BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,331
Wanyakyusa wanasema: "Indalama syalile Juta", yaani Fedha ilimla au ilimuua Yuda [Iskarioti]! Tanzania ya leo, mtu mwenye pesa na mamlaka anaweza kumfundisha na kumuamrisha hata Askofu Mkuu au Mufti katika mambo ya imani hata kama mtoa amri hana hata Cheti cha Theologia au Tauhidi! Ole wake Askofu Mkuu au Mufti akatae, kesho yake anaweza kukuta migogoro kwenye Taasisi yake yenye lengo la kutaka kumng'oa na akipona hiyo, Taasisi yake itawekewa vikwazo katika kupata vibari maalum ikiwemo hata kunujua viwanja!
Hata kama hana Cheti cha Fundi Mchundo (Technician), lakini mtu mwenye Fedha na mamlaka anaweza kutoa maelekezo ya kitaalam kwa Mhandisi (Engineer) mwenye Shahada ya Uzamivu. Ole wake Mhandisi akosoe! Hata kama hana hata Cheti cha Uhasibu Ngazi ya Msingi, mtu huyo anaweza kutoa maelekezo kuhusu utalaam wa Fedha kwa Mhasibu mwenye Cheti za Ubingwa katika Uhasibu (CPA, ACCA, CIMA).
Hata kama hana hata Astashahada ya Kodi, mtu mwenye mamlaka na Fedha anaweza kumfundisha namna ya kupanga mfumo wa Kodi mtu ambaye ni Mkadiliaji wa Kodi (Tax Assessor) mwenye Shahada ya Ubingwa masuala ya Fedha na Kodi (MSc in Fiscal Studies/Policies). Hata kama hana Cheti cha Sheria kutoka Chuo cha Lushoto, mtu huyo anaweza kumpangia namna ya kutafsiri Sheria Jaji Mkuu. Hata kama hana hata Cheti cha masuala ya Siasa na Utawala, mtu huyo anaweza kumfundisha taaluma ya siasa mbombezi aliye Profesa wa Sayansi ya Siasa na Utawala.
Ikifikia hatua hiyo, jamii au nchi inakoma kufuata maadili ya uongozi na mifumo ya uendeshaji nchi (Katiba), bali inaongozwa kwa utashi wa viongozi. Kiongozi anachukuliwa kuwa anajua kila kitu. Taratibu na Kanuni za Kazi na uendeshaji nchi hukoma, badala yake Taasisi na nchi huongozwa kwa matamko. Wakurugenzi huacha kufuata miongozo na kanuni za kazi, badala yake kila siku husubiri matamko ya viongozi na watawala! Watu huanza kuabudu Fedha, vyeo na wenye madaraka. Haki anageuka kuwa kaburi la marehemu asiyekuwa na ndugu ambalo haliwezi hata kufagiliwa.
Hivi ni malaika gani atakayeshuka kutoka mbinguni ili kulionya Taifa la namna hii? Je, ni Gabrieli (Jibrili), Raphael au Mikaeli? Ole wao kizazi kisichosikia sauti na dhamiri ya Mungu kupitia kwa watumishi wake (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Mkuu Bandekile Mwamakula