoka! Hakuwa hata na zaidi
ya miezi tangu amzike baba yake
mpendwa! Machungu bado yalikuwa
moyoni mwake! Nice akainuka na
kumkumbatia rafiki yake huyo, akalia
nae!
***
Kipindi hiki cha likizo kiliwakutanisha
mara kwa mara Nice na Roby, kwa
kuwa walikuwa majirani, mara nyingi
Roby alienda kwao Nice wakaketi
kibarazani na kuongea mambo ya
shule, kwa kuwa wote walikuwa
wanasoma mchepuo mmoja, walikuwa
na mengi ya kuongea. Jioni hii Nice
alikuwa akimsindikiza Roby, walikuwa
wakitembea taratibu huku wakiongea,
mara Nice akamshika mkono Roby
ambae mwili ulimsisimka si kidogo,
walienda mbele kidogo na mara Nice
akageuka na kumkumbatia, busu
murua mdomoni na kumwachia mara!
Roby alibaki na mchecheto alitamani
liendelee, akapeleka mkono mdomoni
huku Nice akitabasamu, kisha
akageuza kurudi kwao! Roby
alisimama pale kwa muda asijielewe
elewe! Badala ya kwenda nyumbani
akaelekea kwa rafiki yake Zuberi,
"hey, mbona leo una furaha sana!"
kilikuwa kitu cha kwanza kwa Zuberi
kusema baada ya Roby kuingia akiwa
ana uso wa furaha! Roby hakujibu
kitu zaidi ya kujirusha kitandani!
Zuberi akacheka na kutania, "au
umeonana na Sigfrida, ha ha haaa!"
akatia utani kidogo! Roby akacheka,
Sigfrida alikuwa girlfriend wa Roby
wakiwa sekondari Mwenge!
"umenikumbusha mbali sana! Kuna
kitu kingine mshkaji wangu!"
Zuberi akaketi kwenye pembe ya
kitanda na kumsikiliza Roby, "Nice
kani kiss!" Roby akasema kwa furaha
huku akiigiza jinsi Nice alivyomkiss!
Zuberi akabaki na mshangao, "acha
bwana! Serious?!"
"yeah, serious like Hell!"
Zuberi akacheka kwa furaha na
kuuliza, "mmeanza lini tena?"
Roby akainuka pale kitandani na
kujaribia tena jinsi Nice alivyombusu!
***
Baada ya mlo wa usiku, Roby
alijifungia chumbani kwake
akiitazama na kuishika simu akiwaza
ampigie Nice ama vipi? Hakuwa
akijiamini kama kweli Nice amefanya
vile kwa kuwa anampenda kimapenzi
au kama rafiki tu? Au kutokana na
matatizo yaliyompata, anajaribu kuwa
karibu nae kumfariji? Hakuwa na
uhakika! Nice alikuwa mzuri wa sura,
umbo na tabia pia! Vijana wengi
shuleni kwao walimpenda, hata
walimu pia wapo waliojaribu
kumrubuni wampate, lakini hakuna
aliefanikiwa! Ucheshi wa Nice
uligeuka shubiri kwa yeyote
aliemtongoza! Wakati anafikiri hayo,
simu yake ikaita, akakurupuka,
alikuwa Nice.....
 
SEHEMU YA PILI
Akaipokea simu kwa furaha sana!
Aliweza kuhisi kuwa hata upande wa
pili Nice atakuwa anacheka ama
kutabasamu! Waliongea na kutaniana
hili na lile huku Roby akitamani
aeleze hisia zake ambazo hakujua
zitapokelewaje! Ambacho hakukitaka
ni urafiki wao kwisha ama kufifia!
Tangu ahamie Mwanza alipoendelea
na kidato cha tano, mtu ambae
alikuwa karibu yake sana ukiacha
Zuberi alikuwa Nice!
"ile song uliyokuwa unaandika
inaitwaje?"
Roby akakumbuka wakati ameketi
eneo moja shuleni kwao, Mwanza Sec,
linaitwa Onyango, akiwa bize
anatunga nyimbo, mara Nice akatokea
nyuma yake!
"aah, inaitwa 'kama ni siri'"
"kama ni siri?"
"yap."
"inamuhusu nani?"
akatabasamu kabla ya kujibu,
"haimuhusu mtu, ni utunzi tu!"
"mmmh, nambie ukweli bwana, au
umemwandikia Sig?" wote wakacheka!
"hapana!"
"uliwezaje kumwacha binti mzuri
vile?"
"mzuri ee?"
"ndio, picha zake zinaonesha tu!"
Roby akashusha pumzi na kujaribu
kubadilisha topic,
"hivi sa ivi ni saa ngapi?"
Nice akacheka na kuamua kulipotezea
suala la Sig! Moyoni alimuonea wivu!
"sa sita kasoro, unataka ulale?"
"eer hapana, nilitaka kujua tu!"
"umeangalia tamthiliya ya 'La Mujer
De Mi Vida?"
"hapana, ilikuwaje leo?"
"unavyopenda kusimuliwa wewe?!
Haya Kike anamtaka Alejandro amuoe
Barbarita!"
"wacha wee, enhe?!"
"itaendelea kesho!"
"mmh, haya bwana!"
baada ya maongezi marefu
walitakiana usiku mwema.
***
Kesho yake asubuhi mida ya saa nne,
Rehema rafikiye Nice akaja. Wakaketi
kibarazani na kupiga soga. Kubwa
lilikuwa juu ya Roby! Nice alimweleza
Rehema jinsi anavyojisikia juu ya
Roby, lakini hakuwa na uhakika kama
Roby anajisikia kama yeye juu yake!
"u cant imagine, jana nime mkiss na
hakufanya lolote! Hata kunishika tu,
nikaona aibu mtoto wa kike na
kuondoka!"
"mmh, mi najua anakupenda, jinsi
anavyokuangalia, kutabasamu nini,
hamku chat usiku?"
"yaani Rey nimekaa na simu kuanzia
saa mbili hadi saa nne, hakuna text
wala missed call!"
"so ukalala?"
"ntaanzaje? Nikampigia nisikie hata
sauti yake tu!"
"ulimuuliza kuhusu ule wimbo
uliomfuma anaandika kule Onyango?"
"kanambia haumhusu mtu eti!"
"chunga shosti, kuna namba inatishia
pale darasani, unaona anavyo
mfanyiaga makusudi?"
"nakwambia silipendi lile toto,
linanikeraje? Kujipendekeza tu!"
wakati wanaendekea na maongezi,
geti likafunguliwa na Roby kuingia,
mapigo ya moyo ya Nice yakapanda
ghafla!
"mmenyoosha miguu wenyewe hamna
hata haraka wakati bado nusu saa tu
kipindi kianze"
"karibu uketi kwanza, hapa na Pamba
Sec sio mbali,"
"mmh, haya, mmeamka poa lakini?"
"shwari, za kwako?"
"poa tu!"
Nice akaingia ndani kujiandaa na
kumwacha Rey na Roby kibarazani.
"nasikia unaandika mashairi mazuri
Roby!"
"kawaida tu Rey" akajibu akitabasamu
"ulimwandikia nani?"
"just for fun"
"niimbie basi kidogo"
akacheka, "ushawahi kunisiki
naimba?"
"sijawahi ndio nataka nikusikie leo!"
Roby akatabasamu na kujibu, "sijui
kuimba jamani, sauti yangu mbayaa!"
"nani kakwambia hujui wakati
hutakagi kuimba mbele za watu, au
unamwimbiaga Nice?"
"nope! Sijawahi kumwimbia mtu!
Huwa najirekodi tu kwenye simu na
kujisikia...!"
mara Nice akatokea, "twendeni
jamani, muda umetuishia!"
"umependeza shosti!" Rey akasema
mara tu alipo mgeukia, Roby
hakusema kitu, alitamani angesema
yeye! Hilo lilimnyong'onyeza Nice!
Walitembea kwa miguu kuelekea
tuition shuleni Pamba, waliongea na
kucheka, mara kwa mara Nice
alimgusa 'bahati mbaya' Roby ambae
ni kama 'hakushtukia' vitendao vile!
Wakati wanaingia geti la shule, bahati
mbaya binti mmoja akamrushia vumbi
Roby wakati akitaniana na mwenzake,
akaja hima aliposimama, "jamani am
so sorry,!" akaomba msamaha na
kutoa kitambaa chake, hima akainama
na kuanza kukifuta kiatu cha Roby
kilichokuwa kimeng'aa kiwi awali,
"its ok, achana nacho!" akamwinua,
"am sorry Roby, sikukuona...!"
"ok ok, poa usijali!" akaendelea mpaka
walipo kina Nice na Rey waliokuwa
wamenuna,
"mi ananikeraga yule!"
"kamchafua makusudi, anajidai bahati
mbaya!"
"its ok jamani, achaneni na hiyo
issue!" akawapoza. Yule binti
aliemchafua Roby alikuwa bado
kasimama anamwangalia, Nice
akaamua kukata mzizi wa fitna,
akamshika mkono Roby wakiondoka!
Ilikuwa kusudi na ni huyo binti
waliekuwa wanamwongea na Rey
kibarazani kwao Nice! Wivu!
***
BAADA YA LIKIZO:
Ilikuwa jumamosi moja tulivu, jijini
Mwanza kulikuwa na shamrashamra
za tamasha la Fiesta, moja ya
matamasha makubwa ya muziki
nchini. Wapenda muziki wote
walikuwa wakimiminika katika viwanja
vya CCM KIRUMBA, miongoni mwao,
walikuwemo Nice, Roby, Rey na
Zuberi! Urafiki wa Nice na Roby
ulijulikana kwa kila mtu mtaani kwao,
kwa marafiki na hata shuleni ambako
Nice alikuwa na upinzani toka kwa
Leila, mtoto mzuri wa uswahilini
ambae alipania kumnyang'anya Nice
Roby! Ilimbidi Nice kumganda Roby
kama luba!
Leo ilikuwa fursa kubwa kwao, mzee
Mbawala na mkewe walikuwa safari,
babake mdogo na Roby alikuwa safari
pia! Ndio muda pekee waliopata wa
kujirusha! Wakiwa na usafiri wa Nice,
walienda kirumba na kujinafasi, lakini
moyoni Nice alikuwa na jambo
kalipanga, ambalo alikuwa
amemshirikisa Rey, alilipanga siku
mbili kabla na kuhakikisha linaenda
sawa! Shoo ilikuwa nzuri sana na
wasanii walijitahidi kulipamba jukwaa
barabara! Baada ya show kwisha
majira ya saa moja usiku, safari ya
kurudi ikaanza, kwanza akapelekwa
Zuberi, kisha Rey. Kutoka hapo Nice
aliendesha hadi La Kairo Hotel! Roby
alijua labda kuna kitu wanafata then
wanageuza, cha ajabu haikuwa hivyo!
Wakaketi na Nice kuagiza wine, wakati
wanaendelea kunywa ndivyo Nice
alivyozidi kumfanyia vituko Roby,
akionesha kulewa..
 
******mwisho wa simulizi********
 
Back
Top Bottom