Lazima bunge lijadiri ishu yoyote ile ya kidini au vinginevyo, isipokuwa lisijihusishe na uanzishwaji wa taasisi yoyote ya kidini, iwe mahakama ya kidini, kujiunga na kundi lolote kama taifa kwa misingi ya dini. Kama dini zinataka kuanzisha mambo yao basi ziachiwe zenyewe na bunge/serikali isijihusishe na uanzishwaji huo.
Mwisho wa yote ni kuwa kila kitu kinaenda kikatiba na unapoamuwa kuiacha kitu bila kuwemo ndani ya katiba unakaribisha machafuko. Haya Waislamu watapoanzisha chombo chao na kuamuwa kufanya watakavyo nani atakuwa muamuzi? Au kukianzishwa kanisa kama la Kibeterwe lenye msingi wa mauwaji nani atawashughulikia na vipi iwapo hayo ni maamuzi yao?
Bottom line Katiba (Bunge) ndio msingi wa utawala Bora!