Kinana atua Kigoma katika ziara ya kuimarisha chama

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
CDE KINANA ATUA KIGOMA KWA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu Abdulrahman Omari Kinana amewasili leo Alhamisi tarehe 01 Septemba, 2022 mkoani Kigoma kwa ziara ya siku moja mkoani humo ya kukagua uhai wa chama, utekelezaji wa ilani pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Kinana amewasili uwanja wa ndege wa Kigoma na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Ndg Amandus Dismas Nzamba, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Ndg Thobias Andengenye, wanachama na viongozi wa chama na serikali.

Kinana ameanza leo ziara ya siku moja mkoani Kigoma ambapo ataendelea katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza. Katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.

#CCMImara
#KaziIendelee
 

Attachments

  • IMG-20220901-WA0045(1).jpg
    IMG-20220901-WA0045(1).jpg
    101.9 KB · Views: 6
  • IMG-20220901-WA0044(1).jpg
    IMG-20220901-WA0044(1).jpg
    77.9 KB · Views: 6
  • IMG-20220901-WA0047(1).jpg
    IMG-20220901-WA0047(1).jpg
    83.7 KB · Views: 6
Ni aibu kwa Chama kilicho madarakani kuamini kwamba mikutano itawawezesha kuimarisha Chama!

Kutatua kero na manung'uniko ya watu ndio namna Bora kwa Chama tawala kuimarisha Chama!
 
Wanalamba asali huku wananchi wakibaki masikini wa kutupwa.

Wanejenga chama wakati wananchi wana manung'uniko.
Yupo kukagua utekelezaji wa ilani ya chama, Hapo tegemea Mambo mengi kupatiwa majibu, lakini pia tegemea kuona matumaini mapya kila atakapopagusa na kupazungumzia lazima papatiwe majibu na suluhisho la haraka ndani ya muda mfupi Sana

CCM Ni chama kiongozi, Ni chama kilichobeba matumaini na Imani kubwa Sana ya wananchi katika kuwaletea maendeleo,

CCM Ni chama kilichobeba na kutekeleza ajenda na Sera zinazogusa maisha ya watu hasa wanyonge wasio na sauti za kusikika,
 
Back
Top Bottom