Rais, Kiongozi anayepotezwa na vijana wake

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,177
Reaction score
2,816
Uongozi ni mgumu sana na kamwe hakuna kiongozi anayepatia kuongoza kwa asilimia mia moja

Kinachofanya uongozi kuwa mgumu ni kuruhusu washauri wengi walioko nje ya mfumo rasmi wa ushauri

Kiongozi anaporuhusu watu wa nje kuwa washauri wakuu ni rahisi sana kutoka kwenye dira na mwelekeo kwasababu hawa walio rasmi wataamua kukaa pembeni na kumuacha afanye anavyoona yeye.

Mama kizimkazi alianza vizuri sana na kwa asilimia kubwa watanzania walijaa matumaini. Lakini yanayotokea sasa watu wanaanza kushangaa

Vifo vya uzembe kwenye vituo vya afya vinazidi kuongezeka maana wahudumu hawanahofu wala wasiwasi kwasababu hawana wa kuwawajibisha wanapokosea

Miradi ya maendeleo hayaendi mbele, maadili ya Kitaifa yanazidi kuporomoka, wageni wanazidi kujipenyeza kwenye kila sekta na ajenda zao.

Teuzi kila siku na wanaoteuliwa ni majina yale yale na hakuna jipya wanaleta.

Huku kunaitwa kuvurugwa; yaani hujui uchukue lipi uache lipi, huku kelele kule kelele na zote unaona zinatakusaidia kwasababu zinatoka kwa watu unaowaamini na unadhani wanakusaidia kumbe wanakupoteza

Hii inaonyesha namna gani viongozi hawana mpango kazi au hawaamini mpango kazi ulioko ofisini ulioandaliwa na wataalamu. Wanaamini zaidi watu wa pembeni
 
Teuzi Kila siku, watu walewale matokeo ZERO.

AMA KWELI, HERI NGUO KURARUKA LAKINI SIO AKILI KWAKUA UTAJIRI WA MASIKINI NI UJINGA WAKE WENYEWE.

Kwann watu wajinga na wasokua na Uwezo, wanakawaida ya kutafuta madaraka Kwa nguvu, Si aache tu alipwe pensheni ?.
 
Uongozi ni mgumu sana na kamwe hakuna kiongozi anayepatia kuongoza kwa asilimia mia moja

Kinachofanya uongozi kuwa mgumu ni kuruhusu washauri wengi walioko nje ya mfumo rasmi wa ushauri

Kiongozi anaporuhusu watu wa nje kuwa washauri wakuu ni rahisi sana kutoka kwenye dira na mwelekeo kwasababu hawa walio rasmi wataamua kukaa pembeni na kumuacha afanye anavyoona yeye.

Mama kizimkazi alianza vizuri sana na kwa asilimia kubwa watanzania walijaa matumaini. Lakini yanayotokea sasa watu wanaanza kushangaa

Vifo vya uzembe kwenye vituo vya afya vinazidi kuongezeka maana wahudumu hawanahofu wala wasiwasi kwasababu hawana wa kuwawajibisha wanapokosea

Miradi ya maendeleo hayaendi mbele, maadili ya Kitaifa yanazidi kuporomoka, wageni wanazidi kujipenyeza kwenye kila sekta na ajenda zao.

Teuzi kila siku na wanaoteuliwa ni majina yale yale na hakuna jipya wanaleta.

Huku kunaitwa kuvurugwa; yaani hujui uchukue lipi uache lipi, huku kelele kule kelele na zote unaona zinatakusaidia kwasababu zinatoka kwa watu unaowaamini na unadhani wanakusaidia kumbe wanakupoteza

Hii inaonyesha namna gani viongozi hawana mpango kazi au hawaamini mpango kazi ulioko ofisini ulioandaliwa na wataalamu. Wanaamini zaidi watu wa pembeni
Mambo yao tuwachie wenyewe
 
hii tengua teuwa ni sehemu ya kushindwa pia.Rais hajui nani akae wapi na afanye nini mwisho wa siku anabeti.
 
Back
Top Bottom