Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,507
Mmh, Siasa za Tanzania bana. "Weka mbali na tembo" ndiyo nani?.Si mimi ninayesema, bali ni maneno yake mwenyewe Peter msigwa kwenye twitter yake. Nimeitafuta Twit yake na kuwawekea hapa.
Kinana ni JANGILI tena anayepaswa KUNYONGWA MPAKA KUFA.
Tembo anauwa anavyotaka halafu leo serikali inamchekea . . .
Mahakama ndo imewasafisha Mburura wewe, Unless useme Mahakama haina akili
KWA WATU WENYE KUANGALIA MBALI nafikiti issue ya igunga haimu tena kwenye vichwa vyao kwani mahakama chini ya utwala wa chama tawala imeisha litolea hukumu! 2+1=3 na siyo 4 !!
huna akili, kesi bado zipo mahaka;ani zinaendelea. Mnalisha watu sumu na kuwamwagia tindikali... Lazima mle miaka wahuni nyie
unachama kweli wewe au uchafu..ccm chama..poor thinkerTumpe hongera Kinana kwa kumfikisha mahakamani huyo mropokaji, kiukweli kwa kuropoka kwake kuhusu Kinana, hata chama changu kilichafuka sana.
WanaJF!
Katibu mkuu wa CCM, bwana Kinana, amefanya kweli kwa kuitimiza dhamira yake ya kumpeleka mchungaji Msigwa mahakamani endapo mchungaji huyo atakaidi fursa ya kumuomba radhi bwana Kinana.
Bwana Kinana alitoa fursa hiyo ya kuombwa radhi kufuatia kuchafuliwa taswira yake kwenye jamii, baada ya kudaiwa kuwa yeye ana jihusisha na masuala ya ujangili, jambo ambalo amelikanusha vikali.
Mchungaji Msigwa ameonekana mahakamani siku ya tar 14 akiwa na mawakili Tundu Lissu na Bwana Kibatala kama watetezi wa upande wa mshtakiwa.
My take,
Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana kesi hii ya kumshtaki mchungaji Msigwa kwa tabia yake ya kuropoka ovyo ovyo. Shukrani bwana kinana kwa hatua uliyo chukua. Sasa kazi kwa Msigwa kuthibitisha tuhuma zake za ujangili kwa bwana Kinana.
Kweli mkuu,
Hakuna gazeti lolote lililotoa hii taarifa, ila ukweli ni kwamba Kinana amefungua mashtaka dhidi ya Msigwa rasmi. Habari zaidi nitaendelea kuweka, na kama kuna mtu anaweza kuzileta pia itakuwa ni jambo jemba kwa maslahi ya wanaJF wote.
Mkuu, sidhani kama Kinana angukuwa na ujasiri wa kwenda mahakamani na kufungua mashtaka kwa Msigwa kama kweli angekuwa jangili au kujihusisha na vitendo hivyo kwa nama yoyote ile.
Mahakama zetu hazijapata kansa ya kisiasa kama polisi na usalama wa taifa, na ninatumaini zitatoa hukumu ambayo ni fair for all.
Kesi hii itatupatia mwanga kuhusu yaliyoko ndani ya biashara hii haramu ya nyara za serikali.
Hapa ndiyo tutajua mbivu na mbichi kwa sababu sheria hazina siasa wakati siasa mara nyingi hazina sheria.
Mkuu bigaraone , Ninashukuru kwa kuliona hilo jambo kama ulivyoainisha hapo juu.A very good input na iliyoenda shule. Mimi nashangaa wanaomtukana Msigwa katika hili ingawa sisemi alikuwa sahii kumhusisha Kinana. Lakini huenda hii kesi ikatusaidia sana na labda ika set precedent kwenye sharia zinaratibu different industries ili kutoa loophole ya watu kurushiana mpira mambo yapoharibika na kuchukua sifa mambo yakienda vizuri. Nina imani kama Kinana mdau kwenye usafiri wa vyombo au chombo cha majini kilichosafirisha meno ya ndovu ingetokea ikafichuliwa au kuzuiwa kusafirishwa kwa meno hayo, hivi tungekuwa tunasema vingine. Hata kampuni ingekuwa ni moja zilizotoa ushirikiano au sio leo angetaka sifa zote ziende kwake. Sasa kwa kuwa hakuzuia na kampuni yake imehusika kwa nafasi yake kama wakala tunahitaji sheria hizi zirekebishwe ili ziende na wakati kuzuia mdau mmoja kuacha uovu ufanyike kwa kisingizio cha wajibu wangu ni mwingine
Mkuu, sidhani kama Kinana angukuwa na ujasiri wa kwenda mahakamani na kufungua mashtaka kwa Msigwa kama kweli angekuwa jangili au kujihusisha na vitendo hivyo kwa nama yoyote ile.
Leo wanampigia makofi kinana kuwa anajitambua.Hongera Msigwa kwa kuzuia ubia wa kifisadi wa Kinana..hapo hata mahakama haiwezi kumsafisha
Mkuu vipi leo..wewe hupigi vigeregere?Hakuna muarobaini wala nini.. Kinana haramia la kisomali,jangili la tembo wetu.. Linyongwe tu!
Nasikia baada ya miaka 7 leo mchungaji ameungama
Inawezekana mkuu.Labda kinana amesajiliwa Chadema wanamsafisha