Kinana aivuruga Lumumba

Kinana aivuruga Lumumba

Kuna sintofahamu katika Ofisi Ndogo za CCM-Lumumba kuhusu ziara zinazoendelea za Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana. Patashika hiyo ya kichama ni kuhusu hasa timu inayoambatana na Kinana katika ziara za mikoani.Makada waandamizi wa Lumumba wanadai kuwa ziara za Kinana hazilengi kuimarisha chama kama zinavyoonekena ila ni kujitangaza na kuwatangaza anaoambatana nao ili kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwakani.

"Werevu tunajua.Katibu Mkuu na timu yake wako katika kujitangaza na kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Hakuna jipya ambalo wanalifanya. Ndiyo maana hata timu yake haibadiliki.Ni kwamba amechagua vijana wa kuwatangaza na wengine kuwatenga. Kwanini timu haibadiliki? Kwani nani hawezi kuhutubia na nani hataki posho?" aliuliza kwa kulalama kada mmoja maarufu aliyehamia CCM katika miaka ya karibuni.

"Ziara za Katibu Mkuu zitaleta ubaguzi chamani na mpasuko usio na maana. Chama hakiimarishwi na watu wale wale kila siku.Kila kada anaweza kwenda mikoani na kukitangaza chama. Kwanini wale wale hata kama wanaonekana kusema mambo ya kawaida sana? Tunajiandaa kuchukua hatua juu ya hili" alidakia kada mwingine wa Ofisi Ndogo Lumumba

Nionavyo,lengo kuu ni posho na umaarufu. Kumbe!??

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Hii post ukiisoma kwa ndani ni uoga kutoka upande wa pili wa shilingi kwa maana ukawa and companies,kama mtakuwa wafuatiliaji kuna kipindi mzee kinana aliposhila ukatibu mkuu alifanya ziara mbili na baadaye kukaa kimya,wengi mlijitokeza na kuhoji ziara za kinana zipo wapi ? Hali hiyo ilijitokeza kwa kudhani ilikuwa nguvu ya soda,sasa inawatisha wengi,kinana anapiga kazi maeneo mbalimbali,anakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuwasilikiza wananchi.Amefanikiwa kuibua ari ya wana ccm kutambua wajibu wao na hii itasaidia hata katika ngazi nyingine za mikoa na wilaya mpaka kata na matawini viongozi wa ccm kufanya majukumu yao na kutokana na kuwa chama chenye mtandao mpana na madhubuti,itakuwa ni vigumu kwa vyama vya ushindani kupenyeza umbeya na propaganda katika jamii
 
Kinana na timu yake waendelea na ziara katika vijiji mbali mbali na kuhutubia umati wa watu, Sikonge
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kabla ya kufanya mkutano mkubwa alizungumza na vijana wa Kijiji cha Vijana cha Path Finder Green Village alipotembelea na kukagua miradi mbalimbali iliyopo katika kijiji hicho chenye jumla ya vijana 88. Kijiji hicho kiko umbali wa Km 40 kutoka Sikonge Mjini. Katibu Mkuu yuko katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata IIani ya uchaguzi ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.


Kijiji hicho kinaendesha miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi vijana, ufugaji kuku, ufugaji nyuki, kilimo, kujifunza ufundi wa aina mbalimbali..


Kijiji hicho kimenzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa kwa lengo la kuwapunguzia umasikini vijana waliokosa fulsa ya elimu wilayani humo.


Akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM,wilayani Sikonge mkoani Tabora, Kinana alizungumzia matatizo makubwa yanayowakumba wakulima wa zao la Tumbaku huku akionesha kabrasha la taarifa ya ukaguzi na uchunguzi wa chama cha Ushirika cha WETCO LTD,ambalo linaeleza namna wakulima wa Tumbaku walivyoibiwa mamilioni ya fedha.


Aidha,Wananchi wa Sikonge wameulalamikia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha uliofanywa na viongozi wa vyama vya ushirika,na kwamba wamekuwa wakicheleweshewa malipo ya fedha zao na pia kutolipwa kwa wakati,jambo ambalo limekuwa likiwakera wakulima hao.


Kinana aliongeza kusema kuwa vyama vya ushirika vimeanzishwa kwa wingi na wajanja wachache kwa ajili ya kujinufaisha wao na kuwanyona na kuwadhuruma wakulima wa Tumbaku, hivyo Kinana alisema kuwa amekisikia kilio cha wakulima hao,na ameahidi kuyafikisha malalamiko hayo kwa Rais Jakaya Kikwete na hatimaye kupatiwa ufumbuzi wa haraka.










Katibu Mkuu, Kinana akihutubia umati wa watu katika uwanja wa CCM, Sikonge.




Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia umati wa watu.


Mbunge wa jimbo la Sikonge, Said Mkumba akiwaeleza wananchi kuhusu mafanikio na malengo yaliyoko mbeleni katika kutimiza ahadi kama zilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM.






Kwa vile ndani ya CCM kuna upendo na furaha, huu ulikuwa ni muda wa kufurahia na kuburudika baada ya mkutano uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.










Baadhi ya vijana wapatao 70 katika kijiji cha PathFinder Green City,wilayani Sikonge,mkoani Tabora. Wakimweleza Kinana kuhusiana na mafanikio na changamoto katika miradi yao mbali mbali ya kujitegemea.






Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisaidia kufunga tumbaku huku akisaidiwa na mmoja wa vijana wa Kituo cha Vjana cha Path Finder Green Village, wilayani Sikonge, Tabora.


ZeMarcopolo likes this.
 
image.jpg image.jpg
 
kwani huyo kinana Posho za ujangili hazimtoshi? kwa nn asitulie ofisini? Au ndo anapita kukagua biashara zake?

Jama huyo anapokuwa ziarani anakuwa ameenda kuchukua mzigo wa tembo!
 
Hakuna rangi mtaacha kuona mwaka huu, jembe kinana linazidi kuwapasua vichwa kwa utendaji makini na wa kukubalika kwa wananchi maskini...
 
Oooh!

Watu makini pia wameshaanza kuhoji kuhusu unafiki wa wazi unaofanywa kwenye ziara hizo tena kwa kukebehi na kudharau wananchi.
 
Oooh!

Watu makini pia wameshaanza kuhoji kuhusu unafiki wa wazi unaofanywa kwenye ziara hizo tena kwa kukebehi na kudharau wananchi.
Makini zaidi wanahoji ukwapuaji wa ruzuku unaofanywa na mbowe kisha anaenda kununulia majumba dubai, unaofanywa na slaa kisha anaenda kuvinjari ulaya na hawara yake mama junior
 
Kinana huwa anambeba sana Nape.
Mwigulu anawabeba sana Mtela na Shonza juliana
Ccm ni makundi kila mahali
 
Cdm kaeni pembeni ligi imewashinda sasa mmeanza fitina acheni wenye nchi tuvinjari
 
Na yeye anaukodolea Urais kwa nguvu zote ili maslahi yake yaendelee kudumu hadi tembo watakapoisha ambapo imekadiriwa ni kama miaka 6 au 7 ijayo!

Angezunguka kutetea kurudishwa kwa Azimio la Arusha tungemuelewa na kumpenda vilevile
 
aliyelalamika atakua ni mwampamba huyo,maana posho ndio zilizompeleka huko
 
Kwanini Kinana anajitangaza ili iweje? Naye anataka kuwania u-RAIS wa JMT?
 
Kinana huwa anambeba sana Nape.
Mwigulu anawabeba sana Mtela na Shonza juliana
Ccm ni makundi kila mahali

Mwigulu kumbeba Juliana tunafahamu malengo yake. Lakini hili la Kinana kumbeba Nape! kwani huwa anamfanya/anafanyiwa nini?
 
Back
Top Bottom