Kinana na timu yake waingia Jimbo la Singida Magharibi, wahutubia katika vijiji mbali mbali.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekemea vitendo vya baadhi ya wabunge kuwakataza wananchi kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao kwani tabia hiyo inadhoofisha juhudi za Serikali kupambana na umasikini.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema hayo alipohutubia wananchi wa kijiji cha Makiungu, wilayani Ikungi kwenye mkutano wa kwanza wa hadhara katika Jimbo pekee lenye Mbunge wa upinzani mkoani Singida la Singida Mashariki.

Kinana alitoa kauli hiyo baada ya kuelezwa na kujionea miradi ilioshindwa kukamilika kutokana na Mbunge wa Jimbo hilo, Tundu Lissu kuzuia wananchi wa maeneo husika kuchangia nguvu na fedha zao katika sehemu ya gharama ya miradi hiyo.

"Kazi ya Mbunge ni kuongoza watu wake kujiletea maendeleo, lakini huyu wenu anakwamisha maendeleo. Anawakataza nyie kuchangia, mambo yenu yanadorora lakini ya kwake yananyooka," alisema Kinana na kuongeza;

"Nawasihi ndugu zangu msisikilize ushauri wa aina hiyo, unawaumiza, mtu anayekupa ushauri mbaya ujue kakudharau, hivyo mpuuzeni na amueni sasa kuanza kuchangia maendeleo yenu vinginevyo mtaendelea kubaki nyuma wakati wenzenu wanaenda mbele."

Kinana amewatahadharisha vijana dhidi ya wanasiasa wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa na kuwataka wajishughulishe zaidi na kazi mbalimbali za ujasiriamali badala ya kuendekeza porojo
pocha.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom