Kiongozi wa Uamsho mahututi Zanzibar

Kiongozi wa Uamsho mahututi Zanzibar

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Zanzibar. Kiongozi mwandamizi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu,Sheikh Khalid Azzan Hamdan amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja akiwa chini ya ulinzi wa askari Magereza na polisi kuanzia Septemba Mosi mjini hapa imefahamika.

Akizungumza na Mwananchi Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar (Magereza), Khalifa Hassan alisema Azzan aliwahi kuishiwa nguvu za miguu mara mbili akiwa katika mahabusu ya Gereza la Kinuai,Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja.

Hassan alisema,kufuatia hali hiyo, magereza waliamua kumpelekea katika hospitali hiyo ya Mnazi Mmoja na kuamriwa alazwe kwa uchunguzi zaidi na matibabu kufuatia afya yake kuzorota ghafla.

Alisema, watuhumiwa wengine wanaokabiliwa na kesi ya uharibifu wa mali na kuhatarisha usalama wa Taifa mbali na Azzan, wanaendelea vizuri na wako katika afya njema ambapo jana walifikishwa mahakamani bila ya mshtakiwa mwenzao huyo kuwapo.

Wakili wa washtakiwa hao, Abdallah Juma alisema baada ya kupokea taarifa za mteja wake kuwa mgonjwa, aliamua kumjulia hali akiwa hospitali, lakini askari walioimarisha ulinzi katika chumba cha wagonjwa wa mahabusu na wafungwa walisema hawawezi kumruhusu bila ya kupewa kibali cha uongozi wa magereza Zanzibar.

Hata hivyo, Wakili Abdallah alisema, mteja wake Azzan anasumbuliwa na matatizo katika kibofu cha mkojo kutokana na kuwa na vijiwe ambapo alitakiwa kutibiwa nchini India na Afrika Kusini.

Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja,Omar Abadllah Ali alisema kwamba tayari daktari anayemshughulikia ameshachukua vipimo muhimu na anaendelea kufanya vipimo maalumu kwa kutumia mashine ya picha.

Hata hivyo alisema ni mapema kuyazungumzia maradhi yanayomsumbua mtuhumiwa huyo, lakini alikiri na kusema amelezwa katika chumba maalumu hospitalini hapo.

Chanzo: Mwananchi
 
pole zake, inshaallah atapata afuani ...
 
Ajiamshe sasa,sianacheza na dola!.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mungu ajalie upendo utawale madaktari wafanye kazi yao bila kuingiliwa hata ikilazimu africa kusin au india aandikiwe kwenda afya yake itibiwe kwa umuhimu wake
 
Kwa kila alokuwa na Magonjwa Tunamuombea kwa Moula Karim Amponyeshe. AMIN
kwa kila mwenye MARADHI sugu Tunamuombea kwa MwenyEzzi Mungu Al-Shaafi Amuondolee Maradhi. AMIN
Kwa kila Mwenye Maumivu au dhikii, au huzuni tunamuombea kwa Allah Ampe takhfifu. AMIN
kwa kila mwenye Shida au Umasikini au Mahbusu(kwa dhulmaa)Tunawaombea kwa Subu-Hana-Wataala Awape Ahweni na Faraja. AMIN na kwa Shk. Khalid Azzan Hamdan Muumba mwenyEzzi Mungu Amrejeshe AFYA na uzima. AMIN
WaSallaLahu Aleiyhi WaSalaam.
 
Amiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiin!
 
Wawasamehe tu huo uamsho...
Wamekaaa jela sana.
 
Ajiamshe sasa,sianacheza na dola!.
Ajiamshe sasa,sianacheza na dola!.
Ndugu Yangu Abi. Umzima wa hali? Hakuna mtu anajitamania Magonjwa/Maradhi/Umasikini hayo ni matakwa ya Muumba(Allah) humkumbuka mjaawake !! Magonjwa sii aibu au kashfaa au fedheha. Haya ni ya "kilimwengu" yanaweza kumkumba mtu yoyote. Nasikitika kuona upeo wako mduchu na akili ulizopewa unazitumia bila mwelekeo maalum " " PoorMan
siwezi kukutukana ila Ujue Mimi, wewe, yule,wale na wenye nguvu, Dola na viumbe vyote siku ikifika hakuna wa kukufaa..............!
tutachimbiwa shimo na kulazwa kuudongo na tuwe chakula cha funza na wadudu.!!! Omba salaama au poa kimya.

alipokuwa akihatarisha amani ya nchi hakujua hayo yote uyasemayo mkuu?
 
Ajiamshe sasa,sianacheza na dola!.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

2acha udini huo na nadhani ukatoliki. Hivi lwakatare hakuichezea dola? yupo wapi sasa hivi? si anapata matibbu nje na wote kesi zao ziko mahakamani.
 
Ajiamshe sasa,sianacheza na dola!.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Ni kweli ameweza kuwaaamsha wazanzibari wengi sana. akina mansour, Hassan Moyo n.k oLE WENU WATANGANYIKA zANZIBAR IMESHAKATAA KUATAWALIWA NA NYINYI FAIDA ZA UAMSHO
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom