#COVID19 Kinga ya Corona isiyothibitishwa na wataalam hii hapa

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kulingana na uzoefu tulioupata kutoka mwaka jana hadi Sasa tunaweza kusema dawa ya Corona amabayo haijathibitishwa na wataalam wa afya ila inasaidia ni hii hapa;

1. Corona inatibika kwa kumwamini Mungu. Binadamu siku zote anaogopa mauti kumkuta akiwa hayupo kwenye mahusiano mazuri na Mungu. Endapo mwanadamu atajiridhisha kwamba yupo kwenye mahusiano mazuri na Mungu hofu ya kifo upungua na kinga ya mwili uimarika. Hivyo kinga namba moja ya corona nikujiweka karibu na Mwenyenzi Mungu ili mapenzi yake yatakapotimia basi uwe na uhakika wakuishi katika mikono yake.

2. Kuchukua taadhari ya afya kwa kunawa, kuvaa barakoa, kupunguza mikusanyiko nk. Pale imani yako inapoimarika ndipo unapokuja kutumia maarifa ya kibinadamu kujikinga na Corona. Usipotoshe bali waruhusu waliokuzunguka kutumia akili zao kujikinga na Corona kwani ugonjwa uangaika na nafsi binafsi siyo nafsi za wengi.

3. Bila kujali ukubwa wako kwenye familia au madaraka yako kwenye Taifa, usipotoshe. Namna unavyotengeneza habari usizoziamini ndivyo unavyojiweka mbali na Mungu kwa sababu unajua wazi unamdanganya, lakini pia ndivyo unavyoacha kuchukua taadhari na mwisho hata kama wewe utaendelea kuchukua taadhari kwakificho basi nafsi za watu waliokusikiliza na kukuamini zitazidi kuugua na wengi watapoteza maisha mbele ya maneno na amri yako.

Hivyo dawa yetu inaundwa na;

IMANI JUU YA MWISHO MWEMA+ TAADHARI- UPOTOSHAJI AIDHA UNAOTOKANA NA MADARAKA AU NAFASI YAKO KWENYE JAMII.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom