Kinana amsafishia njia Mbowe 2015

Kinana amsafishia njia Mbowe 2015

lumumba the son

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2011
Posts
207
Reaction score
60
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinanaamemsafishia njia mbunge wa jimbo la Hai na Mwenyekiti wa kambi yaUpinzani bungeni Mhe. Freeman Mbowe kwa kuzindua miradi ya maendeleojimboni humo na kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabiliwananchi wa jimbo la Hai.

Kinanaambaye yuko Mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya Mikoa mitatuikiwemo Dodoma, Arusha na Kilimanjaro, amefika wilaya ya Hai nakuzindua miradi ya maendeleo ikiwemo kuchangia ujenzi wa shule yamsingi Modio kwa kutoa bati zaidi ya 300 na mifuko ya Cement, iliyopoMasama Mashariki jirani kabisa na kijiji alichozaliwa Mbunge wa Jimbohilo eneo la Machame, iliyopatwa na janga la tetemeko na kubomoka nambunge wa Jimbo hilo kushindwa kuchangia ujenzi kwa muda wote ambaoshule hiyo imepatwa na janga.

Lakinipia Katibu Mkuu ameshiriki ujenzi wa Daraja la MNEPO katika Kitongojicha Kiyungi, daraja la Mnepo ambalo limejengwa kwa waya limekuwalikitumika kwa zaidi ya miaka 30 kuunganisha vijiji viwili vyaKiyungi na Migongweni, na watu wengi kupata kwani daraja hilolimekuwa likikatika mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa namauti kwa wananchi wa vijiji hivyo.

Kinanapia amekagua Ujenzi wa Chumba cha X – ray ya Hospitali ya Wilaya yaHai, Kilimanjaro, na kuhimiza kuharakisha ujenzi huo ili kusaidiakuokoa maisha ya watu yanayopotea kwa kukosa huduma ya X – rayhospitalini hapo.

Kinanaanaendelea na Ziara yake leo katika Wilaya ya Moshi na kukagua nakuhimiza utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa jimbo la moshi vijijini.
 

Attachments

  • 3 (5).jpg
    3 (5).jpg
    67.9 KB · Views: 1,256
  • 5 (3).jpg
    5 (3).jpg
    62.1 KB · Views: 1,224
  • 7 (1).jpg
    7 (1).jpg
    53.2 KB · Views: 1,198
  • 23 (1).jpg
    23 (1).jpg
    43.9 KB · Views: 1,210
  • 9 (2).jpg
    9 (2).jpg
    84.2 KB · Views: 1,228
Ndugu yangu ulisoma shule gani?!! hebu rudia kusoma na kuhalili ili mtu aweze kuelewa ulichoandika, wewe ni mwenyeji wa Kilimanjari kweli mkoa wenye elimu !!?
 
We umeona kafanya nini hapo????yaani hizo bati 300 zilizotokana na ESCROL ndo umeona diiiiili,fuatilia vizuri aliyoyafanya Mbowe kabla ya kupiga tararira hapa dada
Kazi ipo mwaka huu..,Mwenyekiti wa Chadema anashindwa kufanya kazi zake mpaka Katibu Mkuu wa CCM akafanye kwa niaba yake..kweli CCM ndio baba wa wote.
 
We umeona kafanya nini hapo????yaani hizo bati 300 zilizotokana na ESCROL ndo umeona diiiiili,fuatilia vizuri aliyoyafanya Mbowe kabla ya kupiga tararira hapa dada

Ndio wale wale..,sasa wewe kama unayajua aliyoyafanya mbowe si uyaseme sasa..?
 
We nawe unaacha kujadili kilichoandikwa unaanza na mwandishi, suala la uenyeji wa Kilimanjaro linaingiaje hapa..?
Mama usinitafutie ban bure, umezoea sana kuwajibia wenzako kama ulivomjibia NAPE na ukawa umeharibu zaidi. Nitajadilije kitu ambacho sikukielewa?!!
 
Kazi ipo mwaka huu..,Mwenyekiti wa Chadema anashindwa kufanya kazi zake mpaka Katibu Mkuu wa CCM akafanye kwa niaba yake..kweli CCM ndio baba wa wote.

aliyekwambia mbowe ni mjenzi nani ??
 
Kazi ipo mwaka huu..,Mwenyekiti wa Chadema anashindwa kufanya kazi zake mpaka Katibu Mkuu wa CCM akafanye kwa niaba yake..kweli CCM ndio baba wa wote.

Acha ujinga wewe. Mbunge hastahili kufanya hiyo kazi. Wananchi wanalipa kodi hivyo hiyo ni kazi ya serikali ambayo inakusanya kodi kutoka kwa wananchi hao. Mbunge hakusanyi kodi kutoka kwa wananchi, unataka pesa mfukoni mwake ilihali nyie na shoga zako mnafisadi pesa za kodi za hao wananchi. Pumbavu kabisa.

Nilifikiri una akili kumbe ni kopo kabisa. Mbunge anafanya hayo kwa bajeti kutoka wapi? Kutoka mfukoni mwake wakati chama chako kinachukua kodi ya hao wananchi na kugawana.

Dada yangu tumia akili japo kidogo acha ushabiki usio kuwa na maana.
 
Wewe msifie huyo Kinana ila usiponde pasipopondeka,kwani bila kumension CHADEMA post yako haiwezi kamilika???Namna gani Juliana wewe
Kwani chadema ni nani hata wasitajwe..? Ndio maana Nape anawaambia mmeingia kucheza ngoma msiyoijua.,mmeingia kwenye siasa na hamtaki kutajwa.,nyie ni gani aisee..?
 
Back
Top Bottom