Kinana - Wasaka Majimbo Kinyemela Kubanwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameziagiza kamati za siasa za CCM, kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wanachama walioanza kupitapita kusaka ubunge na udiwani.

Amesema wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, utaratibu na miongozo ya uchaguzi ndani ya CCM na watakaobainika hawatapitishwa na vikao vya maamuzi kugombea nafasi hizo, hata kama wataongoza katika kura za maoni.

Kinana ameyasema hayo tarehe 05 Septemba, 2023, Wilayani Hai, Kilimanjaro katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Hai uliohusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, jimboni humo.

Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Hai ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe ambaye alipata nafasi ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 tangu 2020 -2023

“Nataka nitumie fursa hii kuziagiza kamati za siasa za CCM nchi nzima, zikisaidiwa na kamati za maadili nchi nzima, kuwafuatilia wale ambao wameanza kuzungukazunguka kutafuta ubunge, udiwani, uenyekiti wa mtaa au kitongoji kuanzia sasa,” ameagiza Makamu Mwenyekiti na kuongeza:

“Hatuna nafasi ya kuhangaishwa na watu wanaotafuta uongozi kipindi hiki, wasubiri hadi mwezi wa saba mwaka 2025, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itaamua tarehe ya kwenda kuchukua fomu, kabla ya hapo unavunja kanuni".

Amesema mwana CCM asifikiri kwamba akianza kampeni kabla ya wakati, akapigiwa kura akawa wa kwanza, atapitishwa kugombea, hapana, hatapita.

"...alianza kampeni mapema, alitoa rushwa, alikivuruga Chama, hata upate kura za wajumbe wote hutapita," ameonya Ndugu Kinana.

Amebainisha kwamba, kuna vigezo vingi vinatazamwa zikiwamo; kura, uzingatiaji wa maadili na kanuni.

"Je, ulitoa rushwa, ulizingatia kanuni, uliwachafua viongozi wenzako walioko madarakani? Kwa hiyo unaweza ukawa wa kwanza lakini ukawa wa mwisho,” ametahadharisha.

Aidha, amewataka wanaccm wote kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ambao wana wajibu wa kutekeleza ahadi zilizotolewa na Chama kwa Watanzania.

WhatsApp Image 2023-09-06 at 00.02.11.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-06 at 00.02.10(1).jpeg
F5VK6NTXYAAFJTr.jpg
WhatsApp Image 2023-09-06 at 00.02.15(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-06 at 00.02.15.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-06 at 00.02.13(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-06 at 00.02.09.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-06 at 00.01.47.jpeg
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameziagiza kamati za siasa za CCM, kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wanachama walioanza kupitapita kusaka ubunge na udiwani.

Amesema wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, utaratibu na miongozo ya uchaguzi ndani ya CCM na watakaobainika hawatapitishwa na vikao vya maamuzi kugombea nafasi hizo, hata kama wataongoza katika kura za maoni.

Kinana ameyasema hayo tarehe 05 Septemba, 2023, Wilayani Hai, Kilimanjaro katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Hai uliohusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, jimboni humo.

Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Hai ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe ambaye alipata nafasi ya kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 tangu 2020 -2023

“Nataka nitumie fursa hii kuziagiza kamati za siasa za CCM nchi nzima, zikisaidiwa na kamati za maadili nchi nzima, kuwafuatilia wale ambao wameanza kuzungukazunguka kutafuta ubunge, udiwani, uenyekiti wa mtaa au kitongoji kuanzia sasa,” ameagiza Makamu Mwenyekiti na kuongeza:

“Hatuna nafasi ya kuhangaishwa na watu wanaotafuta uongozi kipindi hiki, wasubiri hadi mwezi wa saba mwaka 2025, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itaamua tarehe ya kwenda kuchukua fomu, kabla ya hapo unavunja kanuni".

Amesema mwana CCM asifikiri kwamba akianza kampeni kabla ya wakati, akapigiwa kura akawa wa kwanza, atapitishwa kugombea, hapana, hatapita.

"...alianza kampeni mapema, alitoa rushwa, alikivuruga Chama, hata upate kura za wajumbe wote hutapita," ameonya Ndugu Kinana.

Amebainisha kwamba, kuna vigezo vingi vinatazamwa zikiwamo; kura, uzingatiaji wa maadili na kanuni.

"Je, ulitoa rushwa, ulizingatia kanuni, uliwachafua viongozi wenzako walioko madarakani? Kwa hiyo unaweza ukawa wa kwanza lakini ukawa wa mwisho,” ametahadharisha.

Aidha, amewataka wanaccm wote kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ambao wana wajibu wa kutekeleza ahadi zilizotolewa na Chama kwa Watanzania.

View attachment 2741539View attachment 2741540View attachment 2741541View attachment 2741542View attachment 2741543View attachment 2741544View attachment 2741545View attachment 2741546
hayo ni maneno tu mzee.

Hakuna hatua mnachukua wala nini.

wachaeni watu watafute kujulikana mapema msiwatishe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom