Kinana kufunga barabara jijini Mwanza. Je, ni haki?

Kinana kufunga barabara jijini Mwanza. Je, ni haki?

Nyamwaga

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
454
Reaction score
118
Muda huu kumetokea msongomano wa magari barabara ya nyerere road kisa huyu katibu mkuu wa ccm akipita na polisi ( traffic) kufunga barabara, huku ikifahamika kuwa kinana ni katibu wa chama si wa kiserikali. Je huu ni usitaarabu kila kiongozi wa ccm kuleta adha kwa wananchi?.
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wameongoza makundi ya vijana kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu pamoja na makundi ya jogging vya mjini Mwanza kukimbia mchakamchaka (jogging) kwa umbali wa kilomita 8,kuanzia Barabara ya Stesheni,kupitia barabara ya Posta,Kenyatta, Karuta,Lumumba maeneo ya Soko Kuu mpaka Stendi ya zamani Tanganyika.

Viongozi mbali mbali walishiriki mchakamchaka huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo,Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Mansoor na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu pamoja na wananchi mbalimbali waliojiounga na mchakamchaka huo.

Wakati wa Jogging, shughuli nyingine zote ziliendelea kama kawaida kwani barabara hazikufungwa na magari ya abiria yaliendelea na kazi yake bila usumbufu wowote.,Vijana wa Mwanza wamesema ni kwa mara ya Kwanza wameweza kushiriki jogging na Kiongozi mkubwa kwa ngazi ya Kinana..wamempongeza Katibu Mkuu kwa ukaribu wake kwa vijana.

1.jpg

Katibu Mkuu Ndg Kinana akiwa kwenye mchaka mchakana Vijana wa Mwanza.

Muda huu kumetokea msongomano wa magari barabara ya nyerere road kisa huyu katibu mkuu wa ccm akipita na polisi ( traffic) kufunga barabara, huku ikifahamika kuwa kinana ni katibu wa chama si wa kiserikali. Je huu ni usitaarabu kila kiongozi wa ccm kuleta adha kwa wananchi?.

ni halali
 
Hii ni kuonyesha kuwa mwisho wa ccm unakarbia na ndo maana wanaanza ubabe wa kihitler
 
huko mwanza pia kuna mkuu wa mkoa kituko anatembea na msafara mrefu kuliko rais
 
Natamani kuona Edward Lowasa akijumuika na wananchi kufanya jogging. Sijui kama hataishia ICU
 
Waswahili watu wa ajabu kweli,yule anayewaulia tembo,amabye kampuni yake imekamatwa ikisafirisha meno kibao ya tembo container zima,wanaenendana naye...nchi hii acha tu waibiwe..kina....waibie mpaka wawe majizi....maana vichwa vyao vina makamasi.
 
Kweli anayeshabikia ccm ni haki alivyoandika hapo juu kamasi kamasi kamasi.
 
Hizo ni barabara zilizojengwa kutokana na Ilani ya CCM. Kinana ni Katibu Mkuu wa CCM
 
Ccm ni kama kuku aliye kwisha katwa kichwa kiwiliwili kikadai bado hakijafa
 
Mleta mada Ndugu Nyamwaga, yawezekana haya mambo ya jogging kwako ni mageni sana. Huku Dar tumeshayazoea hasa siku za jumamosi. Vijana kwa wazee wameunda vikundi /club za jogging ambapo hupita hukimbia barabarani kwa umbali hata wa kilomita 10 hadi 20. na hilo la usumbufu wa foleni huwa lipo ingawa si foleni kubwa sana.

DSC_0680.JPG

Wakali-Jogging-e1425618115300.jpg
 
Last edited by a moderator:
Natamani kuona Edward Lowasa akijumuika na wananchi kufanya jogging. Sijui kama hataishia ICU

Ha ha ha ha haa mbavu zangu uuuuuiiiiiiii duu, nadhani itabidi gari la wagonjwa liwe sm 5 karibu na tukaiyo
 
mwaka huu ccm watajikomba kwa wananchi had chooni, ha ha ha
 
Muda huu kumetokea msongomano wa magari barabara ya nyerere road kisa huyu katibu mkuu wa ccm akipita na polisi ( traffic) kufunga barabara, huku ikifahamika kuwa kinana ni katibu wa chama si wa kiserikali. Je huu ni usitaarabu kila kiongozi wa ccm kuleta adha kwa wananchi?.
Unashangaa katibu mkuu wa chama tawala kufunga "barabara ya nyerere road"? Huku pwani ukiwa na kigodoro chako au kaharusi uchwara unafunga barabara au mtaa siku hata mbili halafu unaporomosha bonge taarabu na baikoko kwa buku 10 tu. SEBUSE KINANA!
NB: barabara ya nyerere au sema Nyerere road.
 
Muda huu kumetokea msongomano wa magari barabara ya nyerere road kisa huyu katibu mkuu wa ccm akipita na polisi ( traffic) kufunga barabara, huku ikifahamika kuwa kinana ni katibu wa chama si wa kiserikali. Je huu ni usitaarabu kila kiongozi wa ccm kuleta adha kwa wananchi?.

ata dar jumamosi ; jogging tunafunga na magari yanasimama ;

kwa afya

Rudi na topic ya mkutano
 
Back
Top Bottom