Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Baada ya "wateule" wengine kushindwa kufua dafu mbele ya Mzee wa Monduli, sasa Nape na Kinana wanaonekana wakimnadi Migiro, kama the best alternative na kufuatia maagizo kutoka "juu".
Lakini Lowassa (akisaidiwa vyema na mafisadi wenzake), anaonekana bado atamuacha kwa mbali mama huyu kimvuto ndani ya muda mfupi.
Ndio maana Mwigulu akitambua hilo na akizingatia msemo kuwa "kama huwezi kuwashinda, basi jiunge nao", mapema ameamua kujiunga kambi ya Lowassa. Hii imemfanya kwa sasa kuwekwa pembeni kwenye ziara za akina Kinana.
Ugumu upo kwa Nape, ambaye anaamini kambi yake iliyokuwa chini ya akina Sitta itapeta kama mama Migiro akichukua, lakini kwa Kinana wataalamu wa mambo wanasema anacheza karata zake vizuri, akiuma na kupuliza kote kote.
Swali ni kwamba nini kitatokea kwa Nape na kundi lake siku mamvi akikabidhiwa rasmi bendera ya kijani kupigania kwenda magogoni?