Kinana: Wasaka majimbo kinyemela kubanwa

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
KINANA.jpeg

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameziagiza kamati za siasa za CCM, kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wanachama walioanza kupitapita kusaka ubunge na udiwani.

Amesema wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, utaratibu na miongozo ya uchaguzi ndani ya CCM.

Amesema kwamba watakaobainika hawatapitishwa na vikao vya maamuzi kugombea nafasi hizo, hata kama wataongoza katika kura za maoni.

Kinana ameyasema hayo leo Septemba 5, 2023, wilayani Hai, Kilimanjaro katika mkutano mkuu wa jimbo la Hai, uliohusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, jimboni humo.

“Nataka nitumie fursa hii kuziagiza kamati za siasa za CCM nchi nzima, zikisaidiwa na kamati za maadili nchi nzima, kuwafuatilia wale ambao wameanza kuzungukazunguka kutafuta ubunge, udiwani, uenyekiti wa mtaa au kitongoji kuanzia sasa,” ameagiza Makamu Mwenyekiti na kuongeza:

“Hatuna nafasi ya kuhangaishwa na watu wanaotafuta uongozi kipindi hiki, wasubiri hadi mwezi wa saba mwaka 2025, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itaamua tarehe ya kwenda kuchukua fomu, kabla ya hapo unavunja kanuni".

Amesema mwana CCM asifikiri kwamba akianza kampeni kabla ya wakati, akapigiwa kura akawa wa kwanza, atapitishwa kugombea, hapana, hatapita.

"...alianza kampeni mapema, alitoa rushwa, alikivuruga Chama, hata upate kura za wajumbe wote hutapita," ameonya Ndugu Kinana.

Amebainisha kwamba, kuna vigezo vingi vinatazamwa zikiwamo; kura, uzingatiaji wa maadili na kanuni.

"Je, ulitoa rushwa, ulizingatia kanuni, uliwachafua viongozi wenzako walioko madarakani? Kwa hiyo unaweza ukawa wa kwanza lakini ukawa wa mwisho,” ametahadharisha.

Aidha amewataka wanaccm wote kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ambao wana wajibu wa kutekeleza ahadi zilizotolewa na Chama kwa Watanzania.
== ==
 
Wanayasaka na hamna cha kuwafanya mlisema wavue magamba nani alivua? CCM haina meno wajanja wanapita nyumba kwa nyumba
 
Loophole hiyo hapo,ya kwamba ulikua wa kwanza,ila ulikiuka kanuni,hivyo tunampitisha wa tatu.CHADEMA huo ni mwanya kwenu.Wakipitisha ambaye hatakiwi,kama kipindi cha JPM,inakua rahisi kwenu,kumshinda,kwani atakua na maadui ndani na nje ya chama.
 
Kuna raia mtaani unawaona kabisa wazalendo na wanaweza kutuwakisha bungeni lakini vyama vinatuwekea/kupitisha wasiostahili. Kuna haja ya kuwa na wagombea binafsi.
Kwanza wanakiuka katiba iliyotoa haki ya kuchagua na kichaguliwa
 
Loophole hiyo hapo,ya kwamba ulikua wa kwanza,ila ulikiuka kanuni,hivyo tunampitisha wa tatu.CHADEMA huo ni mwanya kwenu.Wakipitisha ambaye hatakiwi,kama kipindi cha JPM,inakua rahisi kwenu,kumshinda,kwani atakua na maadui ndani na nje ya chama.
Chadema/polisi/Tume,?
 
View attachment 2740198

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameziagiza kamati za siasa za CCM, kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wanachama walioanza kupitapita kusaka ubunge na udiwani.

Amesema wanaofanya hivyo wanakiuka kanuni, utaratibu na miongozo ya uchaguzi ndani ya CCM.

Amesema kwamba watakaobainika hawatapitishwa na vikao vya maamuzi kugombea nafasi hizo, hata kama wataongoza katika kura za maoni.

Kinana ameyasema hayo leo Septemba 5, 2023, wilayani Hai, Kilimanjaro katika mkutano mkuu wa jimbo la Hai, uliohusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, jimboni humo.

“Nataka nitumie fursa hii kuziagiza kamati za siasa za CCM nchi nzima, zikisaidiwa na kamati za maadili nchi nzima, kuwafuatilia wale ambao wameanza kuzungukazunguka kutafuta ubunge, udiwani, uenyekiti wa mtaa au kitongoji kuanzia sasa,” ameagiza Makamu Mwenyekiti na kuongeza:

“Hatuna nafasi ya kuhangaishwa na watu wanaotafuta uongozi kipindi hiki, wasubiri hadi mwezi wa saba mwaka 2025, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itaamua tarehe ya kwenda kuchukua fomu, kabla ya hapo unavunja kanuni".

Amesema mwana CCM asifikiri kwamba akianza kampeni kabla ya wakati, akapigiwa kura akawa wa kwanza, atapitishwa kugombea, hapana, hatapita.

"...alianza kampeni mapema, alitoa rushwa, alikivuruga Chama, hata upate kura za wajumbe wote hutapita," ameonya Ndugu Kinana.

Amebainisha kwamba, kuna vigezo vingi vinatazamwa zikiwamo; kura, uzingatiaji wa maadili na kanuni.

"Je, ulitoa rushwa, ulizingatia kanuni, uliwachafua viongozi wenzako walioko madarakani? Kwa hiyo unaweza ukawa wa kwanza lakini ukawa wa mwisho,” ametahadharisha.

Aidha amewataka wanaccm wote kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ambao wana wajibu wa kutekeleza ahadi zilizotolewa na Chama kwa Watanzania.
== ==
Kamati za siasa na
Kamati za maadili
Ambazo msingi wa kupatikana kwa wajumbe wake wengi ni kwa rushwa, sidhani kama wanamuelewa Kinana. Yaani mtu kauza shamba la ukoo ili akwae nafasi ndani ya chama halafu uanze kumueleza mbambamba za kupambana na rushwa za chaguzi za teuzi.......

Na hawatokaa wamuelewe.
 
Kwa sasa HAKUNA kiongozi wa CCM aliye CHAGULIWA. Wanafahamu Uchaguzi waliuvuruga wao CCM. Sasa iweje anyetafuta ridhaa ya wananchi, wamchague kwamba huyu ndiye tunayemtaka nyie mumkatae huyo, kwa maoni yenu mumkatae kwa sababu aliomba ridhaa ya wananch mapema. CCM lini ikafuata kanuni na taratibu? Nani asiyetoa rushwa ccm? Kwanini sasa rushwa isiwe kigezo kama wote mnapokea rushwa na kuliibia taifa.
Mlioko juu wezi, mafisadi walioko chini wanataka wawe kama nyie, nanyi HAMTAKI, hiyo siyo HAKI.
 
Back
Top Bottom