Kingunge, Makamba mnamuunga mkono Nyalandu na hoja binafsi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingunge, Makamba mnamuunga mkono Nyalandu na hoja binafsi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Sep 7, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mbunge kuwasilisha hoja kupinga mijadala ya dini

  Exuper Kachenje na Fred Azzah

  MBUNGE wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM), jana ametangaza rasmi kuwa atatimiza ahadi yake ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kulitaka Bunge kupiga marufuku mijadala yote inayohusu masuala ya imani za dini ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria wakati wa mkutano wa 17.

  Nyalandu alitangaza hatua hiyo katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam akieleza kuwa tayari amepata wabunge wengi wanaomuunga mkono. Mkutano wa 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano utafanyika mwezi Oktoba.

  Mbunge huyo pia alivitahadharisha vyama vya siasa kuwa makini katika kutunga sera na kuepuka kuingiza kwenye ilani za vyama vyao, mambo yanayoweza kusababisha mgawanyiko na utengano kwa wananchi.

  Mbunge huyo kijana alidai kuwa tayari hoja yake imeungwa mkono na zaidi ya wabunge 100 kutokana na imani tofauti na vyama vyote vyenye wabunge, huku akijinadi kuwa anaamini kwamba hoja yake pia inaungwa mkono na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru.

  Alidai kuwa idadi ya wabunge waliotia saini kuunga mkono hoja yake ni kubwa ikilinganishwa na sheria inavyosema kuwa ili hoja ikubalike, ni lazima iwe imesainiwa na wabunge watano.

  Alibainisha kuwa kwa mujibu wa hoja yake, mijadala itakayoruhusiwa ni ile itakayokuwa na hoja mahususi inayohusu suala la dini, linalotishia usalama wa taifa na kuwa hilo lifanyike baada ya kujadiliwa na kuidhinishwa na kamati ya uongozi ya Bunge.

  Alisema hatua hiyo ifikiwe baada ya kamati hiyo kujiridhisha kwamba hoja husika haikiuki masharti ya misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Hoja yangu ni kulitaka Bunge la Tanzania kupiga marufuku mijadala yote inayohusu masuala ya imani za dini ndani ya Bunge, isipokuwa endapo kutakuwa na hoja mahususi inayohusu suala la dini linalotishia usalama wa taifa," alisema na kuongeza:

  "Hoja hiyo yaweza kujadiliwa tu baada ya kuidhinishwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge na kujiridhisha kwamba ni mahususi na haikiuki masharti ya misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Nyalandu.

  Kuhusu vyama vya siasa, Nyalandu alisema:" Nadhani itakuwa vyema vyama kuepuka masuala ya dini na ukabila. Vyama vinapaswa kuwa makini katika ilani zake visilete mijadala inayoweza kuwagawa wananchi."

  Alifafanua kuwa kimsingi hoja yake ameiandaa kwa kushirikisha wanasheria mbalimbali wakiwemo wa serikali na Bunge na kwamba, inalenga kupinga masuala ya imani za dini kujadiliwa ndani ya bunge kwa kuwa kufanya hivyo ni uvunjaji wa masharti na misingi ya katiba ya nchi ambayo serikali yake haina dini na hivyo kuwa ni hatari kwa amani ya nchi.

  "Msukumo wa kuleta hoja, hii umechangiwa kwa kiasi kikubwa na tabia iliyojitokeza hivi karibuni ya baadhi ya wabunge kujadili na kuitaka serikali kukubali kutungwa kwa sheria itakayowezesha kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi pamoja na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kujiunga na Jumiya ya nchi za Kiisilamu (OIC)," alisema Nyalandu.

  "Ni jambo la wazi kuwa zipo nchi ambazo zimejikuta kwenye migogoro mikubwa ya kisiasa na kijamii hadi kusababisha kuvunjika kwa amani na wakati mwingine hata vita kutokea... na ukifuatilia chanzo cha matatizo hayo, pamoja na mambo mengine, ni mijadala mbalimbali inayohusu masuala ya dini."

  Alisema mijadala ya dini imekuwa mikali na huchangiwa kwa hisia za imani za dini na hivyo kufanya bunge kuacha masuala yenye manufaa kwa nchi na mustakabali wake.

  Nyalandu alisema kuendeleza mijadala hiyo bungeni ni kukiuka masharti ya Katiba ya Tanzania inayotamka bayana kwamba Tanzania sio nchi ya kidini.

  Alisema kwa maana hiyo si vizuri kwa Bunge kubariki uvunjwaji huo wa katiba.

  Nyalandu alimuomba spika wa Bunge, Samuel Sitta na ofisi yake kuidhinisha hoja hiyo ili iwasilishwe katika mkutano wa 17 wa Bunge na kuwasihi wabunge kumuunga mkono.

  Alisema kama Bunge halitapiga marufuku mijadala ya kidini bungeni, kunauwezekano siku zijazo hoja binafsi ya kutaka serikali ianzishe mahakama ya Kikristo ikawasilishwa bungeni na serikali kutakiwa kugharamia uanzishwaji wake.

  Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyotolewa na Waziri Bernard Membe kwenye mkutano wa 16 wa Bunge mjini Dodoma Julai 18 mwaka huu, Nyalandu aliahidi kuwasilisha hoja binafsi kwenye mkutano wa 17, kulitaka Bunge kupitisha azimio la kutoruhusu kabisa kujadili masuala ya imani za dini ndani ya Bunge.
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huyu Mheshimiwa Mbunge DATAZ zinasema ni shushushu wa shirika fulani la kijasusi la nje?
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kumbe ''shemeji'' nae huwa anaongea ongea?duh!haya bwana,we wasilisha.

  vipi shemeji hajambo dada?kifaa chako kilikuwa cool sana pale mabibo hostel.hongera
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa si useme tu hayo uliyoyasikia!!!!
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Big up Nyarandu niko na wewe na Mungu akubariki kwa kazi nzuri.
  Najua wabunge wenye nia mbaya watanuna au kuanzisha maneno hovyo hovyo lakini wewe nenda tu songa mbele.:)
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Nami niko nawe kaka kama nilivyo na Nyalandu hakika .
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu,
  Mkuu sema tena unamuunga mkono Nyalandu kwa sababu maswala kama ya OIC na mahakama ya kadhi hayatakiwi kujadiliwa Bungeni!..
  Hivi why nyie jamaa zangu mnakuwa mnajificha ficha na kutokuwa wawazi.. Huyo mbunge mchovu Nyalandu anatakiwa kulieleza bunge madhara ya kuzungumzia maswala ya dini Bungeni! atoe mifano ambayo itasukuma bunge letu lisiweze kujadili maswala ya dini.

  Bunge ndio utawala wa nchi huwezi kusema ati maswala ya dini yasizungumzwe Bungeni.. huu upuuzi mtupu yaani dini ndio inatwala nchi au ni taasisi tu. Bunge litazungumzia kitu chochote kile kinachotakiwa kuzungumziwa iwe hata kazi za rais wa nchi, United Nation, Marekani, Vatican, Iran na kadhalika.

  Huwezi kuliwekea bunge letu mpaka ya utunzi wa sheria au kutazama issue zinazohusiana na nchi yetu ila tutaziwekea dini mipaka ya kuingia Bungeni ba issue zao. Lakini kama Bunge likitaka kutazama jambo lolote linalohusiana na dini fulani litajadiliwa Bungeni, kwani hakuna sehemu ya utunzi wa sheria zaidi ya Bunge, unless mnataka kunambia dini zetu zipo juu ya Bunge na serikali.
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Boss wangu Mkandara mbona umenikaba koo sana kaka hata sipumui kwikwiwi .Nina dada nitakupa uwe shemeji yangu Lo!

  Kaka naunga mkono hoja ya Nyalangu na wewe usimwite mchovu nina private mail yake nikupe umweleze ? The same time anza ku lobby against hoja yale binafsi kaka maana anasema anao 100 wa CCM ndiyo wengi mwisho wa siku watazuia sasa wewe na mimi tunabishana hapa italeta akili kweli ?
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu,
  Hapana mkuu sikufuati isipokuwa nakusoma vizuri... ndio kipaji nilichojaaliwa..
  Sikiliza huyu mbunge mchovu wa kufikiri kabisa.. haelewi nguvu ya Bunge na bunge ni chombo cha aina gani..
  Inapofikia serikali au kiongozi kupiga marufuku BUnge lisizungumzie maswala ya Dini ni sawa kabisa na utawala wa kina Mao Tse Tung na kina Stalin, tofauti inakuwa tu kwamba wananchi wetu wanaruhusiwa kuwa na dini.
  Ni sawa na nchi isiyofungamana na upande wowote wa kisiasa enzi za Cold war kisha unaweka sheria Bunge lisizungumzie maswala ya Ubepari au Ujamaa ila wananchi wanaweza kufuata mkondo wowote..ndipo tulipopata Ukomunist na Ubepari ktk hali mbaya sana.. zamani huwezi kubepa gazeti lolote la kchina ukaingia USA utarudishwa huko ulikotoka na visa itakuwa cancelled pale pale airport..Hii inajenga Uadui zaidi baina ya wahusika wa pande mbili mkifikiria kwamba ndio solution pekee..

  Huu ni UCHOVU wa kufikiri..
  Vyombo vyote vya dini, taasisi na hata mashirika ndivyo vinatakiwa kuwekewa kiwango cha kuhusishwa na serikali.. ktk swala hili vyombo vya dini vinatakiwa kuwekewa vyenyewe sheria aidha iwe kaa ile ya USA inayoitwa Seperation of Churches and states..Hii imetungwa na bunge lao na bunge lilikaa lika face problem zinazotokana na vitu hivi viwili kuwa pamoja..

  Sisi tunaweza kuandika sheria kama hii kulingana na Watu na Mazingira yetu...yaani badala ya kuandika Seperation of Churches ikawa Seperation of Religon and the Government.

  Hii ndiyo nilitegemea kuisikia toka kwa huyo mbunge wenu yaani anapendekeza Kutenganisha baina ya Dini na serikali. Dini kutoingilia mambo ya serikali na serikali kutoingilia mambo ya dini.. Vyombo hivi viwe seperate na havitegemeani kwa jambo lolote. Hivyo sheria inazuia serikali na vyombo vya dini kuwa na uhusiano jambo ambalo sisi sote tunalikubali na hakika ndio kifo cha BAKWATA.. na mpango wa viongozi wa dini kutupangia viongozi wa serikali..
  Lakini hii habari ya kulizuia Bunge lisijadili mambo ya dini..... come on man huu ni udikteta na ufinyu wa kufikiri kwa huyo mbunge na kina Kingunge... Hii inatokana na visa vya OIC, mahakama ya kadhi, MAu na waraka wa kanisa hakuna kingine. Huyu mjinga kapima ni wapi yeye na Kingunge watakutana.. Kingunge akipinga waraka na yeye akipinga mahakama ya kadhi!.

  Lakini ukweli ni kwamba hayo maswala yanaweza kabisa kujadiliwa na solution ikafikiwa aidha kuukubali au kuukataa waraka.. Kukubali mahakama au kukataa mahakama yakadhi.. Hii ndiyo kazi ya Bunge na sii kulizuia Bunge kuzungumzia maswala ya dini ndio maana unaona sasa tunachaguliwa viongozi.

  Haya siku CCM ikiamua kujikita na dini moja iwe Uislaam mtafanya nini?.. maanake Bunge haliruhusiwi kuzungumzia maswala ya dini na JK kaamua kutumia nafasi hiyo mtamfanya nini..na Mkisema for the sake of Natinal security.. mtaambiwa siku zote wale wote walio against the ruling power ndio mnaohatarisha Usalama wa Taifa. Yaani mnaopinga serikali ya JK isijikite ktk Uislaam ndio mnaohatarisha Usalama wa taifa!..

  Hivyo mkuu wangu wabunge kama hawa ni kuwachapa bakora tu! kuna mambo kibao muhimu wamekaa kimyaaa, wakinywa maji, kulala ktk meza lakini inapofikia maswala ya dini utawaona wakiibeba tasbihi (rozali) zao mbele mikononi kubwe ndio Wanafiki wakubwa.
   
  Last edited: Sep 8, 2009
 10. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe Rwakatare, njaa yako itakumaliza. Nashangaa uliwezaje kukaa na kina maalim pamoja na chuki zako kubwa kwa waislam na uislam. Njaa mbaya kaka!
   
 11. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Shughuli Bwana in action!
   
 12. N

  Nanu JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nammunga mkono Lazaro mia kwa mia. Lakini ikumbukwe pia kuwa hata hao wanaoitwa Wabunge nao wana dini pia. Dini ni sehemu ya jamii na nchi yetu. Ila uwekwe utaratibu wa jinsi ya kuwasilisha hoja kama hizo hasa zikiwa zinagusa imani ili kupunguza tension na kukaziana macho...Nadhani ataifremu vizuri na kuisheheni kwa hoja akionyesha utata, matatizo na faida pia. Halafu yapimwe uzito uonekane uko wapi. Ni kweli kuwa swala la udini mara nyingi linapojadiliwa linapandisha jazba nyingi na linakuwa tete....
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haiwezekani kusema katu Bunge lisijadili mambo ya kidini. Let us be practical. Hivi mswaada kama wa Domestic Relations Bill ukiletwa Bunge litafanyaje? Pale kuna mambo ya kidini chungu mzima. Mfano ikitokea kama ya Kibwetere kule Uganda na Gayana miaka ya 1980 kwa imani za kijinga Serikali na Bunge wasitunge sheria ya kudhibiti mambo kama hayo? Kule Nigeria Mahakama za Kadhi zinaamua kesi watu wapigwe mawe kwa sababu ya uzizi serikali inaigilia kati. Kuna mipaka ambayo Serikali/Bunge haviwezi kuepuka kuingilia na dini kuna wakati lazima ziingilie mambo ya serikali au siasa. Tukimpata kichaa kama Idd Amin wa Uganda akaua watu Makanisa na Bakwata wanyamaze? It is impossible for these two to be mutually exclusive.

  Pli kuna hoja inatolewa kwa kutumia Biblia na kunukuu pale Yesu alipowambia Mafarisayo kwamba "wampe Kaisari yaliyo yake na Mungu ya kwake". Kwamba hii inamanisha viongozi wa dini kamwe wasiingilie mambo ya siasa na siasa isiingilie dini. Ni kweli, lakini mimi nadhani hii ni very narrow interpretation ya Biblia. Nothing can be further from the truth. Historia ya Wayahudi na agano lake kuanzia Kitabu cha Waamuzi hadi nabii Malachi ni muingiliano( msigano) mkubwa kati ya viongozi wa kiroho (wakati ule) na watawala.

  In fact the very essence ya manabii (karibu wote) ni msuguano kati yao na watawala yaani wafalme au wanasiasa. Waaamuzi walikuwa kama watawala na wakati huo huo kama viongozi wa kiroho mpaka wakati wa Samueli. Huyu Samueli alimtawaza Mfalme Sauli lakini mfalme Sauli mpaka anapata mauti walikuwa hawaongei! Kwa nini Nabii Elisha (sio Eliya) alimkimbia Malkia Jazeel? Na pale mfalme Daudi alivyokengeuka na kuwa mkatili kwa watu wake Nabii Nathani alimfanya nini? Maisha karibu yote ya Nabii Isaya na Mika yalikuwa ni msigano kati yao na wafalme wa wakati huo. Nabii Jeremia ni tokeo la ukatili mbaya wa Mfalme Manase aliyewapotosha wayahudi. Ezikiel alitupwa kisimani (akaokolewa na M-Ethiopia) kwa kumwambia mfalme Joacina ukweli. Nani asiyejua kifo cha Yohana Mbatizaji kilitokana na nini?

  Ufasadi na uchoyo wa kupitiliza kama tulionao sasa ni dhambi. Kanisa au misikiti ikiona madhambi na ikanyamaza kwa kuogopa kiungilia mambo ya siasa havitimizi wajibu wao kimungu. Nafasi haitoshi hapa. Lakini chimbuko la waraka ni malalamiko ya watu kuhusu ufisadi na dhuluma mbali mbali zinazofanywa na viongozi wetu au kwa baraka zao. Sasa tufanyeje? Kanisa likasema njia mbadala ni hizi: CHAGUENI VIONGOZI KWA KUTUMIA VIGEZO HIVI KUPATA VIONGOZI BORA SIO BORA VIONGOZI. Is this poking the nose too much into politics?
   
 14. K

  Kagoma Member

  #14
  Sep 8, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ByaseL has a point.
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sawa Mkuu kwa kutaka tuwe na BUNGE POWA! lisiwe na mikiki yoyote kwani kina Nyalandu hawawezi kuwa na hoja za kuzuia mikiki inayolistahiki bunge.
  Hivyo unaposema kitu fulani kisifanywe Bungeni na huku hujakipangia utaratibu wa kukishughulikia huko nje una maana gani? Hivyo masuala yasiyo na utaratibu ndani ya Katiba yanapotokea yanashughulikiwa na nani? Nani anaepanga katiba zaidi ya Bunge na unapoliziba mdomo nini matokeo yake.
  Inasikitisha sana kuwa na Wabunge wasioona mbele zaidi ya matumbo yao yanayoshibisha na jasho la wanajamii.
  Nitasema mengi hapo iwapo Mhe Sitta ataruhusu UBAKAJI wa demokrasia unaotaka kufanywa na Nyalandu lakini kwa sasa tu nafikiri ile DUWA ya kumtaja Mungu kule Bungeni itabidi isitishwe ili kumuunga mkono Mheshimiwa Nyalandu kwani dini zimeletwa na Mungu na huwezi kukataa dini na huku ukimtaja Mungu1
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Dini zimeletwa na wazungu na waarabu . Hakuna ushahidi wa Mungu kuleta dini Afrika . Kama upo naomba umwagwe hapa .
   
 17. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Lazima bunge lijadiri ishu yoyote ile ya kidini au vinginevyo, isipokuwa lisijihusishe na uanzishwaji wa taasisi yoyote ya kidini, iwe mahakama ya kidini, kujiunga na kundi lolote kama taifa kwa misingi ya dini. Kama dini zinataka kuanzisha mambo yao basi ziachiwe zenyewe na bunge/serikali isijihusishe na uanzishwaji huo.
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya ni maajabu. Mbunge ambaye miaka yote amekuwa kuwadi wa Wakristo wenye Siasa Kali wa MAREKANI (right wing evengelicals) na wanausalama wa ISRAEL na maslahi yao ya kizayuni hapa nchini leo hii awe mpinga udini bungeni.

  Huyu si ndiye mwenye utamaduni wa kufanya utafiti wa wabunge wangapi ni waislamu na wangapi ni wakristo kwa kutimia note book yake kunote wanavyokula viapo vyao na hata kutumia nafasi yake bungeni kutuma michango ya baadhi ya wabunge kwa mabosi zake huko nje ambao wanamjengea visima na mambo mengine jimboni kwake.

  Anaposema wabunge 100 inawezekana wakawepo lakini kamwe hakuna Mbunge muislamu anayemjua LAZARO NYALANDU mlokole aliyegubikwa na chuki dhidi ya UISLAMU hadi kufikia kuwasingizia waislamu wanataka kuwazuia wanawake kuendesha magari hapa Tanzania kwa kutolea mfano wa Saudi Arabia, atakayekuwa tayari kumuunga mkono hoja yake yoyote ile.

  Mwisho wa siku huyu jamaa ndiye atayepiga mstari na kuhalalisha siasa za UDINI ambazo zitakuwa mwanzo wa kura za udini zitakazopigwa 2010. Naziona zinakuja.....na ni hawa wanasiasa wa aina ya Nyalandu ndio watakuwa wasadifu na watekelezaji wake...

  Kama angekuwa anataka kuzuia udini basi angepiga marufuku kuanzia wabunge na rais kula kiapo kwa biblia ama msahafu, kuondoa dua ya bunge yenye kumtukuza mungu, kuacha kuendesha vikao vya mtandao wao wa walokole hapo bungeni, kutumia shughuli za kidini kuongelea masuala ya siasa, kuharamisha mikataba ya aina yoyote kati ya serikali na makundi ya kidini, kuzuia vitendo vya makanisa na misikiti kutoa maelekezo ya kisiasa na kadhalika. Mambo ambayo ndiyo yeletayo udini na sio mjadala wa kukubali ama kutokubali MAHAKAMA YA KADHI na OIC TU.

  Na kwanini ahitaji baraka za KINGUNGE na MAKAMBA wakati yake ni hoja ambayo itapaswa kujadiliwa. Ama angependa kwenda mbele zaidi hadi kuzuia wenye kupingana na hoja zake wasiwe na haki ya kuchangia?

  omarilyas
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Whaaat?
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Bwana Mkubwa upo pamoja nasi au pumzi ulizopewa ndio zinakupa kedi?
  Hata hivyo mada ni bunge na hoja ya Nyalanda na ikiwa huna mchango hakuna atakaejali kwa wewe kutokuwa na mchango kwa mada hii.
   
Loading...