Kiongozi wa mbio za mwenge ana nafasi gani kikatiba?

Sabayi

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
2,310
991
Nimekuwa nikiona kiongozi wa mbio za mwenge akitoa amri na maagizo mbali mbali kwa baadhi ya viongozi katika maeneo anayokimbiza Mwenge,Naomba kuelimishwa huyu kiongozi wa Mbio za Mwenge ana nafasi gani katika katiba yetu? Je wanaopewa hizo amri na maagizo wakikataa kutii wanaweza kuwajibishwa?
 
kimsingi mwenge wa uhuru unakimbizwa na mh rais wa jamhuri ya muungano, mkimbiza mwenge anafanya kazi kwa niaba yake. taarifa zote za mikoa na wilaya zinasomwa kwa mh rais. ni kwa mantiki hiyo kuwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa anayo mandate ya kutoa maelekezo!
 
Mimi huo mwenge naona ni ushirikina na mradi wa kuwadhulumu wananchi pesa kwa michango ya kulazimishwa. Usije kushangaa huyo kiongozi akaukwaa uDC mwakani
 
Back
Top Bottom