Wasilalamike, ni wazi kuwa CCM ndiyo imeasisi, kubariki na kuachia utaratibu wa viongozi kujiamulia kufanya wanayotaka. Ni serikali ya CCM iliyotupa kando uwajibikaji na maadili ya viongozi wa umma. Ni CCM na viongozi wake waliofikia hatua ya kuzidharau sheria na kukiuka katiba ya nchi kwa manufaa yao.
CCM ni chama pekee ambapo watu wenye kashfa za ubakaji kama Prof. Kapuya wanaweza kupeta na vyeo vyao bila kubughudhiwa na yeyote. Ni katika CCM ambapo kiongozi anayetuhumiwa na umma anaweza kugombea uongozi wa umma huku akipigiwa kampeni na Mwenyekiti wa chama hicho bila aibu!
Tena ni katika CCM na serikali yake ambapo kiongozi anaweza kuwaamuru polisi au jeshi kuvunja sheria na kutoheshimu katiba, na asiulizwe na yeyoye. Ni katika serikali ya CCM ambapo wahalifu wateule kama Kamuhanda wanaweza kupandishwa vyeo, pamoja na mauaji waliyoyasimamia kuwa na ushahidi wa wazi!
Kwani wao walitegemea nini kutokana na chama chao? Tell them to sit tight. Katika CCM kila kisichowezekana kwingineko kinawezekana kwao. Kila kisichoruhusiwa kwingine ndani ya CCM ni ruksa!
Neno moja lenye maana sawa na maelezo yako yote ni 'Mbugi '