Kingunge: More MPs to lose in 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingunge: More MPs to lose in 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitia, Oct 11, 2009.

 1. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  By Thobias Mwanakatwe
  11th October 2009  [​IMG]
  Kingunge Ngomale-Mwiru.

  Veteran politician Kingunge Ngomale-Mwiru has blamed opposing groups and constant wrangles within Chama cha Mapinduzi (CCM) on selfish persons who would always want to be elected to parliament.

  He said there was no doubt that some of the sitting members of parliament from the ruling CCM and opposition parties would lose in the next general election, observing that such a prospect was causing fear among some of the members of parliament.

  Ngombale-Mwiru who is a member of the CCM National Executive Committee (NEC) made the remarks when officiating at a opening function of regional party youth wing meeting in Mbeya yesterday. He used the occasion to install youth leaders in the region, among them Mbeya regional youth commander, Laurent Mwakajumulo as well as district youth commanders.

  The CCM district commanders are Epson Mwaikambo ( Mbeya Urban), Jovita Diame (Mbeya Rural), Barton Kihaka, (Mbarali), Philemon Msomba (Chunya), Elias Mwakalinga (Kyela), Prof.Mark Mwandosya (Rungwe) and Gedion Cheyo (ILeje). Mbozi district did not get youth commander as it did not meet the required standards.

  However, the politician maintained that opposition parties should not think it would be a joy ride in their efforts to win may parliamentary seats.

  He said: “There are those who are predicting that CCM members of parliament will lose badly in the coming general elections, making some in the opposition camp to feel that victory would be won easily but the truth remains that many new faces will come from within CCM.”

  He said such changes are always experienced even within party elections, citing NEC where new entrants are always not below 50 percent, explaining that it was that kind of democracy that makes CCM alive.

  Kingunge blamed the opposition parties for lack of democracy which he said has almost rocked all of the parties. He alleged that there is no future for the opposition parties in the country.


  SOURCE:
  THE GUARDIAN
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Thanks for Info.
  So Kingunge now is confident that CCM had chose wrong chaps For Parliament and force them to it without consent of Wananchi. Yes that is how it is,they want to change those to new faces hoping Wananchi knows nothing about it.
  Poleni CCM.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  He is still searching for relevancy!
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  Kingunge: Wabunge wengi watabwagwa

  Na Mwandishi wetu
  11th October 2009


  [​IMG] Alilia makundi ndani ya CCM
  [​IMG] Awaonya vijana wasijiingize
  [​IMG] Asema mafiadi ni kikwazo
  [​IMG]
  Kingunge Ngombare Mwiru .


  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na muasisi wa chama hicho, Kingunge Ngombare Mwiru ametabiri kuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2010, wabunge wengi wakiwemo wa CCM wataangushwa vibaya.
  Aidha, amesema suala la makundi ndani ya CCM linatokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi ambao kila mwaka wanataka wachaguliwe wao na anapochaguliwa mtu mwingine inakuwa nongwa.
  Kingunge ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Vijana la Mkoa wa Mbeya.

  Kingunge alisema hivi sasa limekuwa ni jambo lililozoeleka kwani kila baada ya miaka mitano kupita kulingana na utafiti ambao ulishafanywa ni kwamba kati ya asilimia 40 hadi 60 wabunge wanaangushwa kwenye uchaguzi lakini kinachofurahisha ni kwamba wabunge wapya wanaochaguliwa wanatoka CCM na siyo kutoka chama kingine cha siasa.

  Alisema mabadiliko hayo ya wabunge pia yamekuwa yakitokea wakati wa uchaguzi wa viongozi ndani ya chama ambapo mfano mzuri ni uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM (NEC) wapya wanakuwa siyo chini ya asilimia 50 na utaratibu huo ndio unaokifanya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa chama chenye uhai sana kila mwaka.

  Akizungumzia makundi ndani ya CCM, alisema umekuwa ni ugonjwa mbaya sana ambao unasababisha viongozi na wanachama kujengeana chuki, shari na unadhoofisha chama.

  Alisema matatizo yote hayo ya makundi yanasababishwa na ubinafsi wa baadhi ya viongozi na wanachama ambao kila uchaguzi wanataka wachaguliwe wao tu.

  "Ubinafsi umekuwa ni ugonjwa mbaya sana, unavuruga malengo, unadhoofisa na kujengeana shari ndani ya chama, mtu akipata ubunge anataka awe ni yeye tu, ukishindwa inakuwa nongwa, uenyekiti nao unataka uwe wewe tu ukishindwa hapapitiki," alisema Kingunge.

  Kingunge ambaye pia ni Kaimu Kamanda wa Vijana wa CCM Taifa, alisema changamoto iliyopo kwa vijana ni kukataa kujiingiza kwenye makundi ya viongozi ambao wanataka kupata vyeo kwa kutumia mgongo wa vijana ambapo kukiwa na msimamo huo UVCCM itaheshimika kama ilivyokuwa zamani enzi za chama cha TANU.

  Alisema vijana wahakikishe kundi lao liwe ni la UVCCM na CCM na siyo kuwa na kundi kwa ajili ya watu fulani na viongozi ambao kazi yao kubwa imekuwa ni kuwashawishi vijana kwa fedha ili wawakubali na ndipo wanapata nguvu ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ubunge.

  "UVCCM dhamana yake kubwa ni kujenga maadili ya vijana wadogo ili wakue katika maadili ya kichama, mnapojiingiza katika tamaa za fedha mnapoteza maadili na mwelekeo wenu," alisema Kingunge na kueleza kuwa amefurshishwa na hatua ya vijana wa CCM mkoa wa Mbeya kutoa tamko la kwamba hawakubali kutumiwa na watu wanaotaka kugombea ubunge mwakani.

  Katika mkutano huo aliwasimika rasmi Kamanda wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Laurenti Mwakajumulo na Makamanda wengine wapya wa Vijana wa wilaya zote za mkoa mkoa wa Mbeya.

  Makamanda wa vijana wa CCM waliosimikwa rasmi jana kwenye mkutano huo ni Epson Mwaikambo toka Wilaya ya Mbeya Mjini, Jovit Diame (Mbeya Vijijini), Barton Kihaka (Mbarali), Philemon Msomba (Chunya), Elias Mwakalinga (Kyela), Profesa Mark Mwandosya (Rungwe), Gedion Cheyo (Ileje), wakati Wilaya ya Mbozi haikupata Kamanda wa Vijana kwa sababu waliopendekezwa hawakuwa na vigezo.

  Kingunge alisema pamoja na mabadiliko ya wabunge yanayotarajia kutokea wakati wa uchaguzi huo lakini wabunge wapya watatoka CCM na hivyo vyama vya upinzani visitarajie kuwa kuangushwa kwa wabunge toka chama tawala ndio itakuwa mteremko kwao kushinda na kuyanyakua majimbo hayo.

  Mjumbe huyo wa NEC alivigeukia vyama vya upinzani kwa kuvishambulia kuwa wanaodhani kuwa mabadiliko hayo ya wabunge yatawafanya washinde wao wamepotoka kwa sababu vyama hivyo vingi bado havina demokrasia ndani ya vyama vyao hivyo bado vina safari ndefu kuweza kushinda kwa kunyakua viti vingi vya ubunge kama ambavyo CCM imekuwa ikishinda kila mwaka.

  Alisema vyama vya upinzani lazima vitambue kuwa safari ya kwenda Ikulu lazima kwanza chama kiwe na sera nzuri za kuwashawishi wananchi wakipende na kiwe na demokrasia na siyo kukurupuka tu na kuanza mipango ya kutaka kuingia Ikulu huku wakiwa na hoja kwamba CCM imekaa sana madarakani hivyo isichaguliwe tena jambo ambalo haliwezi kuvisaidia vyama hivyo.

  Awali Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Regnald Msomba alisema vijana mkoani hapa wamekusudia kufanya mabadiliko ndani ya chama kwa kukataa kutumiwa na wanachama ambao wanakusudia kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

  Naye Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Rhoda George akitoa taarifa ya jumuiya hiyo alisema hali ya chama katika mkoa wa Mbeya siyo shwari hasa kutokana na kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambapo kumekuwa na makundi ya wanachama wanaotaka kugombea na pia baadhi ya viongozi wamekuwa wakifanya mikakati ya kupanga safu yao ya wanachama wanaowataka wachaguliwe.
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kingunge has outlived his usefullness.

  He is dead wood.

  Wengi tulimheshimu sana kingunge kama a left-of-centre political activist.

  Alikuwa mtu wa watu. Ni kati ya viongozi wachache walioamini tena kwa kuapa kiapo cha chama kutetea Taifa kiitikadi katika ule mlengo wake wa kushoto unaofahamika na wengi.

  Mlengo wa kushoto ni pamoja na nguvu ya umma, uongozi wa kutetea maskini na wanyonge kushika hatamu za utawala.

  Kingunge alianza kuonekana kama mchangiaji wa mawazo ya kiitikadi katika muelekeo nilioulezea.
  Tulikuwa tumekosea kabisa.

  Kumbe kama kinyonga Kingunge is an opportunist.

  Inatia kinyaa kuona mtetezi mahiri wa ujamaa anajiingiza katika biashara za kitapeli kama za uendeshaji wa stendi ya Ubungo na uzoaji taka , bila kulipa kodi za Serikali.

  Kitendo cha Kingunge vile vile cha kukumbatia mafisadi ndio kimmemmaliza kabisa katika ulingo wa kuweza kuaminika kama mchangiaji serious wa siasa za hapa nchini.

  Sana sana Kingunge ameshakuwa mtawala (a doer not a thinker)
   
Loading...