Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Morogoro, Kanali Mtaafu Kinana alikubana na dhoruba la kuzomewa maeneo ya Ruaha, mpakani mwa wilaya ya Kilosa na Kilombero akielekea Ifakara na Mahenge.
Wananchi bila ya kuogopa chochote walipokea msafara wa CCM kwa zomea zomea ya mafisadi hao hatuwataki. Ndipo Kinana aliamua kuongea na wananchi wale, bila ajizi aliulizwa na mmoja wa wanainchi, Katibu wetu mkuu mbona kuna tuhuma wewe unahusika na uwindaji haramu na biashara ya meno ya Tembo?
Kinana kabla hajajibu alijadiliana kitu na Nnape kisha akajibu, "ndugu yangu najua wewe umetumwa, kama madai hayo yana ukweli basi nenda mahakamani" alijibu kwa jazba. Baadaye yule kijana alifuatwa na polisi kutakiwa akatoe maelezo kituo cha polisi kidatu. Alipofika polisi aliambiwa Nnape alitaka awekwe ndani sasa sisi hatuoni kosa la kukufungulia chaji wewe ondoka zako ila usiulize mambo ya kukera wakubwa.
Kama haitoshi walipofika mji mdogo wa Ifakara hawakupata mapokezi yeyote badala yake viongozi wa CCM walihangaika kununua wananchi kati ya shs 70,000 na 120,000 ili wakabidhiwe kadi na kuombwa wafungue matawi na kupandisha bendera za CCM, hivi sasa wananchi wale wameshusha na kuvunja mawe ya msingi. Wanadai pesa za CCM ni kuzila na Kura ni CDM. Mikakati ya uchaguzi wa Diwani kata ya Ifakara mjini imeanza kwa 100 % hawa CCM wataangukia pua.
Awali sikujua kama Kinana na yeye ni msanii, alijua kabisa wale wanainchi wamenunuliwa sasa kiko wapi bendera zimeshushwa? Huyu Katibu mkuu atumie muda wake kusafisha chama zidi ya Magamba yalomshinda Mukama
Wozoza - Mulongo Poteka