Tanzania ya viwanda imeishia wapi au ilikuwa mwendelezo wa kuwadanganya wananchi?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Awamu ya 5 ilipoingia Madarakani CHINI ya TINGATINGA wa CCM Bwana MAGUFULI tulitangaziwa kuwa NCHI inaenda kuwa ya VIWANDA VITUPU na Tatizo la VIJANA wetu KUZURURA na Bahasha za VYETI Kusaka AJIRA linafika Mwisho. Kuna Waziri alizunguka lila Mkoa kuhakikisha Kila Mkoa unajenga VIWANDA 100. Tukambiwa sasa ni zamu ya WAZUNGU kuvaa MITUMBA kutoka TANZANIA.

Wenye AKILI KUBWA tulijua ni UONGO hakuna cha TANZANIA ya VIWANDA kwani ilikuwa RAHISI kufufua VIWANDA vilivyopo kuliko Kutafuta Maeneo Mapya na kuanza kujenga Upya kwani Gharama zake ni Kubwa.

Kufufua Viwanda ni rahisi kwa sababu Majengo yapo,Maji na Umeme vipo Barabara zipo kinachobadilika ni MITAMBO TU.

Je ni VIWANDA vingapi vimejengwa na kukamilika? Je vipi ktk Mikoa gani? Je, ni Viwanda vya Nini? Je vimeajiri watu wangapi? Je, Vijana wetu wameacha kuzurura na Bahasha kusaka Ajira?

Mwenye hizi TAKWIMU naomba Aziweke hadharani.
 
Viwanda vipo, mkoa wa pwani unaviwanda zaidi ya 300 ila havimilikiwi na serikali.

Vinatengeneza material mbali mbali, vinafanya kazi siku saba kwa week, sasa kama wewe unahoji uwepo wa viwanda unahisi vijana watembea na bahasha za vyeti watajua hivyo viwanda mahali vipo?

Kingine viwandani inatakiwa skills
Welders, operators, mechanicals, na sio theory.
 
Tanzania inajivunia kuwa na wakata mauno tu waimba amapiano na singeli tu, machawa, wambea, wapenda udaku tu.

Hicho ndiyo mjivunie

Ova
 
Ni jambo zuri kuwa na serikali ya viwanda lakini ni vyema kuwa na tafsiri ya mambo ambayo hujiri baada ya bidhaa yoyote kutengenezwa kiwandani. Kwanza kabisa, watanzania hatuna mazoea ya kuunga mkono uzalishaji unaofanywa na watanzania wenzetu.

Hali hii inaweza kufanya bidhaa zinazo tengenezwa nchini kushindwa kuuzika. Tuelewe kwamba hii ni biashara na masoko ya bidhaa nyingi duniani yameisha kamatwa na viwanda vyenye umaarufu pamoja na viwanda vyenye uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zaidi.

Tunapofikiria kuongeza uzalishaji viwandani, tufikirie pia utangazaji, usambazaji wa bidhaa na jinsi ya kuwashawishi walio wengi kutumia bidhaa hizi. Zoezi hili lisipo fanyika kwa uangalifu, viwanda hivi havita weza kustahimili wimbi ya biashara.

Kama uwekezaji ungekuwa rahisi kama tunavyo fikiria, tunaweza kushiriki katika suala zima la kuboresha bidhaa za nchi rafiki katika makampuni ambayo tayari yamejizatiti katika biashara mbalimbali. Hili linaweza kuwa tangaza watanzania walio bobea katika tasnia ya uzalishaji
 
Nenda pwani uone watu walivyoangusha viwanda..kwa sasa mnasema mmefungua nchi mnaagiza hadi cement na tiles..hivyo viwanda vitapataje hamsa.
 
Viwanda vipo, mkoa wa pwani unaviwanda zaidi ya 300 ila havimilikiwi na serikali.

Vinatengeneza material mbali mbali, vinafanya kazi siku saba kwa week, sasa kama wewe unahoji uwepo wa viwanda unahisi vijana watembea na bahasha za vyeti watajua hivyo viwanda mahali vipo?

Kingine viwandani inatakiwa skills
Welders, operators, mechanicals, na sio theory.
Tuliambiwa kila Mkoa uwe na VIWANDA 100 ndio tunahoji mkuu maana hapa Dar hatuvioni hivyo 100 vilivyojengwa
 
Awamu ya 5 ilipoingia Madarakani CHINI ya TINGATINGA wa CCM Bwana MAGUFULI tulitangaziwa kuwa NCHI inaenda kuwa ya VIWANDA VITUPU na Tatizo la VIJANA wetu KUZURURA na Bahasha za VYETI Kusaka AJIRA linafika Mwisho. Kuna Waziri alizunguka lila Mkoa kuhakikisha Kila Mkoa unajenga VIWANDA 100. Tukambiwa sasa ni zamu ya WAZUNGU kuvaa MITUMBA kutoka TANZANIA.

Wenye AKILI KUBWA tulijua ni UONGO hakuna cha TANZANIA ya VIWANDA kwani ilikuwa RAHISI kufufua VIWANDA vilivyopo kuliko Kutafuta Maeneo Mapya na kuanza kujenga Upya kwani Gharama zake ni Kubwa.

Kufufua Viwanda ni rahisi kwa sababu Majengo yapo,Maji na Umeme vipo Barabara zipo kinachobadilika ni MITAMBO TU.

Je ni VIWANDA vingapi vimejengwa na kukamilika? Je vipi ktk Mikoa gani? Je, ni Viwanda vya Nini? Je vimeajiri watu wangapi? Je, Vijana wetu wameacha kuzurura na Bahasha kusaka Ajira?

Mwenye hizi TAKWIMU naomba Aziweke hadharani.

View: https://youtu.be/SopTDQLMKxk?si=4s4lpmFEusOj_A0a
 
Back
Top Bottom