MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Mwanakwaya akiimba kwa kuonesha ishara ya vidole ya Serikali mbili zatosha katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Sepuka, Jimbo la Singida Magharibi, Wilaya mpya ya Ikungi, mkoani Singida
Wasanii wakicheza ngoma ya beni wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Igombwe wakati wa ziara ya Kinana wilayani Ikungi, ambapo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutegemea misaada, bali watumie nguvu na maarifa yao kujiletea maendeleo.
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Sepuka, wilayani Ikungi, Jimbo la Singida Magharibi, ambapo aliwataka wananchi wa jimbo hilo walioambukizwa tabia na wenzao wa Jimbo la Singida Mashariki ya kukataa kuchangia fedha za miradi ya maendeleo wakiambiwa fedha zote za miradi zitolewe na serikali. Sumu hiyo inadaiwa kuenezwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alisikitishwa na tabia hiyo na kuwataka wananchi kumpuuza mbunge huyo na kujikita kwenye maendeleo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Sepuka, ambapo aliwataka wananchi kuipenda CCM inayowaletea maendeleo badala ya vyama vya upinzani ambavyo havisaidii kabisa katika masuala ya miradi ya maendeleo bali wanaishia kupiga makelele na kutoa matusi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Sepuka, wilayani Ikungi
Wafuasi na wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii cha CCM wakati wa mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Igombwe, ambapo baadhi walikabidhiwa kadi na Kinana baada ya kujiunga na CCM
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizindua mashina la wakereketwa wa CCM, moja nila Vijana waendesha pikipiki Puma, wilayani Ikungi huku jingine ni shina la wakereketwa la CCM la Puma, wilayani Ikungi. Shina hilo awali lilikuwa na CHADEMA.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mohamed Misanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Zahanati ya Mnang'ana, iliyopo Kata ya Sepuka, wilaya mpya ya Ikungi ambapo Misanga alisema kuwa jengo hilo lilisimama kwa muda mrefu bila kujengwa baada ya wanachi kukataa kuchangia fedha. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana.
Kinana akisaidia kujenga jengo la CCM katika Kijiji cha Igombwe wakati wa ziara yake katika Jimbo la Singida Magharibi la Mbunge Mohamed Misanga.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia baada ya kufungua tawi la CCM la Wajasiriamali Wanawake katika Kijiji cha Puma, wilayani Ikungi leo.