MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,294
- 39,977
"Mimi nimetokea familia maskini", "Mimi nimelala kwenye ngozi ya ng'ombe badala ya godoro".... "Mimi sina biashara yoyote na kiasi nilicho nacho benki hakizidi hata Tsh 20m".... viongozi wenye kauli za aina hii HATUWATAKI. Hakuna ufahari wowote kwenye umaskini. UMASKINI NI LAANA.
Ninaandika huu uzi nikiwa nimekasirika hatari. Kwa muda mrefu nimesikia viongozi kibao wakiunadi umaskini pale wanapotafuta uungwaji mkono na wananchi (wapiga kura). Utakuta kiongozi nyakati za kampeni ataanza kuendesha baiskeli na kupanda daladala kuonyesha naye ni maskini kama wapiga kura walio wengi ili aungwe mkono. Kwenye chama chetu pendwa kuna viongozi wengi wenye hizi pigo za kiwaki.
Watanzania kwa sasa wanataka kiongozi atakayewaongoza watanzania kuuchukia umaskini na kujiondoa huko. Hatutaki kiongozi wa kutufariji tuendelee kuuona umaskini kama jambo la kawaida. Kama kiongozi analipwa mamilioni kwa mwezi na anakopesheka hadi 500m kuna haja gani ya yeye kufanya maigizo ya kuonyesha kuwa bado kapigika?
WanaJF niwatamkie rasmi kuwa mimi NINAUCHUKIA UMASKINI HALAFU ANAFUATIA SHETANI. UMASKINI NI FEDHEHA. UMASKINI NI LAANA. TUWAKATAE VIONGOZI WANAOTAKA KUTUAMINISHA KUWA WAO NI MASKINI.