Kinana na timu yake waingia Jimbo la Singida Magharibi, wahutubia katika vijiji mbali mbali.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195

Mwanakwaya akiimba kwa kuonesha ishara ya vidole ya Serikali mbili zatosha katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Sepuka, Jimbo la Singida Magharibi, Wilaya mpya ya Ikungi, mkoani Singida

Wasanii wakicheza ngoma ya beni wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Igombwe wakati wa ziara ya Kinana wilayani Ikungi, ambapo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutegemea misaada, bali watumie nguvu na maarifa yao kujiletea maendeleo.

Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Sepuka, wilayani Ikungi, Jimbo la Singida Magharibi, ambapo aliwataka wananchi wa jimbo hilo walioambukizwa tabia na wenzao wa Jimbo la Singida Mashariki ya kukataa kuchangia fedha za miradi ya maendeleo wakiambiwa fedha zote za miradi zitolewe na serikali. Sumu hiyo inadaiwa kuenezwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alisikitishwa na tabia hiyo na kuwataka wananchi kumpuuza mbunge huyo na kujikita kwenye maendeleo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Sepuka, ambapo aliwataka wananchi kuipenda CCM inayowaletea maendeleo badala ya vyama vya upinzani ambavyo havisaidii kabisa katika masuala ya miradi ya maendeleo bali wanaishia kupiga makelele na kutoa matusi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Sepuka, wilayani Ikungi

Wafuasi na wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii cha CCM wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Igombwe, ambapo baadhi walikabidhiwa kadi na Kinana baada ya kujiunga na CCMKatibu Mkuu wa CCM, Kinana akizindua mashina la wakereketwa wa CCM, moja nila Vijana waendesha pikipiki Puma, wilayani Ikungi huku jingine ni shina la wakereketwa la CCM la Puma, wilayani Ikungi. Shina hilo awali lilikuwa na CHADEMA.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mohamed Misanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Zahanati ya Mnang'ana, iliyopo Kata ya Sepuka, wilaya mpya ya Ikungi ambapo Misanga alisema kuwa jengo hilo lilisimama kwa muda mrefu bila kujengwa baada ya wanachi kukataa kuchangia fedha. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana.

Kinana akisaidia kujenga jengo la CCM katika Kijiji cha Igombwe wakati wa ziara yake katika Jimbo la Singida Magharibi la Mbunge Mohamed Misanga.

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia baada ya kufungua tawi la CCM la Wajasiriamali Wanawake katika Kijiji cha Puma, wilayani Ikungi leo.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekemea vitendo vya baadhi ya wabunge kuwakataza wananchi kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao kwani tabia hiyo inadhoofisha juhudi za Serikali kupambana na umasikini.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema hayo alipohutubia wananchi wa kijiji cha Makiungu, wilayani Ikungi kwenye mkutano wa kwanza wa hadhara katika Jimbo pekee lenye Mbunge wa upinzani mkoani Singida la Singida Mashariki.

Kinana alitoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na kujionea miradi ilioshindwa kukamilika kutokana na Mbunge wa Jimbo hilo, Tundu Lissu kuzuia wananchi wa maeneo husika kuchangia nguvu na fedha zao katika sehemu ya gharama ya miradi hiyo.

“Kazi ya Mbunge ni kuongoza watu wake kujiletea maendeleo, lakini huyu wenu anakwamisha maendeleo. Anawakataza nyie kuchangia, mambo yenu yanadorora lakini ya kwake yananyooka,” alisema Kinana na kuongeza;

“Nawasihi ndugu zangu msisikilize ushauri wa aina hiyo, unawaumiza, mtu anayekupa ushauri mbaya ujue kakudharau, hivyo mpuuzeni na amueni sasa kuanza kuchangia maendeleo yenu vinginevyo mtaendelea kubaki nyuma wakati wenzenu wanaenda mbele.”

Kinana amewatahadharisha vijana dhidi ya wanasiasa wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa na kuwataka wajishughulishe zaidi na kazi mbalimbali za ujasiriamali badala ya kuendekeza porojo
 
DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,614
2,000
Vp kwa vile MISSANGA ubunge wake ni miaka 15,tatizo sugu la maji limekwisha,umeme umeenea kuliko Singida Mashariki?

Kwa kuwa jimbo la Singida Mashariki kuna Upungufu wa walimu kutokana na kutawaliwa na cdm TUNDU, Huko magharibi kwa ccm Missang hakuna shida ya walimu.

Gongo imepanda bei IKUNGI.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
kwa sasa UKAWA ndiyo habari ya mujini,hawa majangili ni wa kupuuza tu!
Ndugu, ninakubaliana na wewe kwa sababu kikundi kinachojiita UKAWA kinaenda pekee kwenye sehemu ambazo ni makao makuu ya Mkoa.

Kwa sasa CCM ndiyo habari ya Tanzania kama taifa. Huhitaji kuambiwa tazama kama picha zinavyokueleza.
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Ni mwelekeo mzuri tu wa ziara zisizo na maana. Kwani lengo ni kuzima moto unaowashwa na UKAWA!

Ila nilikuwa nafikiria jambo hapa "hivi kama kule mahali kwingine walikunywa gongo, Singida Mashariki wakavuna uwele na mtama, hapo Singida Magaribi si ingekuwa poa kama Kinana na Nape wangeendesha mbojo kidogo kuonyesha mshikamano wao na wananchi?" .....hata hivyo ni mawazo tu.....msinimaindi ndugu wananchi.
 
Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
16,558
2,000
Ndugu, ninakubaliana na wewe kwa sababu kikundi kinachojiita UKAWA kinaenda pekee kwenye sehemu ambazo ni makao makuu ya Mkoa.

Kwa sasa CCM ndiyo habari ya Tanzania kama taifa. Huhitaji kuambiwa tazama kama picha zinavyokueleza.

....mgodini hii kitu tuna semaga.... Tingisha Dunia shetani apewe talaka !!!

mkalli

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
225
0
Ndugu, ninakubaliana na wewe kwa sababu kikundi kinachojiita UKAWA kinaenda pekee kwenye sehemu ambazo ni makao makuu ya Mkoa.

Kwa sasa CCM ndiyo habari ya Tanzania kama taifa. Huhitaji kuambiwa tazama kama picha zinavyokueleza.

Hebu tutoe hofu kidogo Ccm wanafika kote huko ruzuku wanatoa wapi?
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Ni mwelekeo mzuri tu wa ziara zisizo na maana. Kwani lengo ni kuzima moto unaowashwa na UKAWA!

Ila nilikuwa nafikiria jambo hapa "hivi kama kule mahali kwingine walikunywa gongo, Singida Mashariki wakavuna uwele na mtama, hapo Singida Magaribi si ingekuwa poa kama Kinana na Nape wangeendesha mbojo kidogo kuonyesha mshikamano wao na wananchi?" .....hata hivyo ni mawazo tu.....msinimaindi ndugu wananchi.
Ndugu, Hayo ni mawazo yako yanayokubalika cross-section of so called UKAWA.

UKAWA wanajiandaa na mchakato wa Katiba, CCM wanajiandaa na uchaguzi wa Madiwani.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Hebu tutoe hofu kidogo Ccm wanafika kote huko ruzuku wanatoa wapi?
Ndugu, CCM inapata ruzuku kutoka hapa,
Mbali na CCM, vyama vingine, ambavyo vinapata ruzuku, baadhi vikilingana na vingine vikitofautiana sifa ya kupata ruzuku hiyo, ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP. Viwango vya mgawo wa ruzuku hiyo, vilitangazwa na Tendwa alipozungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ruzuku hiyo ilianza kutolewa na ofisi yake kwa vyama hivyo, kuanzia Novemba, baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 31, mwaka huu na ule uliofanyika baadaye katika baadhi ya majimbo kukamilisha uchaguzi huo.
“CCM imeshuka kwa ruzuku. Huko nyuma ilikuwa inapata Shilingi bilioni moja, lakini sasa inapata Sh. milioni 818,” alisema Tendwa.
 
ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,650
1,250
kinana namfananisha na timu ya liverpool,yeye anajifanya kushambulia wakati huku nyuma hajui amemwacha adui ukawa anamvizia amfunge,mwambien atapigwa counter attack,chezea mourinho (mbowe)
 
Kavunja

Senior Member
Apr 16, 2014
158
0
Kinana ni nani katika serikali, hadi apokelewe na wakurugenzi na kuwahoji watendaji wa serikali? kwani amewaajili yeye? kwanini anaingilia kazi za serikali na anaachwa? kinana anapomuhoji mtendaji wa serikali ni sawa na kumuhoji mwenyekiti wake kikwete ambaye ni mwajili na msimamizi mkuu wa utendaji. je, ni vyema kwa katibu wa chama kumuhoji mwenyekiti wake? huo ni usanii wa ccm
 
kingukitano

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,971

Serikali ni ya chama,gani,serikali,ni mpangaji mwenye nyumba ni CCM,kinana yuko sahihi
 
Ngaramu

JF-Expert Member
May 7, 2009
382
195

Mwanakwaya akiimba kwa kuonesha ishara ya vidole ya Serikali mbili zatosha katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Sepuka, Jimbo la Singida Magharibi, Wilaya mpya ya Ikungi, mkoani Singida

Wasanii wakicheza ngoma ya beni wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Igombwe wakati wa ziara ya Kinana wilayani Ikungi, ambapo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutegemea misaada, bali watumie nguvu na maarifa yao kujiletea maendeleo.

Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Sepuka, wilayani Ikungi, Jimbo la Singida Magharibi, ambapo aliwataka wananchi wa jimbo hilo walioambukizwa tabia na wenzao wa Jimbo la Singida Mashariki ya kukataa kuchangia fedha za miradi ya maendeleo wakiambiwa fedha zote za miradi zitolewe na serikali. Sumu hiyo inadaiwa kuenezwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alisikitishwa na tabia hiyo na kuwataka wananchi kumpuuza mbunge huyo na kujikita kwenye maendeleo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Sepuka, ambapo aliwataka wananchi kuipenda CCM inayowaletea maendeleo badala ya vyama vya upinzani ambavyo havisaidii kabisa katika masuala ya miradi ya maendeleo bali wanaishia kupiga makelele na kutoa matusi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Sepuka, wilayani Ikungi

Wafuasi na wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii cha CCM wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Igombwe, ambapo baadhi walikabidhiwa kadi na Kinana baada ya kujiunga na CCMKatibu Mkuu wa CCM, Kinana akizindua mashina la wakereketwa wa CCM, moja nila Vijana waendesha pikipiki Puma, wilayani Ikungi huku jingine ni shina la wakereketwa la CCM la Puma, wilayani Ikungi. Shina hilo awali lilikuwa na CHADEMA.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mohamed Misanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Zahanati ya Mnang'ana, iliyopo Kata ya Sepuka, wilaya mpya ya Ikungi ambapo Misanga alisema kuwa jengo hilo lilisimama kwa muda mrefu bila kujengwa baada ya wanachi kukataa kuchangia fedha. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana.

Kinana akisaidia kujenga jengo la CCM katika Kijiji cha Igombwe wakati wa ziara yake katika Jimbo la Singida Magharibi la Mbunge Mohamed Misanga.

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia baada ya kufungua tawi la CCM la Wajasiriamali Wanawake katika Kijiji cha Puma, wilayani Ikungi leo.

Hivi hao WATU (nyomi) wazidi mia moja (100) kweli!!!! Alaf kama wameandaliwa na MAJEZI ya KIJANI, sijui wamesombwa kutoka wapi leo. Nahisi itakua mpaka mikoa ya jirani.
 
Gwalihenzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
5,126
2,000
Ni mwelekeo mzuri tu wa ziara zisizo na maana. Kwani lengo ni kuzima moto unaowashwa na UKAWA!

Ila nilikuwa nafikiria jambo hapa "hivi kama kule mahali kwingine walikunywa gongo, Singida Mashariki wakavuna uwele na mtama, hapo Singida Magaribi si ingekuwa poa kama Kinana na Nape wangeendesha mbojo kidogo kuonyesha mshikamano wao na wananchi?" .....hata hivyo ni mawazo tu.....msinimaindi ndugu wananchi.
Duh!Elly B, hapo kwenye mbojo umenikumbusha zamani sana! watu wakitumia usafiri wa fisi, ha hah!!
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,783
2,000
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekemea vitendo vya baadhi ya wabunge kuwakataza wananchi kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao kwani tabia hiyo inadhoofisha juhudi za Serikali kupambana na umasikini.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema hayo alipohutubia wananchi wa kijiji cha Makiungu, wilayani Ikungi kwenye mkutano wa kwanza wa hadhara katika Jimbo pekee lenye Mbunge wa upinzani mkoani Singida la Singida Mashariki.

Kinana alitoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na kujionea miradi ilioshindwa kukamilika kutokana na Mbunge wa Jimbo hilo, Tundu Lissu kuzuia wananchi wa maeneo husika kuchangia nguvu na fedha zao katika sehemu ya gharama ya miradi hiyo.

“Kazi ya Mbunge ni kuongoza watu wake kujiletea maendeleo, lakini huyu wenu anakwamisha maendeleo. Anawakataza nyie kuchangia, mambo yenu yanadorora lakini ya kwake yananyooka,” alisema Kinana na kuongeza;

“Nawasihi ndugu zangu msisikilize ushauri wa aina hiyo, unawaumiza, mtu anayekupa ushauri mbaya ujue kakudharau, hivyo mpuuzeni na amueni sasa kuanza kuchangia maendeleo yenu vinginevyo mtaendelea kubaki nyuma wakati wenzenu wanaenda mbele.”

Kinana amewatahadharisha vijana dhidi ya wanasiasa wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa na kuwataka wajishughulishe zaidi na kazi mbalimbali za ujasiriamali badala ya kuendekeza porojo

CCM muache hadaa zenu hamtamuweza Lissu kwa porojo zenu hizi.Hakuna kiongozi yeyote ambaye ana weza kuwakataza watu kuchangia shughuli za maendeleo.Viongozi wengi na hasa wa upinzani wanachokifanya ni kuwaelimisha wananchi kuchangia shughuli za maendeleo kwa kiwango cha halali wanachojipangia wenyewe kulingana na uzito wa kazi wanayokusudia kuifanya na kusimamia michango wanayoitoa isitafunwe na mchwa.Hata hivyo kutokana na madai yenu kama ni ya kweli kuwa Lissu amewazuia watu wasichangie huduma za maendeleo na wao ambao ni wengi wamemsikiliza mtu mmoja basi musahau kulitwaa hilo jimbo kwani Lissu atawaagiza wanajimbo wasiichague CCM na wao kwa vile wanaonekana wanamtii sana Lissu hata pale ana poagiza mambo ya kipuuzi hawataichagua CCM.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom