Slow pancha
Senior Member
- Mar 16, 2013
- 182
- 121
Kwa abiria wa iringa mi nashauri mpande sanya one,ndio basi ya uhakika
huyu ni dereva wa NDEJELA jamani hii gari ni nzuri kupanda usipime utafikiri uko sijui kwenye ndege ama kwenye hoteli fulan nzuri kwa huduma zao
Kwa route ya Dar Mbeya natoa ushauri wa bure kabisa, mwanaJf yeyote atakayesafiri njia hiyo ajaribu kupanda basi linaitwa NDENJELA , hakika utashangaa na kujiuliza kwanini wanamjali abiria kiasi kile.
Basi linapoondoka pale Ubungo unaweza kujisahau ukadhani upo kwenye ndege, maana utasikia sauti mororo ya mdada ikiwasalimia, kisha wanatoa briefing ya safari yote na kusisitiza kuwa abiria ukiwa na tatizo lolote usisite kumwita mhudumu akusaidie.
Basi kama hilo likija route ya Arusha hakika akina Ngorika, Saibaba, Dar Xpress wote watatafuta vigagura ili wawawekee ndumba lipinduke.
nikuombe samahani san wahusika tupo humu humu jf. Nimelisikia hilo nitalifanyia kazi huwa kuna no zetu kwenye tiketi unaeza kupiga ukaomba kuongea nasi ofisi kuu kabla hujashuka kwenye gari. Nimepeta no ya gari nitafanyia kazi. Ila tusamehe sana ndugu yangu. Ngorika leading other follow. Tupo barabarani kuanzia mwaka 1963 hatutaki tupoteze wateja leo kwa ajili ya mtu mmoja. Usiache kupakia ngoria pakia yeyote.
Wiki iliyopita, ilikuwa jumanne, nilipanda gari la RATCO kutoka Dar hadi Muheza. Nilihudumiwa vizuri. Jioni ya siku hiyo hiyo, saa 10:30 jioni nikapanda tena RATCO kurejea Dar. Nikiri kuwa hili gari la jioni nilihudumiwa vizuri zaidi. Kiyoyozi safari nzima. Kilichonivutia zaidi ni moyo wa uungwana aliouonyesha mhudumu (kondakta?) wa basi hilo. Ni mweupe, mwembamba. Nilimuomba tukifika Mkata nipate 'mchuzi' wa mbuzi. Yule dada hakufanya hiana. Akanitaka tukishakaribia, nimkumbushe. Kweli, tulipokaribia nilimkumbusha. Wakati huo nilishamweleza jamaa yangu muuza 'mchuzi' awe tayari. Kilichofanywa ni dereva kushika breki na mimi nikakabidhiwa 'mchuzi' wangu kwa raha mustarehe kabisa. Kwa ukarimu huo, sidhani kama kampuni nyingine zaidi ya RATCO zitakuwa na fursa ya kunitambua kama abiria wao.
huyu ni dereva wa NDEJELA jamani hii gari ni nzuri kupanda usipime utafikiri uko sijui kwenye ndege ama kwenye hoteli fulan nzuri kwa huduma zao