Kinana Atia Aibu CCM

Kinana Atia Aibu CCM

Masanilo

Platinum Member
Joined
Oct 2, 2007
Posts
22,282
Reaction score
4,556
Akiwa katika ziara ya kichama mkoani Morogoro, Kanali Mtaafu Kinana alikubana na dhoruba la kuzomewa maeneo ya Ruaha, mpakani mwa wilaya ya Kilosa na Kilombero akielekea Ifakara na Mahenge.

Wananchi bila ya kuogopa chochote walipokea msafara wa CCM kwa zomea zomea ya mafisadi hao hatuwataki. Ndipo Kinana aliamua kuongea na wananchi wale, bila ajizi aliulizwa na mmoja wa wanainchi, Katibu wetu mkuu mbona kuna tuhuma wewe unahusika na uwindaji haramu na biashara ya meno ya Tembo?

Kinana kabla hajajibu alijadiliana kitu na Nnape kisha akajibu, "ndugu yangu najua wewe umetumwa, kama madai hayo yana ukweli basi nenda mahakamani" alijibu kwa jazba. Baadaye yule kijana alifuatwa na polisi kutakiwa akatoe maelezo kituo cha polisi kidatu. Alipofika polisi aliambiwa Nnape alitaka awekwe ndani sasa sisi hatuoni kosa la kukufungulia chaji wewe ondoka zako ila usiulize mambo ya kukera wakubwa.

Kama haitoshi walipofika mji mdogo wa Ifakara hawakupata mapokezi yeyote badala yake viongozi wa CCM walihangaika kununua wananchi kati ya shs 70,000 na 120,000 ili wakabidhiwe kadi na kuombwa wafungue matawi na kupandisha bendera za CCM, hivi sasa wananchi wale wameshusha na kuvunja mawe ya msingi. Wanadai pesa za CCM ni kuzila na Kura ni CDM. Mikakati ya uchaguzi wa Diwani kata ya Ifakara mjini imeanza kwa 100 % hawa CCM wataangukia pua.

Awali sikujua kama Kinana na yeye ni msanii, alijua kabisa wale wanainchi wamenunuliwa sasa kiko wapi bendera zimeshushwa? Huyu Katibu mkuu atumie muda wake kusafisha chama zidi ya Magamba yalomshinda Mukama

Wozoza - Mulongo Poteka
 
Hivi unajisikiaje pale unapoongoza/kutawala wananchi ambao wanakuchukia, hawakutaki tena uwatawale na hawakupendi... Hapa tulipofikia sasa inabidi tuanze kuwapopoa na mawe kabisa ili wajue hatuwataki...
 
Awali sikijua kama Kinana na yeye ni msanii, alijua kabisa wale wananchi wamenunuliwa sasa kiko wapi bendera zimeshushwa? Huyu Katibu mkuu atumie muda wake kusafisha chama zidi ya Magamba yalomshinda Mukama

Wozoza - Mulongo Poteka
Hivi wewe AWALI kwako ina maana gani?.

Mabandiko yako yanaonyesha tokea Kinana awe Katibu Mkuu wa CCM umeendelea kumponda mpaka dakika hii tunaposoma bandiko lako.

Hii kazi huiwezi, waachie wengine ambao ni magwiji wa propaganda waendelee nayo kwa sababu bandiko lako linadhihirisha jinsi ulivyo mweupe na kichanga katika ulingo wa siasa.

Wewe kwa akili zako hizi za chekechea unaweza kutoa ushauri kwa Kinana?. You must be joking.

Hata hicho kitengo cha mitandaoni cha CHADEMA hukitendei haki.

Kwa ushauri nasaha, Kazi unayofanya hapa ni zaidi ya uwezo wako!!
 
mkuu dr slaa aliwahi sema kweny mkutano pale ruaha ccm wakitaka kununua kadi zenu muwauzie tena kwa bei kubwa lakin kura chadema nadhan wana ifakara walikuwa wanatimiza hayo ccm wenyew walidhani wamepata hahaha
R.I.P ccm
 
Hivi wewe AWALI kwako ina maana gani?.

Mabandiko yako yanaonyesha tokea Kinana awe Katibu Mkuu wa CCM umeendelea kumponda mpaka dakika hii tunaposoma bandiko lako.

Hii kazi huiwezi, waachie wengine ambao ni magwiji wa propaganda waendelee nayo kwa sababu bandiko lako linadhihirisha jinsi ulivyo mweupe na kichanga katika ulingo wa siasa.

Wewe kwa akili zako hizi za chekechea unaweza kutoa ushauri kwa Kinana?. You must be joking.

Hata hicho kitengo cha mitandaoni cha CHADEMA hukitendei haki.

Kwa ushauri nasaha, Kazi unayofanya hapa ni zaidi ya uwezo wako!!

Kinana is a joker, I can prove that.
 
Acha porojo, message has been sent and received at the right time "Kinana is the source of all evils".
 
Hivi unajisikiaje pale unapoongoza/kutawala wananchi ambao wanakuchukia, hawakutaki tena uwatawale na hawakupendi... Hapa tulipofikia sasa inabidi tuanze kuwapopoa na mawe kabisa ili wajue hatuwataki...

Tangulini Mwizi anafikiri zaidi ya kunyata,kodokoa, kujificha na kutumia mali za watu! Viongozi wengi wa TZ ni wezi, hawana utu wala muda wa kufikiri wewe unawaonaje.
 
Huyu Kinana ni mtu hatari sana, ila cha kufurahisha CCM (Nape, Kinana na magamba wengine) pamoja na dola wamefyata mikia baada ya kusikia makamanda waliosimamishwa bungeni wanashitaki kwa wananchi, sasa hivi kimyaaaaaaaaaa, aibu tu maana wanajua jamaa wanaenda kuwaeleza wananchi ukweli, wanajuta kwa nini wamewasimamisha bungeni sababu imeleta madhara makubwa dhidi ya ccm kiasi kwamba wanagombana wenyewe kwa wenyewe!
 
Mbunge wa Morogoro Mjini, Aboud bila aibu alidanganya wananchi mbele ya Kinana amechimba visima 23, ajabu hivyo visima ni changa la macho. Akiomba avionyeshe itakuwa aibu
 
Hivi wewe AWALI kwako ina maana gani?.

Mabandiko yako yanaonyesha tokea Kinana awe Katibu Mkuu wa CCM umeendelea kumponda mpaka dakika hii tunaposoma bandiko lako.

Hii kazi huiwezi, waachie wengine ambao ni magwiji wa propaganda waendelee nayo kwa sababu bandiko lako linadhihirisha jinsi ulivyo mweupe na kichanga katika ulingo wa siasa.

Wewe kwa akili zako hizi za chekechea unaweza kutoa ushauri kwa Kinana?. You must be joking.

Hata hicho kitengo cha mitandaoni cha CHADEMA hukitendei haki.

Kwa ushauri nasaha, Kazi unayofanya hapa ni zaidi ya uwezo wako!!

we ulipewa training pale Lumumba??maana inawezekana umepitia kabisa mafunzo ya propaganda chafu za mtandaoni wakati hiku vijana wa Cdm ni wazalendo wanaopambana na nyie mafisadi MwanaDiwani
 
Last edited by a moderator:
Hii yote ni kukosa uwajibikaji ,angekubali kuikana nafsi yake ,akakaa nyumbani kwake kama alivyofanya mkama angeheshimika.kichwa ngumu ,tia maji!!!
 
Allah! Kumbe hata ziara huko Ifakara ni katika pita pita karibu na mbuga ya Mikumi Mzee wa Tembo!!!
 
Thread mufilisi.

Sent from my hp EliteBook 8460p using JamiiForums
 
JF raha sana. Unakurupuka muda wowote unatunga story unaiweka Jukwaani.

Sent from my hp EliteBook 8460p using JamiiForums
 
Back
Top Bottom