Kioja cha mhudumu wa basi la ngorika:

Kioja cha mhudumu wa basi la ngorika:

meidimu sirkon

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
202
Reaction score
37
Juzi siku ya j'mosi nilikuwa nasafiri kutoka Simanjiro kwenda Mkoa K'njaro.

Nilipomaliza shughuli zangu Moshi nikaamua kwenda Mkoa wa Arusha kwa ndugu ambayo ilinilazimu kupanda basi la kuanzia Moshi au yale mabasi ya Mikoani .

Kwa sababu mabasi ya mikoani hayasimami mara kwa njiani nikaamua kupanda basi la Ngorika na kupata kiti cha mwisho ktk gari hilo.

Hivyo safari ikaanza kwenda Ars basi ilipofika eneo la mailisita Mhudumu wa Kike akafika eneo tulipo akiwa amevaa miwani mkononi amepakata kitabu cha tiketi au risiti na kalamu Akaanza kuandika tiketi na kukikata na kudai na nauli kwa kusema "HAPO WEWE" nilifikiri sana mambo mengi kichwani kuwa huyu mhudumu angalau amefuzu mafunzo VETA ili kufanya kufanya kazi hii muhimu .

Pili kazi inafikirika kuwa na ubavu wa kufokea wateja au abiria hii ilidhihirika pale nilpomuuliza mbona hii tiketi ulionipa haina namba ya usajili wa gari hili nililopanda ,Alichonijibu namba ya nini? Kwani una shida gani mpaka unaniuliza za gari ,kwanza una begi kwenye buti la gari useme litapotea.

Nami nikamjibu kuwa kila binadamu ana jina lake,na magari yanatambulika kwa namba ya usajili.

Ndipo kwa hasira akachukua tiketi yangu akaandika namba ya gari ambayo ni T768- akanikabidhi tiketi nilpoisoma nikagundua kwamba sio namba sahihi ,Nikamuuliza tena mbona namba hii sio sahihi?

Alichonijibu nyie watu Moshi mnasumbua sana unataka nikubebe mgongoni ,name nikamjibu sikufika huku unaonekana kuwa somo la "customer care hukupata"

Mwisho akaniambia kama nimekuudhi sana unaweza kwenda ofisi yetu pale Arusha au soma namba gari hapo nyuma baadae hukishuka kwenye basi hili ,Nikamwambia hata mbele kuna namba za usajili wa gari.

Namba la gari lenyewe ni T768 BKW.

Hitimisho langu kwamba Sumatra & TRA wanalijua jambo hili kuwa magari mengi hayatoi tiketi kwa kwa abiria au wakitoa haikuandikwa namba za usajili kwenye tiketi hizo.

Pia wenye magari mnaajiri wafanyakazi wenye taaluma ya usafirishaji au mnaajiri wapiga debe vituo vya mabasi?Madereva wenu huwa na likizo ya kila mwaka?

Naomba kuwasilisha hoja JF! Angalia tiketi hapo chini.
DSC00413.JPG
 
Pole sana mimi pia yamenitokea nilikuwa nampeleka mdogo wangu shule weruweru akaanza maneno yake ya shombo eti mizigo imezidi hawezi pakia wakati tiken nilikata jana yake ubungo na nikawaelekeza napandia kimara nina mizigo.
Kaongea njia nzima nilikasirika sana uvumilivu ukaniisha mimi ni askari jeshi (nilivaa kiraia) ikabidi nimpe makonde na kumwamuru dereva apeleke gari polisi.
 
Juzi siku ya j’mosi nilikuwa nasafiri kutoka Simanjiro kwenda Mkoa K’njaro.
Nilipomaliza shughuli zangu Moshi nikaamua kwenda Mkoa wa Arusha kwa ndugu ambayo ilinilazimu kupanda basi la kuanzia Moshi au yale mabasi ya Mikoani .Kwa sababu mabasi ya mikoani hayasimami mara kwa njiani nikaamua kupanda basi la Ngorika na kupata kiti cha mwisho ktk gari hilo.Hivyo safari ikaanza kwenda Ars basi ilipofika eneo la mailisita Mhudumu wa Kike akafika eneo tulipo akiwa amevaa miwani mkononi amepakata kitabu cha tiketi au risiti na kalamu Akaanza kuandika tiketi na kukikata na kudai na nauli kwa kusema “HAPO WEWE” nilifikiri sana mambo mengi kichwani kuwa huyu mhudumu angalau amefuzu mafunzo VETA ili kufanya kufanya kazi hii muhimu .Pili kazi inafikirika kuwa na ubavu wa kufokea wateja au abira hii ilidhihirika pale nilpomuuliza mbona hii tiketi ulionipa haina namba ya usajili wa gari hili nililopanda ,Alichonijibu namba ya nini? Kwa unashida gani mpaka unaniuliza za gari ,kwanza una begi kwenye buti la gari useme lipotea .Nami nikamjibu kuwa kila binadamu ana jina lake,na magari yanatambulika kwa namba ya usajili.Ndipo kwa hasira akachukua tiketi yangu akaandika namba ya gari ambayo ni T768- akanikabidhi tiketi nilpoisoma nikagundua kwamba sio namba sahihi ,Nikamuuliza tena mbona namba hii sio sahihi ?Alichonijibu nyie watu Moshi mnasumbua sana unataka nikubebe mgongoni ,name nikamjibu sikufika huku unaonekana kuwa somo la “customer care hupata”
Mwisho akaniambia kama nimekuudhi sana unaweza kwenda ofisi yetu pale Arusha au soma namba gari hapo nyuma baadae hukishuka kwenye basi hili ,Nikamwambia hata mbele kuna namba za usajili wa gari.Namba la gari lenyewe ni T768 BKW
Hitimisho langu kwamba Sumatra & TRA wanalijua jambo hili kuwa magari mengi hayatoi tiketi kwa kwa abiria au wakitoa haikuandikwa namba za usajili kwenye tiketi hizo.Pia wenye magari mnaajiri wafanyakazi wenye taaluma ya usafirishaji au mnaajiri wapiga debe vituo vya mabasi?Madereva wenu huwa na likizo ya kila mwaka?
Naomba kuwasilisha hoja JF! Angalia tiketi hapo chini.
View attachment 118705

Suala la customer care B0NG0 ni taabu tupu!
 
Kwa kweli kampuni ya NGORIKA inabidi iangalie wafanyakazi wake, Pole sana inakera na inauzi sana unapokutana na wafanyakazi wabovu kama hao wanajisahau hawajui we are in the free market economy. Kesho wakikosa wateja wanasema wamelogwa kumbe ni customer care mbaya zao na maneno ya dharau yanayoweza kuwakatisha watu tamaa ya kutumia magari yao. Ninaandika hivi kwani umenitonesha kidonda ni asubuhi ya tarehe 19/10/2013 siku ya Jumamosi nilipofika Ubungo muda wa saa 12 kasoro dk 20 nikitafuta basi la kwanza la kwenda Moshi ndani ya booking office yao tuliwakuta kaka na dada mmoja wanakatisha tiketi swali langu kwao lilikuwa ngorika ya kwanza imejaa nikaambiwa bado nikauliza tena ni luxury au basi la kawaida nikaambiwa kuna ngorika 2 zinaondoka saa 12 ya kawaida na luxury nikawaambia ok luxury ni shilingi ngapi nikaambiwa 32000 bila ajizi nililipa kwani nilikuwa sitaki kukosa basi hilo na sikuhitaji kupoteza muda nikaingia ndani kutafuta basi, nililikuta basi na kwa bahati alikuwepo mwana dada mwingine naye akafanya kama mimi akakata basi hilohilo kwa bei hiyohiyo. Eeh bwana yaliyotukuta tulipofika kwenye basi yalinikera sana kwani tulimkuta dada amesimama mlangoni akiwa anakatia watu tiketi tukamuuliza basi linaondoka saa ngapi kwani tumesimaa muda mpaka tunaona ngorika nyingine inaondoka we! we! Sikujua kama tunaongea na mtu mwenye uelewa mbovu akaanza wewe unachotaka ni kuona siti au ni kujua basi linaondoka saa ngapi ww choma ndani usituwekee usiku mwenzangu akamueleza tumeuliza hivyo kwani saa 12 imeshafika na hatuoni dalili yoyote acha wahudumu waanze kumfokea kwa maneno ya ukali nikawaambia hii ni biashara lazima muwe wakweli walitutusi na kutudhalilisha sana niliwatizama wale wahudumu bila kujua nn cha kufanya kaka mmoja akatuambia mmedanganywa hiyo gari inatoka saa 12.30 nikawaambia mnapaswa kuwa wakweli kwa wateja wenu ila huyu dada ambaye ana mwili wa kati na nywele amenyoa akiwa amepaka lipshine nyingi mdomoni na kaka mmoja walikuwa kama vichaa. Kioja ni hiyo gari wanayoiita luxury si kweli hata city belt hakuna ni gari namba 1767 BKW ndani ya gari tukagundua abiria wamekatiwa tiketi 25000 jirani yangu alinishangaa na kwa vile walikuwa wameshanichafua ilibidi nikae kimya nikiwa na maamuzi mimi kupanda Ngorika marufuku hata nikikwama porini kwa bahati aliibuka dada mmoja ndani ya gari akihoji kwanini ametozwa sh 32000 wakati walio wengi wametozwa 25000 wakati anahoji hayo yote kwa mwanadada mwingine ambaye ndiye hutembea na gari nilimwonea huruma nikasema ngoja huyu dada mkata tiketi amsikie ataonja kauli za dharau mpaka atajuta na ndiyo yaliyomkuta aliambiwa acha kuchezea riziki za watu kwahiyo unataka tukale wapi kilichofuata waliamua kumshusha kwani aliwaambia nakwenda kuwaambia SUMATRA akaambiwa ngoja tukuitie ili ujue hatuwaogopi nao ni watu kama sisi.
Napenda kuwashauri wamiliki wa mabasi kuwafuatilia waajiri wao na kwa hili nipo tayari kulitolea ushahidi utakapohitajika nilitamani nimjue mkurugenzi wa magari haya nimweleze nini kinaendelea kwani nina hakika hamna mtu anayependa kuona biashara yake inaharibiwa hivi. Poleni sana wahanga wenzangu wa NGORIKA
 
Achaneni na majina ndugu zangu!!!!

Yapo makampuni mapya mazuri ajabu nimewahi panda Dar express saa tatu asbh (Benz) kufika arusha saa nne usiku,head lamps haziwaki vizuri yaani hatari tupu ,wadau mlirekebishe!!!!!

Wakati wa kurudi nikapanda Kidia baada ya kishauriwa na tax driver kwa kweli sikujuta,nice bus,mwendo mzuri!!!

Inawezekana majina yamewalevya wamiliki wanajisahau!!!
 
Pole sana mimi pia yamenitokea nilikuwa nampeleka mdogo wangu shule weruweru akaanza maneno yake ya shombo eti mizigo imezidi hawezi pakia wakati tiken nilikata jana yake ubungo na nikawaelekeza napandia kimara nina mizigo.
Kaongea njia nzima nilikasirika sana uvumilivu ukaniisha mimi ni askari jeshi (nilivaa kiraia) ikabidi nimpe makonde na kumwamuru dereva apeleke gari polisi.

...Wewe ndio Ulijua cha Kufanya, Sio kulalamika tu! Big Up. Ningekuwepo ningekupa tafu kuwabwenga makonzi hao wakalamba! Mtu unatoa hela yako yliyoisotea halafu wao wanaleta za kuleta! Costumer care Bongo ni Majanga matupu.

Pole sana mimi pia yamenitokea nilikuwa nampeleka mdogo wangu shule weruweru akaanza maneno yake ya shombo eti mizigo imezidi hawezi pakia wakati tiken nilikata jana yake ubungo na nikawaelekeza napandia kimara nina mizigo.
Kaongea njia nzima nilikasirika sana uvumilivu ukaniisha mimi ni askari jeshi (nilivaa kiraia) ikabidi nimpe makonde na kumwamuru dereva apeleke gari polisi.

ha ha ha askari jeshi, enhee alipopelekwa polisi ikawaje?
 
Huyo mjeda ndo alifanya cha maana. Unampa hata makwenzi ma5 yanatosha. Wanakera sana hawa wahudumu wa ma bus
 
ndo matokeo ya ajira za kupeana hizo

Mtoto wa mjomba mtoto wa shangazi

Kwa route ya Dar Mbeya natoa ushauri wa bure kabisa, mwanaJf yeyote atakayesafiri njia hiyo ajaribu kupanda basi linaitwa NDENJELA , hakika utashangaa na kujiuliza kwanini wanamjali abiria kiasi kile.
Basi linapoondoka pale Ubungo unaweza kujisahau ukadhani upo kwenye ndege, maana utasikia sauti mororo ya mdada ikiwasalimia, kisha wanatoa briefing ya safari yote na kusisitiza kuwa abiria ukiwa na tatizo lolote usisite kumwita mhudumu akusaidie.
Basi kama hilo likija route ya Arusha hakika akina Ngorika, Saibaba, Dar Xpress wote watatafuta vigagura ili wawawekee ndumba lipinduke.
 
Ungemtandika makofi akili imkae sawa, anafikiri kila abiria ni wakuburuzwa
 
Juzi siku ya j’mosi nilikuwa nasafiri kutoka Simanjiro kwenda Mkoa K’njaro.
Nilipomaliza shughuli zangu Moshi nikaamua kwenda Mkoa wa Arusha kwa ndugu ambayo ilinilazimu kupanda basi la kuanzia Moshi au yale mabasi ya Mikoani .Kwa sababu mabasi ya mikoani hayasimami mara kwa njiani nikaamua kupanda basi la Ngorika na kupata kiti cha mwisho ktk gari hilo.Hivyo safari ikaanza kwenda Ars basi ilipofika eneo la mailisita Mhudumu wa Kike akafika eneo tulipo akiwa amevaa miwani mkononi amepakata kitabu cha tiketi au risiti na kalamu Akaanza kuandika tiketi na kukikata na kudai na nauli kwa kusema “HAPO WEWE” nilifikiri sana mambo mengi kichwani kuwa huyu mhudumu angalau amefuzu mafunzo VETA ili kufanya kufanya kazi hii muhimu .Pili kazi inafikirika kuwa na ubavu wa kufokea wateja au abira hii ilidhihirika pale nilpomuuliza mbona hii tiketi ulionipa haina namba ya usajili wa gari hili nililopanda ,Alichonijibu namba ya nini? Kwa unashida gani mpaka unaniuliza za gari ,kwanza una begi kwenye buti la gari useme lipotea .Nami nikamjibu kuwa kila binadamu ana jina lake,na magari yanatambulika kwa namba ya usajili.Ndipo kwa hasira akachukua tiketi yangu akaandika namba ya gari ambayo ni T768- akanikabidhi tiketi nilpoisoma nikagundua kwamba sio namba sahihi ,Nikamuuliza tena mbona namba hii sio sahihi ?Alichonijibu nyie watu Moshi mnasumbua sana unataka nikubebe mgongoni ,name nikamjibu sikufika huku unaonekana kuwa somo la “customer care hupata”
Mwisho akaniambia kama nimekuudhi sana unaweza kwenda ofisi yetu pale Arusha au soma namba gari hapo nyuma baadae hukishuka kwenye basi hili ,Nikamwambia hata mbele kuna namba za usajili wa gari.Namba la gari lenyewe ni T768 BKW
Hitimisho langu kwamba Sumatra & TRA wanalijua jambo hili kuwa magari mengi hayatoi tiketi kwa kwa abiria au wakitoa haikuandikwa namba za usajili kwenye tiketi hizo.Pia wenye magari mnaajiri wafanyakazi wenye taaluma ya usafirishaji au mnaajiri wapiga debe vituo vya mabasi?Madereva wenu huwa na likizo ya kila mwaka?
Naomba kuwasilisha hoja JF! Angalia tiketi hapo chini.
View attachment 118705
Wenye mabasi wakileta LONGOLONGO piga namba hizi 0657576646 au 0752340820. Hizi ni namba za chama cha kutetea maslahi ya abiria. Huwa wanawashikisha adabu wafanyakazi wa kwenye mabasi.
 
Nia aibu kubwa kwa basi hilo ambalo lipo katika biashara hiyo kwa zaidi ya miaka 40 sasa...
 
Yaani mkuu ninakuunga mkono asilimia mia nimetembea mikoa mingi kwa usafiri wa aina mbalimbali sijawahi kutana na customer care kama ya Ndenjela bus, wako sawa sana kwa customer care utasema kwenye ndege, on top of that wana tangaza kwa kingereza na kiswahili pia wana dereva wakike kwenye basi mojawapo yuko very competent.

Back
Top Bottom