SoC01 Kiongozi ni vema kuchunga Ulimi wake

Stories of Change - 2021 Competition

Noel Shao

Member
Jan 19, 2017
89
185
Utimamu wa kiongozi bora ni kuwa na kichwa chenye ubongo wa hekima, unaowaza, unoainisha, unaochambua, na kuweza kufanya tathimini. Vile vile ukamilifu wa kiongozi ni awe na kinywa chenye ulimi wa ufasaha, unaonena maneno ya staha, unaosema maneno ya uhakika, weledi na wenye kutoa nasaha bora.

Aghalabu vitu hivyo vikichagizwa na kifua kilicho na moyo wa wema, utu na busara, pasipo na shaka haki, umoja, upendo, amani vitatamalaki katika taifa.

Natanguliza haya ili kutoa rai kwa viongozi walio na nyazifa mbalimbali kutathimini lugha zinazotoka katika ndimi zao wawapo katika kutimiza wajibu na majukumu ya kila siku kwenye nafasi wanazo hudumu.

Kiongozi ni kiungo
Kiongozi ni mtu anayepaswa kuwa kiungo cha kuwaunganisha watu wa rika zote, katika umoja, urafiki, utu, upendo bila kujali itikadi ya vyama vya siasa, ukabila, tofauti ya uchumi, jinsia, na ukanda. Kwa hatua hii ndipo utulivu, na amani hujengwa na watu kuwa na wasaa wa kujikita katika shughuli za kujiletea maendeleo.

Kiongozi mwenye ulimi wa kusema lugha zinazo kusudia kuleta chuki, dhihaka, uadui, uchonganishi, uchochezi, uhasama wa kisiasa, kidini, kiuchumi, au kikabila ni kiongozi asiye tambua nafasi yake katika jamii anayepaswa kushauriwa namna ya kuutumia ulimi vema na si kazi jepesi kwa namna viongozi hasa walio hudumu katika nafasi za juu wanavyo pata ulinzi wa kikatiba .

Hazina bora na tunu ya Tanzania ni amani, hiki ndicho kilicho bora kuliko uchumi, na siasa zetu. Mengine yote yanabaki kama ziada ya haya.

Nazungumzia viongozi kwa kuwa ndio wenye wajibu wa mambo mengi nchini. Lugha za kutugawa hatutegemei zitolewe na kiongozi mwenye amana ya kuongoza umma. Maneno ya dhihaka, chuki au yasiyo tangaza umoja wetu tulioridhi yataligawa taifa vipande vipande.

Urithi wetu
Tangu enzi za muasisi wa taifa, Hayati Julius Nyerere aliweka juhudi za dhati kuhakikisha umoja wa kitaifa unakuwepo, ndio urithi wa kukumbukwa. Ikatokea siku ama kwa sababu yoyote kushindwa kuilinda na kuitunza amani tuliyo nayo basi hakika historia ya taifa hili itapotea.

Historia ni mwalimu mzuri wa kurejelea, mataifa mengi yaliyo chezea amani, yalijikuta yakiingia katika machafuko, ambayo hayakuwa suluhu ya matatizo yao bali yalivimbisha mioyo ya raia chuki na uhasama.

Hivyo, vipawa na karama za uongozi walizo pewa viongozi hawana budi kuvitawala kwa ufasaha, busara, utashi, hekima na weledi mkubwa. Wajikite kuheshimu utumishi kwa umma, utawala wa sheria na utawala bora.

Ubabe na matendo mabaya yapingwe, kwani kutoyakemea na kuyaacha yataja sababisha taharuki. Lazima viongozi wakumbushwe mipaka yao, wale wanaowazunguka viongozi wawe ndio msaada wa kutoa ushauri.

Tusibebe dhana kuwa siasa ni uadui. Kutofautiana kifikira, kimawazo ni sehemu ya demokrasia, na kutofautiana huko kusisababishe wengine wabebeshe gharama za demokrasia.

Wito wangu
Wito wangu ni viongozi kutambua wajibu wa kulinda amani, uhai na umoja wa taifa. Wakubali ushauri, na kukosolewa kwa lengo la kuboresha. Adui mkubwa wa amani ni pale tunapo ona viongozi hawatendi sawa na kuchagua kukaa kimya”

Nimeandika haya kwa kutopendezwa na kauli za viongozi wa taifa hili kwani iliwahi tokea huko nyumba Rais mmoja aliwaita wapinzani kuwa ni Wapumbavu na Malofa. Kamusi sanifu inatoa tasfiri kuwa mpumbavu ni sawa na juha, fala, mbumbu, na bwege. Huku neno “Lofa” Likiwa na maana ya mtu anaye zururazurura asiye na kitu wala kazi”.
Kiongozi mwingine aliwahi wadhihaki wananchi kuwa yeye ndiye kiongozi anayekula raha kuliko viongozi wote.

Na hivi karibuni wakati watanzania wengi wakilia juu ya makali ya tozo mpya za miamala ya simu, alinukuliwa waziri wa uchumi akisema wale wanaohoji kuhusu makato kuwa makubwa basi wahamie Burundi kwenye unafuu.

Kauli kama hii si ya kutia faraja, au kuleta suluhu bali kusiliba chumvi kwenye kidonda na haipaswi kutolewa na kiongozi wa umma tena waziri. Nachelea kusema ni dhihaka kwa umma ambalo wana haki ya kutoa maoni yao kwa viongozi walio wachagua tena kwenye mambo yanayo wahusu wao moja kwa moja kwa sababu ukweli ni kuwa tozo mpya za miamala ni mzigo wa msumari kwenye vichwa vyenye upara vya wananchi.

Kadhalika, kabla ya kumaliza siwezi acha kugusia tabia ya viongozi wa hasa wa jeshi la polisi jinsi wanavyo dili na viongozi wa vyama vingine vya upinzani kwa kauli za kutisha, kuwabakizia kesi nk.

Tuhuma za ugaidi dhidi ya Mbowe
Binafsi sijapendezwa na ukamatwaji wa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe na viongozi wengi huku Mbowe akipewa kesi ya ugaidi, na kupanga njama za mauaji. Hii ni habari mbaya kwenye jicho la kidiplomasia na katika uongozi wa Rais SSH.

Aidha, wajibu ulio mbele ya viongozi ni kujenga utaifa, na kudumisha umoja. Ndimi za viongozi ziwe chemchem ya maneno yenye hekima na busara, ndani ya vifua vya viongozi ikae mioyo ya kupenda haki na amani, isiwe mioyo ya chuki, uadui, uhasama, na kuminya haki za wengine, mambo hayo hayajawahi kuwa chachu ya amani bali mbegu ya uharibifu.
 
Kauli mbovu unaziona tu Chama tawala ila vyama vya upinzani hauzioni?

Umeumia kuhusu Mbowe kukamatwa ila akina mude walipokuwa wanaropoka ulifurahi!?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Two wrong doesn't make one wrong right.. na Kuhusu Mbowe unaweza weka unazi ndani yke ila mazingira ya kisiasa kwa sasa na tulipo toka, tulihitaji relief than any thing else.
 
Nilivyosoma na kuelewa nimeona kuwa kesi ya mbowe siyo ya juzi bali ni ya tangu mwaka jana hata kabla ya uchaguzi. Alipogundua kuwa alikuwa anatafutwa kwa kesi hiyo, mara tu baada ya uchaguzi akakimbilia Dubai hadi pale Magufuli alipofariki akiamini kesi nayo itakuwa imekufa na Magufuli ndipo akarudi Tanzania.
 
Two wrong doesn't make one wrong right.. na Kuhusu Mbowe unaweza weka unazi ndani yke ila mazingira ya kisiasa kwa sasa na tulipo toka, tulihitaji relief than any thing else.
Relief kwa kuwaacha CDM waendelee kujiropokea wanavyotaka..au waibadilishe nchi wanavyotaka na kumpangia Rais ratiba!

Wewe ni mnafiki. .
Jitahidi kutoa boriti lako kabla hujatoa banzi jichoni kwa mwenzio.

Huyu Rais ni wa wananchi wote ,siyo wa CDM pekee.

Na sheria itaendelea kufwata mkondo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pam
Nilivyosoma na kuelewa nimeona kuwa kesi ya mbowe siyo ya juzi bali ni ya tangu mwaka jana hata kabla ya uchaguzi. Alipogundua kuwa alikuwa anatafutwa kwa kesi hiyo, mara tu baada ya uchaguzi akakimbilia Dubai hadi pale Magufuli alipofariki akiamini kesi nayo itakuwa imekufa na Magufuli ndipo akarudi Tanzania.
Pamoja na hayo! Umesoma charge sheet yake?
 
Wito wangu ni viongozi kutambua wajibu wa kulinda amani, uhai na umoja wa taifa. Wakubali ushauri, na kukosolewa kwa lengo la kuboresha. Adui mkubwa wa amani ni pale tunapo ona viongozi hawatendi sawa na kuchagua kukaa kimya”
Thank you much.. your vote please
 
Pam

Pamoja na hayo! Umesoma charge sheet yake?
Hapana, ila nimesoma summary iliyotolewa na vyombo vya habari tu. Hata hivyo jambo ninaloongelea ni kwamba "hakubambikizwa"kesi na SSH, bali ni kesi ya tangu mwaka jana.
 
Hapana, ila nimesoma summary iliyotolewa na vyombo vya habari tu. Hata hivyo jambo ninaloongelea ni kwamba "hakubambikizwa"kesi na SSH, bali ni kesi ya tangu mwaka jana.
Taarifa y awali y jeshi la polis ilikuwa mbowe anashtakiwa kwa ugaid na tuhuma za kutaka, kuua viongozi, ila charge sheet ikaeleza kuwa alikuwa anataka kuchoma vituo vya mafuta! Huoni hii tofaut inatia doa mamlaka?
 
Taarifa y awali y jeshi la polis ilikuwa mbowe anashtakiwa kwa ugaid na tuhuma za kutaka, kuua viongozi, ila charge sheet ikaeleza kuwa alikuwa anataka kuchoma vituo vya mafuta! Huoni hii tofaut inatia doa mamlaka?
Kuchoma vituo vya mafuta ni ugaidi kama ambavyo kuanguasha WTC ilivyokuwa ugaidi. Sioni kilichobadilika katika lugha hiyo zaidi ya kuongeza specificity.
 
Back
Top Bottom