Kinana: Wakataeni wanaotumia udini, ukabila na ukanda kutaka uongozi

AFRIKAMOJA

Member
Aug 11, 2022
30
37
Ujiji, Kigoma
01 Septemba, 2022

Umoja na mshikamano wa watanzania na Taifa kwa ujumla ni masuala yaliyopewa kipaumbele kabla na baada ya uhuru kupitia vyama vya TANU na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya viongozi na waasisi wake hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Mara kadhaa siasa zenye mwelekeo wa kuwagawa watanzania zimeonekana kukemewa wazi wazi na viongozi wa Chama tawala CCM, wanataaluma wazalendo na waumini wote wa umoja.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omari Kinana akiongea katika kikao cha ndani cha kupokea taarifa za kazi za chama na serikali amesema CCM kimekuwa chama bora na kinachoungwa mkono na watanzania walio wengi kwa sababu nyingi ikiwemo kupinga ubaguzi wa aina zote na kuwaunganisha watanzania.

"CCM kupitia sera zake imejitambulisha kuwa chama kinachojali utu, usawa wa binadamu na umoja kwa maana ya kuunganisha watu pamoja na kupiga vita ubaguzi. Sasa nawashauri viongozi wenzangu, katika uchaguzi unaoendelea kote nchini wakateni viongozi wanaotumia udini, ukabila au ukanda kama sifa ya kupata uongozi maana hao hawafai kuongoza chama chetu. Tuwapime na kuwapa watu uongozi kwa kuzingatia uwezo, sifa na uadilifu wao na sio kwa misingi ya ubaguzi wa aina yoyote." Alisema Kinana

Kinana alilazimika kusema hayo baada ya kupewa taarifa ya kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya mkoa wa Kigoma iliyowasilishwa na Katibu wa CCM mkoa huo Ndg. Mobutu Malima iliyoeleza kumeanza kuibuka hisia za ukabila, udini na ukanda kutafuta uongozi katika uchaguzi unaoendelea ndani ya CCM mkoani humo.

Aidha Kinana amewataka wanachama na viongozi wa CCM Mkoani Kigoma kujua wanao wajibu wa msingi wa kusema na kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi unaofanywa na serikali ya CCM Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ili wananchi wajue nini serikali yao inafanya.

Kinana yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kuimarisha chama, kukagua utekelezaji wa ilani na kusikiliza kero za wananchi akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.

IMG-20220901-WA0076.jpg
 
Na wake wanaowabeza watanzania kwa kigezo cha kuwaita wanyonge ,mbona hajasema tuwakatae?
 
..kauli ya Mzee Kinana ni sawa na kuwaelekeza Watz waikatae Ccm.

..huenda Mzee Kinana amechanganyikiwa, au chama chake kimekosa hoja za kuwavutia wananchi.
Tanzania tuliruhusu ubaguzi wa kiitikadi na mahali Fulani wa kikanda na pengine viwango vya ukabila tulishafika na yote hata yalisababishwa au yaliletwa na ccm.Hivi Leo wapo wanaoteseka magerezani kisa ubaguzi wa kiitikadi wa CCM.Nivyema mkatubu Dhambi hii Kwa uwazi mbele ya Watanzania,Kwani watanzania ni wasikovu.Baada ya kutubu msisahau kurejea viapi vyenu,"Ewe Mwenyezi Mungu naomba unisaidie"
 
Back
Top Bottom