King'amuzi cha Azam cha Antenna mlonunua tupeni mrejesho

Wakati mwingine sio utajiri ni ujanja tu, mimi naangalia ligi zote za mpira ulimwenguni, tennis, mbio za magari, baiskeli, mieleka ya WWE naiona live wakati nyie mnasubiri recorded ya miezi 6 baadae, muvi mpya, discovery , national geographic...zote HD na 4K....mahojiano ya Oprah na Prince Harry na Meghan kupita CBS ambayo wabongo wenzangu mtayaona mwakani (lol). Habari naangalia cnn, fox,abc, nbc, aljazeera .. yote hayo kwa chini ya sh elfu 5(tano) kwa mwezi....
Interesting....
 
Nje ya mada wadau . nataka kuongeza king'amuzi cha azam . je naweza kutumia dishi la sasa la DSTV . nikimaanisha dishi DSTV ila king'amuzi azam
 
Wakati mwingine sio utajiri ni ujanja tu, mimi naangalia ligi zote za mpira ulimwenguni, tennis, mbio za magari, baiskeli, mieleka ya WWE naiona live wakati nyie mnasubiri recorded ya miezi 6 baadae, muvi mpya, discovery , national geographic...zote HD na 4K....mahojiano ya Oprah na Prince Harry na Meghan kupita CBS ambayo wabongo wenzangu mtayaona mwakani (lol). Habari naangalia cnn, fox,abc, nbc, aljazeera .. yote hayo kwa chini ya sh elfu 5(tano) kwa mwezi....
Tupeane huu ujanja mkuu
 
Tupeane huu ujanja mkuu
Hapa JF kuna jukwaa la teknolojia kuna uzi mmoja wa haya mambo yanaongelewa sana, sema wengi wa wachangiaji ni majirani zetu ambao hawafyatuki kama wabongo, wanaongea kwa code hadi uwaelewe inabidi kutumia bongo....kwa kifupi haya mambo yapo wazi tu
 
Azam walianza vizuri sana ila sasa nataka nikigawe king'amuzi chao,yaani channels kibao wamezitoa ,hakuna Nigeria movie AMC /Star etc zote wameondoa ,Fox hakuna , Fine living,E! Ent wameondoa yaani full utopolo.
 
Back
Top Bottom