Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

CCM kama taasisi haina tatizo, na vigezo vya kuanzishwa kwake ni vizuri tu, tena kuliko vigezo vya vyama kadhaa vya upinzani. Tatizo ni kwamba kuna watu ndani ya CCM ambao wanapindisha melongo mazuri ya CCM. Hili ndilo tunataka CCM ilitanbue na kutokukubali kuwa na watu wa namna hiyo.

Chachu ya maendeleo ya Tanzania ni pamoja kuwa na CCM na UKAWA vyenye nguvu. Kimoja kikiwa na nguvu sana zaidi ya kingine haitatusaidia mimi na wewe na mwananchi wa kawaida. Mara ngapi umesikia au kuona CCM wakipitisha utumbo kule Bungeni kwa kuwa tu wao ni wengi kuloko wabunge wa upinzani? Sasa hilo si nzuri kwa CCM, na haliwezi kuwa zuri kwa UKAWA kuwa na nguvu ya namna hiyo pia.

Upo pamoja na mimi sema kwa maelezo yaliyotofautiana kidogo.Sitaki ife bali ivunjike vunjike ili tupate CCM iliyobora zaidi yaani katika ubora wake na tukiwa na ukawa katika ubora wake lazima tutafika tunakoenda...

Tunahitaji viongozi watakoionea HURUMA nchi yetu,wazalendo,wakweli kwao wenyewe na kwa jamii watakayoiongoza,hatuhitaji tena mafisadi,wanaotembea na pesa kwa ajili ya kupata uongozi.

Kwa sasa ili CCM iwe na nguvu basi lazima ivunjike vipande vipande na muda wake ndiyo huu.............Hata kikombe ukipendacho kikifika muda wake kitavunjika tu.............
 
Kingunge ana njaa na anatafuta kuponya njaa yake kama Lowassa akipitishwa. Huyo anajua atapewa sehemu afanye biashara ili atengeze. Kwani mmesahau ni CCM haohao walimpa UNBINGO BUS TERMINAL kukusanya viingilio? Labda ana hasira na kunywang'anywa Ubungo sasa anajua Lowassa akiingia atapata uaji mwingine.
 
Kwa sasa siasa ndani za CCM ni za kimakundi kila mtu na utashi wake kwa Mgombea amtakaye mie nawashangaa sana kumwona mzee Kingunge kakosea,kakosea lipi???

Mbona akina mzee John Malichela na Chleopa Msuya wamejibainisha wazi wao wako kinyume na Lowassa na wanamuunga mkono Membe bila kificho hao mnawaona wako sahihi???
Acheni unafiki uliopindukia,Lowassa amewanyima usingizi mtakoma mwaka huu.
Na asiiyemtaka Lowassa ahame CCM ama akale malimao.
 
Ambaye hataki lowassa awe rais wa nchi hii ni bora akakimbia nchi mapema kwasababu ndio rais ajae, hata J.K. alipokuwa anaingia walisema ivo, ivo, mara ooh J.K. akichukua tunahama nchi lakini mpaka leo wamo humu humu. sasa kauli zile leo wameanza kwa lowassa, mara ooh, fisadi. sasa ndowa Tanzania wanamtaka huyo huyo, kama ilivyokuwa kwa J.K.

HABARI NDO HIYO.
 
Nawaheshimu sana wazee, maana wazazi wangu wamepitia hatua hiyo, na mie najua nitapitia, Mungu akibariki. Hata hivyo ni ukweli usiofichika kwamba ule msemo "kuna watu wanazeeka vibaya" unakuwa kweli sana ninapochunguza kauli za Kingunge kuhusu uteuzi wa CCM wa mgombea uraisi.

Nimeshindwa kabisa kumwelewa mzee huyu, na ninachoweza kusema ni kwamba pengine Kingunge anazeeka vibaya.

Wengi tunajua Kingunge, licha ya kuwa kiongozi wa CCM, ni kiongozi wa "kitaifa", na katika hili amejijengea heshima kubwa kwa muda mrefu. Ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini huyu mzee ameamua kuiweka heshima yake rehani kwa kuwa msemaji wa kambi ya Lowassa?

Mie nilitarajia Kingunge angekuwa muwakilishi na mshauri wa wagombea wote wa CCM, badala ya kujikita katika kambi moja tu ya Lowassa, ukizingatia historia yake Kingunge katika uongozi wa CCM na kitaifa. Hivi amewaza nini huyu mzee na kuamua kuwa sambamba na Lowassa?

Na mbaya zaidi, kwa namna moja au nyingine ameamua kuendeleza ule mkakati wa kuishinikiza na kuitishia nyau CCM ili kumteua Lowassa kama mgombea wao wa uraisi. Amefikia kudiriki kuonyesha kwamba CCM wasipomteua Lowassa basi CCM itafia awamu ya nne! Hivi Kingunge haelewi kwamba lolote analolisema sasa, ushauri au maonyo yeyote anayoyatoa hadi sasa kuhusu CCM watu wote wenye akili wanaona kabisa yanalenga kumsaidia mgombea wake aliyeamua kwa sababu anazozifahamu yeye, kupalilia njia ya kuelekea hiyo inayosemwa safari ya matumaini?

Lowassa amemuahidi nini Kingunge hadi mzee wa watu aamue kujishusha hadhi kisiasa kwa kiasi hiki?

Watu wote wenye akili wangeona labda Kingunge anaongea jambo la maana ikiwa angesema haya anayosema dhidi ya CCM bila kuwa amejiweka kambi ya mgombea mmojawapo wa CCM, Lowassa. Kinyume cha hapo ni kwamba Kingunge anadhani viongozi wa CCM wana upeo mdogo sana wa kufikiri na kutambua anachofanya, kwamba anatumiwa na Lowassa kuishinikiza CCM. Sidhani kama mbinu hii itamsaidia Lowassa au Kingunge mwenyewe.

Anachofanya Kingunge ni usaliti wa kiwango cha juu kwa CCM, na CCM inapaswa kutambua hilo. Kingunge anataka kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM ili tu amnufaishe Lowassa. Ameamua kwamba liwe na liwalo, the end justifies the means. Kama JK bado hajamuita Kingunge na kumweka sawa bila kumuonea aibu, basi ningeshauri JK afanye hivyo haraka sana, kabla huyu mzee hajawaharibia CCM hata zaidi.

Ushauri wangu kwa Kingunge ni kwamba baada ya haya yote uliyofanya, makosa makubwa sana ya kisiasa, nenda kijijini ukakae kimya huko na kuwa mjamaa halisi, kama ambavyo siku zote ulijionyesha kwa Nyerere, kwamba wewe ni zaidi ya mjamaa.
Kingunge : mmoja kati ya wanasiasa wakongwe wanafiki ambao sijapata kuona.
Aliwahi kuwa mjamaa hadi kuiponda dini yake, kisa ni kumfurahisha Nyerere.
Ndiye alikuwa msemaji mkuu wa itikadi ya kijamaa ndani ya chama.
Baada tu ya kifo cha Mwalimu kilichobaki kichwani kwake ni kung'ang'ania nafasi ndani ya chama naserikali ili kujinufaisha kibinafsi.
T
Leo anakusanya kodi kwa ajili ya wananchi , na anaila yeye na familia yake.
Aliumbuliwa na CAG pale Ubungo baada ya kudhihirika kuwa ANAIBA!!!
Leo vile vile Kingunge ni swahiba mkubwa wa mafisadi na HANA UHALALI WOWOTE wa kutueleza itikadi au misimamo ya chama.
Kingunge ni mwizi tu, full stop.
mkuu tulishasema, huyo mganga wa kienyeji alishashindikana!
 
Ndio maana mfalme Daudi alisema, ukiwa na Bwana unakiwa na hekima kuliko hata wazee, na akili kuliko wakufunzi(Zaburi 119:97-101), sasa mganga wa kienyeji unategemea awe na hekima? Hekima inatoka katika vibuyu vyake vya kazi? Hana hekima kwa kuwa alishaamua kuachana na chanzo cha hekima(Mungu) na akaamua kujiungamanisha na vibuyu(mungu).
 
Nawaheshimu sana wazee, maana wazazi wangu wamepitia hatua hiyo, na mie najua nitapitia, Mungu akibariki. Hata hivyo ni ukweli usiofichika kwamba ule msemo "kuna watu wanazeeka vibaya" unakuwa kweli sana ninapochunguza kauli za Kingunge kuhusu uteuzi wa CCM wa mgombea uraisi.

Nimeshindwa kabisa kumwelewa mzee huyu, na ninachoweza kusema ni kwamba pengine Kingunge anazeeka vibaya.

Wengi tunajua Kingunge, licha ya kuwa kiongozi wa CCM, ni kiongozi wa "kitaifa", na katika hili amejijengea heshima kubwa kwa muda mrefu. Ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini huyu mzee ameamua kuiweka heshima yake rehani kwa kuwa msemaji wa kambi ya Lowassa?

Mie nilitarajia Kingunge angekuwa muwakilishi na mshauri wa wagombea wote wa CCM, badala ya kujikita katika kambi moja tu ya Lowassa, ukizingatia historia yake Kingunge katika uongozi wa CCM na kitaifa. Hivi amewaza nini huyu mzee na kuamua kuwa sambamba na Lowassa?

Na mbaya zaidi, kwa namna moja au nyingine ameamua kuendeleza ule mkakati wa kuishinikiza na kuitishia nyau CCM ili kumteua Lowassa kama mgombea wao wa uraisi. Amefikia kudiriki kuonyesha kwamba CCM wasipomteua Lowassa basi CCM itafia awamu ya nne! Hivi Kingunge haelewi kwamba lolote analolisema sasa, ushauri au maonyo yeyote anayoyatoa hadi sasa kuhusu CCM watu wote wenye akili wanaona kabisa yanalenga kumsaidia mgombea wake aliyeamua kwa sababu anazozifahamu yeye, kupalilia njia ya kuelekea hiyo inayosemwa safari ya matumaini?

Lowassa amemuahidi nini Kingunge hadi mzee wa watu aamue kujishusha hadhi kisiasa kwa kiasi hiki?

Watu wote wenye akili wangeona labda Kingunge anaongea jambo la maana ikiwa angesema haya anayosema dhidi ya CCM bila kuwa amejiweka kambi ya mgombea mmojawapo wa CCM, Lowassa. Kinyume cha hapo ni kwamba Kingunge anadhani viongozi wa CCM wana upeo mdogo sana wa kufikiri na kutambua anachofanya, kwamba anatumiwa na Lowassa kuishinikiza CCM. Sidhani kama mbinu hii itamsaidia Lowassa au Kingunge mwenyewe.

Anachofanya Kingunge ni usaliti wa kiwango cha juu kwa CCM, na CCM inapaswa kutambua hilo. Kingunge anataka kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM ili tu amnufaishe Lowassa. Ameamua kwamba liwe na liwalo, the end justifies the means. Kama JK bado hajamuita Kingunge na kumweka sawa bila kumuonea aibu, basi ningeshauri JK afanye hivyo haraka sana, kabla huyu mzee hajawaharibia CCM hata zaidi.

Ushauri wangu kwa Kingunge ni kwamba baada ya haya yote uliyofanya, makosa makubwa sana ya kisiasa, nenda kijijini ukakae kimya huko na kuwa mjamaa halisi, kama ambavyo siku zote ulijionyesha kwa Nyerere, kwamba wewe ni zaidi ya mjamaa.
Mzee alichelewa kutafuta pesa sasa kaijulia pesa uzeeni hata busara zinamtoka. Ukimtetea fisadi lazima nawe uwe fisadi
 
Ambaye hataki lowassa awe rais wa nchi hii ni bora akakimbia nchi mapema kwasababu ndio rais ajae, hata J.K. alipokuwa anaingia walisema ivo, ivo, mara ooh J.K. akichukua tunahama nchi lakini mpaka leo wamo humu humu. sasa kauli zile leo wameanza kwa lowassa, mara ooh, fisadi. sasa ndowa Tanzania wanamtaka huyo huyo, kama ilivyokuwa kwa J.K.

HABARI NDO HIYO.

Na anayetamani Lowassa awe Rais afanyeje pale Lowassa akikosa Urais?
 
Kingunge anajua analolifanya. Tunajua amesimama na anahesabiwa upande wa Lowasa. Je mlitaka awadanganye? Tuombe tuwepo July 12, 2015. Maamuzi yatafanyika na CCM itapata stahili yao kwa umoja wao. Na baadae Tanzania tutapata stahili yetu kwa umoja wetu.
 
Kwa sasa siasa ndani za CCM ni za kimakundi kila mtu na utashi wake kwa Mgombea amtakaye mie nawashangaa sana kumwona mzee Kingunge kakosea,kakosea lipi???

Mbona akina mzee John Malichela na Chleopa Msuya wamejibainisha wazi wao wako kinyume na Lowassa na wanamuunga mkono Membe bila kificho hao mnawaona wako sahihi???
Acheni unafiki uliopindukia,Lowassa amewanyima usingizi mtakoma mwaka huu.
Na asiiyemtaka Lowassa ahame CCM ama akale malimao.

Mkuu, sikatai walivyofanya kina Malechela na Msuya, lakini namna anayofanya Kingunge ni tofauti sana. Yeye ana toa shinikizo kwa CCM ili imteue Lowassa. Inabidi uangalie kwa makini anayosema Kingunge ili kuelewa yale anayofanya.

Hata hivyo, suala la kina Malechela na Msuya kufanya hivyo nalo ni kosa. Mie nilishawahi kutamka humu JF kwamba viongozi wa CCM, hasa wale ambao bado wako madarakani, ni makosa kutoa matamko ya kuwaunga mkono wagombea, kwa sababu kwa kufanya hivyo wanahujumu (undermine) mchakato wa uteuzi ndani ya chama. Hamna tofauti na ile sheria inayokataza kujadili kesi wakati kesi iko mahakamani.

Pengine wagombea wanaweza kuungana mkono, ikibidi, lakini leo Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya wanapojitokeza na kuunga mkono mgombea fulani inaleta picha gani kama sio migawanyiko isiyo ya lazima ndani ya chama? Wewe ukiwa mgombea na kujua kabisa waziri au mkuu wa mkoa fulani hakukuunga mkono na alimuunga mkono mpinzani wako, utafanyaje ukisha kuwa raisi?

Mie ningekuwa mgombea nikapitishwa kuwa mwenyekiti wa chama na raisi, huyu Kingunge hata salamu ya Mwanyekiti wa Kitongoji wa CCM huko anakokaa asingeipata, kwa kuchochea mgongano ndani ya chama! NIngewaambia waachane naye kabisa!
 
Mkuu, sikatai walivyofanya kina Malechela na Msuya, lakini namna anayofanya Kingunge ni tofauti sana. Yeye ana toa shinikizo kwa CCM ili imteue Lowassa. Inabidi aungale kwa makini anayosema KIngunge ili kuelewa yale anayofanya.

Hata hivyo, suala la kina Malechela na Msuya kufanya hivyo nalo ni kosa. Mie nilishawahi kutamka humu JF kwamba viongozi wa CCM, has wale ambao bado wako madarakani, ni makosa kutoa matamko ya kuwaunga mkono wagombea, kwa sababu kwa kufanya hivyo wanahujumu (undermine) mchakato wa uteuzi ndani ya chama. Hamna tofauti na ile sheria inayokataza kujadili kesi wakati kesi iko mahakamani.

Pengine wagombea wanaweza kuungana mkono, ikibidi, lakini leo Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Wilaya anapojitokeza na kuunga Mkono mgombea fulani inaleta picha gani kama sio migawanyiko isiyo ya lazima? Wewe ukiwa mgombea na kujua kabisa waziri au mkuu wa mkoa fulani hakukuunga mkono na alimuunga mkono mpinzani wako, utafanyaje ukisha kuwa raisi?

Mie ningekuwa mgombea nikapitishwa kuwa mwenyekiti wa chama na raisi, huyu Kingunge hata salamu ya Mwanyekiti wa Kitongoji wa CCM huko anakokaa asingeipata, kwa kuchochea mgongano ndani ya chama! NIngewaambia waachane naye kabisa!

kingunge hashinikizi uteuzi wa Lowassa ila anahitaji haki kutendeka kwa kuzingatia kura za maoni na sio kupitia maamuzi ya wachache wanaoamini katika kukata jina ili kumwondoa ulingoni,tatizo tunapenda kudanganywa tu lazima ukweli usemwe wazi na kuikosoa ccm sio dhambi ila mzee anakumbusha palipo dhaifu,hivo Lowassa aparekebishe.
TEAM lowassa
 
Last edited by a moderator:
Kada maarufu wa CCM,mzee Kingunge, amesema hawatakubali kuona jina la Lowassa linakatwa.

=============================

Chanzo: Mwananchi

Comment
-------
11. (C) While the immediate reason for PM Lowassa tendering
his resignation was his implication in the illegal
procurement of the energy contract with Richmond, Lowassa's
corrupt activities have been an open secret throughout
Tanzania for many years. In addition, rumors of a cabinet
shake-up had been rampant since the conclusion of the CCM's
Party Congress on November 5, 2007. As a result of CCM
elections for the party's National Executive Committee,
several of President Kikwete's close circle took on new roles
in the party. Other CCM stalwarts were moved to "lower"
positions, indicating that Kikwete was maneuvering to
distance himself from ministers and others with reputations
for lining their pockets.

12. (C) In January 2007, testing the waters of high-level
political will to fight corruption, the DCM had asked Edward
Hosea, head of the PCCB, if Kikwete was sincere about
battling graft (Ref A). Hosea replied he believed the
President Kikwete to be honest, but "the test will be whether
he is ready to go after the big fish." Ironically, the
Parliamentary Committee report has also condemned Hosea for
allowing PCCB to whitewash its own Richmond investigation.
It remains to be seen if in Kikwete's upcoming Cabinet
announcements, Hosea, whose PCCB is directly under the

DAR ES SAL 00000098 004.2 OF 004

President's Office, retains his position or not. In any
case, President Kikwete is facing a critical crossroads in
selecting his cabinet. He appears to have chosen a
well-respected Parliamentarian as his new Prime Minister.
Through his selection of his other ministers and deputies,
Kikwete will craft the message he wants to send on
corruption, not only to his government and the 82 percent of
the electorate who put him into office in December 2005, but
to all of Africa.

13. (C) Kikwete's January 31 election as Chair of the African
Union (AU) has thrust him into a central role with
expectations that he will assist in resolving crises from
Kenya to Chad to Zimbabwe. In anticipation that he may spend
a lot of time "on the road" this next year trouble shooting
for the AU, we presume Kikwete's goal would be put in place
not only a reliable and honest PM, but to surround himself
with capable ministers who could keep the Government on
course when he is away.
 
Kingunge anajua analolifanya. Tunajua amesimama na anahesabiwa upande wa Lowasa. Je mlitaka awadanganye? Tuombe tuwepo July 12, 2015. Maamuzi yatafanyika na CCM itapata stahili yao kwa umoja wao. Na baadae Tanzania tutapata stahili yetu kwa umoja wetu.

Mkuu tunaomba utuelewe. Kingunge anaweza kumuunga mkono Lowassa, japo sio busara kufanya hivyo. Lakini kikubwa kibaya anachofanya Kingunge ni kuanza kuikosoa CCM katika mambo anayojua yanaweza kufanya mtu wake asipitishwe, na kwa namna moja kutia shinikizo kwa CCM ili imputishe Lowassa.

Hebu angalia taarifa hii hapa chini kutoka gazeti moja hapa nchini uniambe kama kweli ni busara kwa kiongozi kama Kingunge kutamka maneno haya, katika mazingira ya kumuunga mkono Lowassa. Haya ni mambo ambayo hayafai kusemwa wakati umeshajidhihirisha unamuunga mkono mgombea fulani;

-Atahadharisha uteuzi wagombea Urais CCM
-Si mchezo wa kuchezwa na kila mtu

Alisema wanaofanya jitihada za kuunda mazingira ya kukitafutia chama kushindwa, wanataka historia ya CCM iishie katika awamu ya nne.

Alisema ni mwiko kumhukumu mtu kabla ya vikao kwani haijawahi kufanywa hivyo mwaka 1995 na 2005, na hawatafanya hivyo mwaka huu "Wakifanya hivyo tutakataa, tunataka mchakato ufuate taratibu zilizowekwa, nimemsikia kiongozi wetu mmoja alizungumzia katika Tv kuwa mtu hawezi kwenda kujinadi yeye binafsi bali chama ndio kinamnadi...Mimi nataka niseme kuna ngazi mbili; mwanachama anatakiwa kujinadi ndani ya chama na ndiyo tumefanya hivyo miaka yote kwa mujibu wa taratibu na ndivyo wanavyofanya kina Lowassa, anajinadi kwa wanachama," alisema.

"Katika utaratibu wetu tuna misingi ya kuamua na mwenyekiti wa chama chetu, Jakaya Kikwete, alitangaza yeye mwenyewe kwamba tutafute mgombea anayekubalika ndani na nje ya chama na ndio msimamo wa chama...CCM inamtafuta mtu anayekubalika ili kuleta ushindi ndani ya chama, wale wanaojitahidi kufanya hivyo kukitafutia chama kushindwa wanataka historia ya Chama Cha Mapinduzi iishie katika awamu ya nne," alitahadharisha.

Alisema suala la urais lisifanyiwe mizengwe, watu waulizwe wanamtaka nani na nani atakayewatatulia changamoto zao.

"Watu wenye busara wanafuatilia mambo yanavyoenda na wameona, wagombea wapo wengi, wenye macho wapo wengi na wanaona, hivyo watu watulize vichwa na kuamua ni nani watamchagua," alisema Kingunge.
 
Kata hao wengine lkn siyo lowasa

Ndio maana wanaotaka lowasa awe rais marazote huwa hawana sababu zozote za msingi na hapo ndipo nguvu ya pesa inapojidhihirisha.
Mtaji wa lowasa ni masini wa aina tatu
1. Masikini wa kipato
2. Masikini wa akili (elimu ndogo)
3. Masikini wa taarifa zinazomhusu lowasa

WEWE UKO KUNDI GANI?
 
Mungu akubariki Kingunge, na uzidi kuishi miaka elfu na kenda...!!!

Na hakika CCM haiwezi mchagua mwingine zaidi ya Lowassa...!!!
 
Mkuu, sikatai walivyofanya kina Malechela na Msuya, lakini namna anayofanya Kingunge ni tofauti sana. Yeye ana toa shinikizo kwa CCM ili imteue Lowassa. Inabidi uangalie kwa makini anayosema Kingunge ili kuelewa yale anayofanya.

Hata hivyo, suala la kina Malechela na Msuya kufanya hivyo nalo ni kosa. Mie nilishawahi kutamka humu JF kwamba viongozi wa CCM, hasa wale ambao bado wako madarakani, ni makosa kutoa matamko ya kuwaunga mkono wagombea, kwa sababu kwa kufanya hivyo wanahujumu (undermine) mchakato wa uteuzi ndani ya chama. Hamna tofauti na ile sheria inayokataza kujadili kesi wakati kesi iko mahakamani.

Pengine wagombea wanaweza kuungana mkono, ikibidi, lakini leo Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya wanapojitokeza na kuunga mkono mgombea fulani inaleta picha gani kama sio migawanyiko isiyo ya lazima ndani ya chama? Wewe ukiwa mgombea na kujua kabisa waziri au mkuu wa mkoa fulani hakukuunga mkono na alimuunga mkono mpinzani wako, utafanyaje ukisha kuwa raisi?

Mie ningekuwa mgombea nikapitishwa kuwa mwenyekiti wa chama na raisi, huyu Kingunge hata salamu ya Mwanyekiti wa Kitongoji wa CCM huko anakokaa asingeipata, kwa kuchochea mgongano ndani ya chama! NIngewaambia waachane naye kabisa!

Tofauti ya Mzee kingunge na S J Malecela pamoja na C.Msuya ni:-
Kigunge alihutubia kusanyiko kubwa AKIWA AMESIMAMA na wenzake anaongea WAKIWA WAMEKAA KWENYE VITI.
Lengo Kingunge ni kuhakiki kuna kuwa FAIR PLAY kwa mgombea wote ili kila mtaka Urais apenye kwa halali kupeperusha bendera ya CCM.
 
Ndio maana wanaotaka lowasa awe rais marazote huwa hawana sababu zozote za msingi na hapo ndipo nguvu ya pesa inapojidhihirisha.
Mtaji wa lowasa ni masini wa aina tatu
1. Masikini wa kipato
2. Masikini wa akili (elimu ndogo)
3. Masikini wa taarifa zinazomhusu lowasa

WEWE UKO KUNDI GANI?

Wewe sema uko lipi hapo ndio yeye aseme Maembe wewe
 
kingunge hashinikizi uteuzi wa Lowassa ila anahitaji haki kutendeka kwa kuzingatia kura za maoni na sio kupitia maamuzi ya wachache wanaoamini katika kukata jina ili kumwondoa ulingoni,tatizo tunapenda kudanganywa tu lazima ukweli usemwe wazi na kuikosoa ccm sio dhambi ila mzee anakumbusha palipo dhaifu,hivo Lowassa aparekebishe.
TEAM lowassa
Acha fix wewe! Hiki kigagula cha kiume kilim-endorse fisadi laivi pale Sheikh Amri Abeid!
Utakuwa hukufuatilia ule mkutano!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom